7-10-2016

Haleluya Baba na Mungu wetu wa mbinguni jina lako takatifu litukuzwe milele zote. Asante kwa nafasi nyingine umetupatia watoto wako, umetulinda cku nzima ya leo umetuepusha na hatari zote ukauhifadhi uhai wetu tunakurudishia sifa na shukrani Mungu wetu.

Baba yetu, wewe watujua tu dhaifu na wanyonge tutie nguvu katika udhaifu wetu na unyonge wetu Baba ili tuweze kusimama imara kutetea imani yetu nyakati zote. Mungu wetu, tumekutenda dhambi mno na ktk wenye dhambi cc ndio wakuu mno tusiostahili maana tumezama ktk lindi la dhambi, lkn Baba tumetambua uwezo wako kwa damu yako tunaomba utusamehe na utuoshe tuwe safi kisha tuwe huru. Tupatie uwezo utokao juu ili tuwe washindi wa dhambi, tupatie uwezo wa kutambua hila za shetani, tutegemeze ktk neno lako na Roho Mtakatifu atutie ktk kweli tukujue wewe Mungu wa kweli na Yesu kristo uliyemtuma, kisha tuandae kuurithi uzima wa milele cc na watoto wetu, wazazi wetu, ndugu jamaa na rafiki zetu.

Tunakuja kwako Mungu wetu kati yetu tunayo mahitaji kama kundi, lkn pia kwa mtu binafsi, yupo rafiki yetu anayo Changamoto ktk ndoa yake tunakuomba Yesu wewe ukiye muasisi wa taasisi hii takatifu uliyouanzisha mwenyewe nenda kaikarabati rejesha upendo ule wa zamani wakukuone weweuliye nguzo ya familia zetu, Bwana onesha ukuu wako na jamii inayowazunguka wakajue yupo Mungu wa kweli anaweza mambo yote.

Baba, tunayo mahitaji ktk kundi kwa ajili ya uinjilisti mikutano sehemu mbalimbali, bajeti ya biblia, bajeti ya vipaza sauti Mungu wetu tunaketa kwako mahitaji haya yafanikishe kwa utukufu wa jina lako.
Baba, kati yetu wapo wanafunzi tunawaleta miguuni pako tunakuomba kila wanapokulilia ktk mahitaji yao sikia maombi yao, watendee na mapenzi yako yatimizwe. Wengine wanahitaji Ada fungua milango ya mibaraka tenda yote kwa utukufu wa jina lako Mungu wetu.

Tunawaleta wagonjwa miguuni pako, Mungu wetu wewe ndie tabibu mkuu tunakusihi Yesu waguse ucku huu yumkini ni mchana, asbh ama jioni kule waliko lkn wewe unaweza kutenda wakati wowote jidhihirishe kwao wakuone utukufu wako ktk magonjwa yao na jina lako litukuzwe milele.

Neno lako linatuambia vijana wana nguvu ya kuifanya kazi yako, tunakuomba sana Yesu ujana wetu ukutukuze wewe Mungu wa mbinguni, tutumie vile upendavyo tuifanye kazi yako, tuimarishe ili tukawainarishe na ndugu zetu, ili ujapo Bwana utukute cc pamoja na wale watakaoamini kupitia neno lile ulilotukabidhi kuwapasha na kuwavuta kwako tukiwa tayari kukulaki mawinguni kwa shangwe kupaa nawe juu mbinguni.

Ni tumaini letu kuwa utatenda yote sawasawa na mapenzi yako kwani tumeomba kwa jina la Yesu aliye Bwana na mwokozi wa maisha amina.