7-31-2016

KARIBUNI KATIKA IBADA YA ASUBUHI

Vipindi vya Asubuhi

 1. Maombi/Amka na Bwana (Nyimbo)
 2. Masomo Maalum ya Asubuhi
 3. Kitabu cha Waebrania

Toa Sifa & Shukrani kwa MUNGU wako, kwa:

 1. Tabia Yake isiyobadilika
 2. Baraka tele & Uaminifu Wake kwetu
 3. Msamaha wa dhambi zetu
 4. Nafasi nyingine ya uhai leo, n.k.

MADA KUU KATIKA MAOMBI YA LEO

 • Ufalme wa Mbinguni (Jumapili)
 • Tuombe ili tuwe Raia wa Ufalme wa Mungu

WAGONJWA WETU

 1. Dada Dorotea

CHANGAMOTO ZINGINE

 1. Patrick anapitia changamoto ngumu sana.

USHUHUDA WA LEO

 1. Ndugu mmoja tuliyekua tukimwombea apone ugonjwa wa Kansa, taarifa zinasema amepona.

Tunakaribishwa kufanya yafuatayo:

 1. Ushuhuda wa Matendo makuu ya Mungu
 2. Kuomba, na kuweka sala humu (sauti/ maandishi)
 3. Kutujulisha kama ombi lako limejibiwa

Karibuni sasa katika Chumba Cha Maombi

 • July 31, 2016
 • Yeyote anayeguswa kuwa katika Timu ya Maombi atujulishe tafadhali.
 • Bwana Atubariki sote.

 

 

TUOMBE WAPENDWA.

“Ee Bwana, fadhili zako zafika hata mbinguni, Uaminifu wako hata mawinguni. Haki yako ni kama milima ya Mungu, Hukumu zako ni vilindi vikuu, Ee Bwana, unawaokoa wanadamu na wanyama. Ee Mungu, jinsi zilivyo na thamani fadhili zako! Wanadamu huukimbilia uvuli wa mbawa zako”.
Baba yetu na Mungu wetu Mpendwa, Jina lako na lihimidiwe milele. Asante Bwana kwa nafasi nyingine ya Uhai. Asante kwa Tabia Yako isiyobadilika Bwana. Asante Bwana, kwa sababu wewe ndiwe MUNGU pekee. Tunakumbushwa katika maandiko kua Kristo Yesu ni “mng’ao wa utukufu Wako na Chapa ya nafsi Yako” maandiko yanaendelea kusema, huyu Kristo “akivichukua vyote kwa amri ya Uweza Wake, Akiisha kufanya Utakaso wa dhambi, Aliketi mkono wa Kuume wa Ukuu huko juu”. Asante kwa hilo, Bwana.

Baba asante kwa sababu Yesu Anatawala Milele Zote. Tusaidie siku hii ya Leo tuwe wafuasi Wake, tuwe waumini wa kweli, tutambue utupu wetu na udhambi wetu na tuje kwake na Maungamo na Toba za kweli. Tusaidie pia ili tuige tabia ya Mbinguni: tuwe “Raia wa Ufalme wa MUNGU”
Ee Bwana tunaomba pia kwa ajili ya kila familia, kila shida, kila changamoto iliyoletwa kwako Bwana.

Tunakushukuru sana kwa kujibu ombi la ndugu yetu mmoja tuliyekua tukimwombea apone ugonjwa wa Kansa, na taarifa zinasema amepona. Asante kwa uponyaji huo. Dada yetu mwingine (Dorotea) bado anaumwa, kaka yetu (Patrick) anapitia changamoto katika maisha yake. Wasaidie hawa watoto wako, Bwana.

Ee Bwana, wana na binti Zako wanapoamka na kuliita Jina Lako sasa, ebu Usikie maombi yao toka katika Mlima wako Mtakatifu. Ebu uwe Mungu wetu, nasi tuwe watu wako leo.

Tumeomba haya tukiamini kua umesikia na utatenda sawasawa na Fadhili Zako. Ni katika Jina Pekee la Yesu Kristo aliye Bwana na Mwokozi wetu, Amina.