58-018 YESU-Bora Kuliko Musa (Waebrania 3:1-6)

YESU: “BORA ZAIDI KULIKO MUSA”

Utangulizi (Waebrania 3:1a)

 1. Kwa hiyo,
 2. Nafasi ya Musa akilini mwa Waebrania

Sifa za Wasikilizaji: Waebrania (Waebrania 3:1b)

 1. Ndugu Watakatifu,
 2. Wenye Kuushiriki Mwito Wa Mbinguni,

Ushauri Unaotolewa (Waebrania 3:1c)

 1. Mtafakarini sana Mtume
 2. Mtafakarini sana Kuhani Mkuu wa Maungamo Yetu,
 3. Mtafakarini sana Yesu Kristo

Kwa nini tumtafakari Yesu? (Waebrania 3:2 a)

 1. Yeye (Mungu Mwana) alikuwa Mwaminifu Kwake
 2. Yeye (Mungu Baba) aliyemteua

Kwa nini Kristo ni bora zaidi kuliko Musa? (Waebrania 3:2-6)

 1. Ofisi Yake ni bora zaidi: Kristo Kama Mungu
 2. Kazi Yake ni bora zaidi: Kristo-Mjenzi
 3. Uaminifu Wake ni bora zaidi: Trustworthy
 4. Uhusiano Wake na Nyumba/ Familia ya Mungu.
 5. Mtu Wake ni bora zaidi: Kristo Kama Mwana

MWITO WA KUDUMU KUKAA KATIKA NYUMBA YA KRISTO (Waebrania 3:6a-c)

 1. Bali Kristo, kama Mwana,
 2. Juu ya Nyumba ya Mungu;
 3. Ambaye Nyumba Yake ni sisi,

Tufanye Nini Basi (What must we do)? (Waebrania 3:6 d)

 1. Tukishikamane sana
 2. Tushikamane kwa ujasiri wetu
 3. Tusisahau “fahari ya taraja letu”
 4. Tumtafakari Yesu “Mpaka Mwisho”.

BWANA ATUBARIKI SOTE


 

Waebrania 3:1-6

1 Kwa hiyo, ndugu watakatifu, wenye kuushiriki mwito wa mbinguni, mtafakarini sana Mtume na Kuhani Mkuu wa maungamo yetu, Yesu,
2 aliyekuwa mwaminifu kwake yeye aliyemweka, kama Musa naye alivyokuwa, katika nyumba yote ya Mungu.
3 Kwa maana huyo amehesabiwa kuwa amestahili utukufu zaidi kuliko Musa, kama vile yeye aitengenezaye nyumba alivyo na heshima zaidi ya hiyo nyumba.
4 Maana kila nyumba imetengenezwa na mtu; ila yeye aliyevitengeneza vitu vyote ni Mungu.
5 Na Musa kweli alikuwa mwaminifu katika nyumba yote ya Mungu kama mtumishi, awe ushuhuda wa mambo yatakayonenwa baadaye;
6 bali Kristo, kama mwana, juu ya nyumba ya Mungu; ambaye nyumba yake ni sisi, kama tukishikamana sana na ujasiri wetu na fahari ya taraja letu mpaka mwisho.


 

NZK #139. Uliniimbie Tena

 • Sing them over again

  1. Uliniimbie tena, Neno la uzima;
  Uzuri wake nione, Neno la uzima;
  Neno hili zuri, lafundisha kweli:

  Maneno ya uzima ni maneno mazuri,
  Manemo ya uzima ni naneno mazuri.

  2. Kristo anatupa sote, Neno la uzima:
  Mwenye dhambi asikie Neno la uzima:
  Latolewa bure, Tupate wokovu:

  3. Neno tamu la Injili, neno la uzima;
  Mwenye dhambi asikie Neno la uzima:
  Litatutakasa, kwa haki ya Mwana: