Amri ya Pili

Usijifanyie Sanamu ya Kuchonga

 

Kutoka 20:4-6 {Exodus 20:4-6)

4 Usijifanyie sanamu ya kuchonga, wala mfano wa kitu cho chote kilicho juu mbinguni, wala kilicho chini duniani, wala kilicho majini chini ya dunia.
5 Usivisujudie wala kuvitumikia; kwa kuwa mimi, Bwana, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu; nawapatiliza wana maovu ya baba zao, hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao, 6 nami nawarehemu maelfu elfu wanipendao, na kuzishika amri zangu.

z1