58-010 YESU – Mtakasaji Wetu (Heb 2:11a)

Waebrania 2:11-13

 • 11 Maana Yeye Atakasaye na hao wanaotakaswa wote pia watoka kwa Mmoja. Kwa ajili hii haoni haya kuwaita ndugu Zake;
 • 12 akisema, Nitalihubiri Jina Lako kwa ndugu zangu; Katikati ya kanisa nitakuimbia sifa.
 • 13 Na tena, Nitakuwa nimemtumaini yeye. Na tena, Tazama,mimi nipo hapa na watoto niliopewa na Mungu.

 

Injili Ya Asubuhi ya Leo

 • Jumapili:      28 -8 -2016
 • Fungu Kuu: Waebrania 2:11a
 • Neno Kuu:   Utakaso:  ἁγιάζω (hagiazō)
 • 58-010:       YESU- “MTAKASAJI WETU”

Muhtasari wa Somo

 • Utangulizi: Neno “Utakaso”
 • Matumizi ya Neno “Utakaso” katika Biblia

MASWALI MUHIMU KATIKA INJILI YA LEO

 • Yeye Atakasaye (Nani anatoa utakaso)?
 • Na hao wanaotakaswa (nani wanatakaswa)?
 • Sayansi ya Utakaso huu: “wote pia watoka kwa Mmoja”.
 • Je, katika ubinadamu Wake, Kristo Alitakaswa?
 • Kama ndiyo, ni kwa Njia gani na kwa Jinsi gani?
 • Je, sisi nasi twaweza kutakaswa Leo?

MATOKEO YA UTAKASO HUU:

 • (11b) Kwa ajili hii “Haoni Haya Kuwaita Ndugu Zake”;
 • (12a) akisema, Nitalihubiri Jina Lako kwa ndugu Zangu;
 • (12b) Katikati ya kanisa Nitakuimbia Sifa.
 • (13a) Na tena, Nitakuwa Nimemtumaini Yeye.
 • (13b) Na tena, “Tazama,mimi nipo hapa na watoto niliopewa na Mungu”.

Bwana Atubariki Sote


Utakaso ni nini?

 • Mchakato wa upya na kuwekwa wakfu ambapo waumini hufanywa watakatifu kupitia kazi ya Roho Mtakatifu. Utakaso ni matokeo ya Kuhesabiwa Haki na utegemezi wa mtu kuwa kwenye mahusiano sahihi na Mungu.

 

UTAKASO UMEJENGWA KATIKA UTAKATIFU WA MUNGU

 1. Mungu ni Mtakatifu
  1. Ezekieli 39: 7; Na jina langu takatifu nitalifanya kuwa limejulika kati ya watu wangu Israeli; wala sitaliacha jina langu takatifu kutiwa unajisi tena; nao mataifa watajua ya kuwa mimi ndimi Bwana, na Aliye Mtakatifu katika Israeli.
  2. Walawi 22:32; Wala msilinajisi jina langu takatifu; lakini nitatakaswa mimi katika wana wa Israeli; mimi ndimi Bwana niwatakasaye ninyi,
 1. Mungu anahitaji watu Wake wautafakari Utakatifu Wake
  1. Walawi 19:2; Nena na mkutano wote wa wana wa Israeli, uwaambie, Mtakuwa watakatifu; kwa kuwa mimi Bwana, Mungu wenu, ni mtakatifu.
  2. 1 Petro 1:15-16; (15) bali kama yeye aliyewaita alivyo mtakatifu, ninyi nanyi iweni watakatifu katika mwenendo wenu wote; (16) kwa maana imeandikwa, Mtakuwa watakatifu kwa kuwa mimi ni mtakatifu.

 

MSINGI WA UTAKASO

Utakaso unajengwa kwa Uchaguzi wa Mungu kwa watu Wake, Yaani: Alituchagua kwanza.

 • 1 Cor 1:1-2(1) Paulo, aliyeitwa kuwa mtume wa Yesu Kristo kwa mapenzi ya Mungu, na Sosthene ndugu yetu, (2) kwa kanisa la Mungu lililoko Korintho, wale waliotakaswa katika Kristo Yesu, walioitwa wawe watakatifu, pamoja na wote wanaoliitia jina la Bwana wetu Yesu Kristo kila mahali, Bwana wao na wetu.
 • Waefeso 1:4-11;
  • 4 kama vile alivyotuchagua katika yeye kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu, ili tuwe watakatifu, watu wasio na hatia mbele zake katika pendo.
  • 5 Kwa kuwa alitangulia kutuchagua, ili tufanywe wanawe kwa njia ya Yesu Kristo, sawasawa na uradhi wa mapenzi yake.
  • 6 Na usifiwe utukufu wa neema yake, ambayo ametuneemesha katika huyo Mpendwa.
  • 7 Katika yeye huyo, kwa damu yake, tunao ukombozi wetu, masamaha ya dhambi, sawasawa na wingi wa neema yake.
  • 8 Naye alituzidishia hiyo katika hekima yote na ujuzi;
  • 9 akiisha kutujulisha siri ya mapenzi yake, sawasawa na uradhi wake, alioukusudia katika yeye huyo.
  • 10 Yaani, kuleta madaraka ya wakati mkamilifu atavijumlisha vitu vyote katika Kristo, vitu vya mbinguni na vitu vya duniani pia. Naam, katika yeye huyo;
  • 11 na ndani yake sisi nasi tulifanywa urithi, huku tukichaguliwa tangu awali sawasawa na kusudi lake yeye, ambaye hufanya mambo yote kwa shauri la mapenzi yake.
 • 1 Wathesalonike 5:9 Kwa kuwa Mungu hakutuweka kwa hasira yake, bali tupate wokovu, kwa Bwana wetu Yesu Kristo;

