58-006 Upendo wa Yesu Kristo (Waebrania 2:5-8)

Marudio: Waebrania 2:1-4

 • 1 Kwa hiyo imetupasa kuyaangalia zaidi hayo yaliyosikiwa tusije tukayakosa.
  2 Kwa maana, ikiwa lile neno lililonenwa na malaika lilikuwa imara, na kila kosa na uasi ulipata ujira wa haki,
  3 sisi je! Tutapataje kupona, tusipojali wokovu mkuu namna hii? Ambao kwanza ulinenwa na Bwana, kisha ukathibitika kwetu na wale waliosikia;
  4 Mungu naye akishuhudu pamoja nao kwa ishara na ajabu na nguvu za namna nyingi, na kwa magawanyo ya Roho Mtakatifu, kama alivyopenda mwenyewe.

Somo la Leo: Waebrania 2:5-8

 • 5 Maana hakuuweka chini ya malaika ulimwengu ule ujao tunaounena, ila mtu mmoja ameshuhudia hivi mahali fulani, akisema,
  6 Mwanadamu ni nini hata umkumbuke, Ama mwana wa binadamu, hata umwangalie?
  7 Umemfanya mdogo punde kuliko malaika, Umemvika taji ya utukufu na heshima, Umemtawaza juu ya kazi za mikono yako;
  8 Umeweka vitu vyote chini ya nyayo zake. Kwa maana katika kuweka vitu vyote chini yake hakusaza kitu kisichowekwa chini yake. Lakini sasa bado hatujaona vitu vyote kutiwa chini yake.

Hoja kuu muhimu katika somo la Leo:

 1. Utangulizi
 2. Upendo wa Yesu vs. Mwanadamu
 3. Asili ya Mwanadamu ni nini?
 4. Kwa nini mwanadamu alipoteza cheo alichopewa na Mungu?
 5. Mpango wa Mwanadamu kurejeshwa cheo alichokuwa nacho awali
 6. Upendo wa Yesu Kristo.