58-008 YESU: Mbadala wetu (Waebrania 2:9)


 

CHRIST: OUR SUBSTITUTE

  • YESU: MBADALA WETU
  • Fungu Kuu: Waebrania 1:9

Maswali muhumu Leo:

  1. Je, umewahi kuchukua nafasi kumshukuru KRISTO kwa kuchukua nafasi yako (badala yako) pale Kalvari?
  2. Je, ina maana gani kuwa YESU alikuwa Mbadala wetu?
  3. Je, Fungu hili la Waebrania 2:9 lina maana gani?

Hata leo (2016) kuna wengi sana ambao hawajaelewa fundisho hili la Waebrania.

Ni ombi langu kwamba kwa Neema ya MUNGU, utaelewa maana ya somo hili.

Bwana Atubariki sote


d17

Waebrania 2:9-11

9 ila twamwona yeye aliyefanywa mdogo punde kuliko malaika, yaani, Yesu, kwa sababu ya maumivu ya mauti, amevikwa taji ya utukufu na heshima, ili kwa neema ya Mungu aionje mauti kwa ajili ya kila mtu.
10 Kwa kuwa ilimpasa yeye, ambaye kwa ajili yake na kwa njia yake vitu vyote vimekuwapo, akileta wana wengi waufikilie utukufu, kumkamilisha kiongozi mkuu wa wokovu wao kwa njia ya mateso.
11 Maana yeye atakasaye na hao wanaotakaswa wote pia watoka kwa mmoja. Kwa ajili hii haoni haya kuwaita ndugu zake;


NZK # 144: Ni Wako Bwana
       (I am Thine O Lord)

1. Ni wako Bwana, ninasikia Unaponena nami;
Lakini, kweli, nataka kwako Nizidi kusongea.

Bwana vuta, (vuta) nije nisongee
Sana kwako mtini.
Bwana, vuta, vuta, nije nisongee
Pa damu ya thamani.

2. Niweke sasa nikatumike kwa nguvu za neema;
Uyapendayo nami nipende Nizidi kukwandama.

3. Nina furaha tele kila saa nizungumzapo nawe;
Ninanena kama kwa rafiki Nikipiga magoti.