Kifo cha Upatanisho wa Yesu Kristo: (The Atoning Sacrifice)

 • Waebrania 13:12; Kwa ajili hii YESU naye, ili Awatakase watu kwa Damu Yake Mwenyewe, aliteswa nje ya lango.
 • Ro 6:11; 7:4; 8:2; 1 Co 1:30; 6:11; Efe 5:25-27; Ebr 10:10-14; 1 Pet 2:5

Neema ya Mungu

 • 2 Timotheo 1:9; ambaye Alituokoa Akatuita kwa Mwito Mtakatifu, si kwa kadiri ya matendo yetu sisi, bali kwa kadiri ya Makusudi Yake Yeye na Neema Yake. NEEMA HIYO TULIPEWA KATIKA KRISTO YESU tangu milele,

Kazi ya Mungu -Roho Mtakatifu

 • Warumi 15:16; 
  • 15 Lakini nawaandikia, kwa ujasiri zaidi katika sehemu za waraka huu, kana kwamba kuwakumbusha, kwa neema ile niliyopewa na Mungu,
  • 16 ili niwe mhudumu wa KRISTO YESU kati ya watu wa Mataifa, niifanyie Injili ya Mungu kazi ya ukuhani, kusudi Mataifa wawe sadaka yenye kibali, ikiisha kutakaswa na ROHO MTAKATIFU.
 • 2 Wathesalonike 2:13;  Lakini imetupasa sisi kumshukuru Mungu sikuzote kwa ajili yenu, ndugu mliopendwa na BWANA, kwa kuwa MUNGU amewachagua tangu mwanzo mpate wokovu, katika KUTAKASWA NA ROHO, na KUIAMINI KWELI;
 • 1 Pero 1:2; kama vile MUNGU BABA alivyotangulia kuwajua katika KUTAKASWA NA ROHO, hata mkapata kutii na kununyiziwa damu ya Yesu Kristo. Neema na amani na ziongezwe kwenu.

Neno la Mungu

 • Yohana 17:17;Uwatakase kwa ile KWELI; Neno Lako Ndiyo
 • Waefeso 5:25-26; (25) Enyi waume, wapendeni wake zenu, kama Kristo naye alivyolipenda Kanisa, akajitoa kwa ajili yake; (26) ili makusudi alitakase na kulisafisha kwa maji katika NENO;
 • 2 Timotheo 3:16; (16) Kila andiko, lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya watu makosa yao, na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadibisha katika haki; (17) ili mtu wa Mungu awe kamili, amekamilishwa apate kutenda kila tendo jema.

 

Hitaji La Utakaso

Dhambi ya asili ya Mwanadamu

 • Isaya 64: 6; Kwa maana sisi sote tumekuwa kama mtu aliye mchafu, na matendo yetu yote ya haki yamekuwa kama nguo iliyotiwa unajisi; sisi sote twanyauka kama jani, na maovu yetu yatuondoa, kama upepo uondoavyo.
 • Ayubu 15:14-15;
 • Zaburi 51: 5;  Tazama, mimi naliumbwa katika hali ya uovu; Mama yangu alinichukua mimba hatiani.
 • Warumi 5:12-19;
 • Waefeso 2:3

Utumwa wa dhambi waweza tu kuvunjwa kwa kupitia kifo cha Yesu Kristo

 • Yohana 8:34-36
 • Warumi 6:16-18; 8:5-7;
 • Waefeso 4:17-24

Haja ya kufanywa UPYA na UKUAJI wa kiroho

 • 2 Petro 3:18
 • 1 Wathesalonike 4:3-6;
 • Waebrania 6:1-3
 • Warumi 12:1-2; (1) Basi, ndugu zangu, nawasihi, kwa huruma zake Mungu, ITOENI MIILI YENU iwe dhabihu iliyo hai, takatifu, ya kumpendeza Mungu, ndiyo ibada yenu yenye maana. (2) Wala msiifuatishe namna ya dunia hii; bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu, mpate kujua hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema, ya kumpendeza, na ukamilifu.
 • Wakolosai 1:10; mwenende kama ulivyo wajibu wenu kwa Bwana, mkimpendeza kabisa; mkizaa matunda kwa kila kazi njema, na kuzidi katika maarifa ya Mungu;

 

Asili Ya Utakaso

Mchakato ambao tayari umeshaanzishwa katika maisha ya Muumini

 • 1 Wakorintho 1:2; 6:11

Mchakato wa ukuaji katika utakatifu

 • Warumi 12:1-3;
 • 2 Wakorintho 3:18;
 • Waefeso 4:15;
 • 1 Wathesalonike 4:3-7;
 • Waebrania 12:14;
 • 1 Petro 2:1-3;
 • 2 Petro 3:18

Kuwekwa wakfu kwa Mungu

 • Kutoka 32: 29;
 • 1 Nyakati 29: 5;
 • Mithali 23:26;
 • Warumi 12:1

 

MAPENZI YA MUNGU NI YAPI KWAKO?

Utakaso ni mapenzi ya Mungu kwa watu wake

 • 1 Wathesalonike 4:3; Maana haya ndiyo mapenzi ya Mungu, kutakaswa kwenu, mwepukane na uasherati;
 • Waefeso 1:4; kama vile alivyotuchagua katika yeye kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu, ili tuwe watakatifu, watu wasio na hatia mbele zake katika pendo.
 • Waefeso 2:10; Maana tu kazi yake, tuliumbwa katika Kristo Yesu, tutende matendo mema, ambayo tokea awali Mungu aliyatengeneza ili tuenende nayo.
 • Efesians 2:10 (NKJV); For we are His workmanship, created in Christ Jesus for good works, which God prepared beforehand that we should walk in them.