7-5-2016

KARIBUNI KATIKA IBADA YA ASUBUHI

 • Saa 11 (Nyimbo za Injili)
 • Saa 12 (Maombi ya Jumla)
 • Saa 1   (Injili Ya Leo Asubuhi)

SIFA & SHUKRANI: Mshukuru MUNGU kwa:

 • Tabia yake isiyobadilika
 • Baraka tele & Uaminifu wake kwetu
 • Msamaha wa dhambi zetu
 • Nafasi nyingine ya Uhai Leo.

RATIBA YA MAOMBI SIKU HII YA LEO

 • Magonjwa, Mikosi, Vifo
 • Tujiandae pia kiroho kwa ajili ya Ratiba ya Mfungo Jumatano

WAGONJWA WETU

 • (Dada Noela) “wagonjwa wetu”
 • Babu mwenye Kansa ya Ini huko Kenya
 • Zaidi ya Majeruhi 200 (Uturuki, Istanbull Airport)
 • AJALI: ajali mbaya sana iliyohusisha mabasiyakampuni ya city boy. Yenye route ya Kahama – Dar.

CHANGAMOTO ZINGINE

 • (Dada Noela) “Nina changamoto ya kuabudu bado”
 • Tumwombee binti yangu (Kilingog3)
 • Makambi yanayoendea sasa sehemu mbalimbali
 • Bajeti ya Biblia, na vipaza Sauti
 • Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Iringa.
 • Tuwaombee vijana katika karne ya 21
 • (mdogo wa Br. Isaac) Madawa ya kulevya na bangi “kwa Sasa anaendelea vizuri, ila Kuna Saa zingine anakuwa kama akili yake haijakaa vizuri tumuombee”

Tuwakumbuke familia na ndugu waliopoteza maisha jana Kwa Mabasi kugogana na takribani watu 46 wamepoteza maisha, tuzikumbuke familia zao hasa katika kipindi hiki kigumu

KAMPENI ZA INJILI (USA & Zimbabwe)

 • Tuombee pia campeni za kununua Biblia (TGV Bible Project)

USHUHUDA WA LEO: “Mungu hujibu maombi”

 • Tumekua tukimuombea Babu yake Mr. Wisley (huko Kenya); babu huyu aliyepelekwa Hospitalini wiki iliyopita, amepata nafuu na ameruhusiwa kurudi nyumbani.

AHADI YA LEO:  (Ufunuo 14:13)

 • Nikasikia sauti kutoka mbinguni ikisema, Andika, Heri wafu wafao katika Bwana tangu sasa. Naam, asema Roho, wapate kupumzika baada ya taabu zao; kwa kuwa matendo yao yafuatana nao.

TUNAKARIBISHWA KUFANYA YAFUATAYO:

 • Kutoa ushuhuda wa Matendo makuu ya MUNGU
 • Kuweka Maombi humu (Sauti/ Maandishi)
 • Kutujulisha kama ombi lako limejibiwa
 • Kushiriki kipindi kingine cha maombi ya Jioni (Saa 3 Usiku)

KARIBUNI KATIKA CHUMBA CHA MAOMBI ILI TUSHIRIKI IBADA YA MAOMBI YA JUMLA PAMOJA.

 • July 05, 2016
 • BWANA AWABARIKI.

Ombi hili limetolewa na ndugu:

 • Adovocate Kinja

Mungu wetu na Baba yetu unaetupenda upeo, jina lako takatifu litukuzwe milele. Tunakushukuru kwa namna ya pekee ambavyo unadhihirisha upendo wako kwetu, vile ambavyo matendo yako yalivyo makuu kwetu, ingawa hatukustahili kwa namna yyte kuwepo, lkn ni Neema na Rehema zako kwetu umetupatia nafasi nyingine ili tuweze kuzitanga Fadhili zako uhimidiwe milele na milele.

Mungu wetu, tumekutenda dhambi nyingi mno ktk kuwaza kunena na kutenda kwetu, hakuna jema lililoonekana kwetu, lkn bado uneshikilia uhai wetu, tusamehe Mungu wetu. Tunakuomba tupatie Roho Mtakatifu ili atutie ktk kweli za neno lako, atufundishe na atuongoze kuenenda sawasawa na mapenzi yako na tuweze kuiishi sheria yako takatifu ya upendo ambayo hutufunuliwa tabia yako ilivyo, sifa na shukrani vikurudie wewe ulie alfa na omega yaani mwanzo na mwisho.
Baba yetu wa mbinguni, sote ktk kundi hili tu wagonjwa wa kiroho na kimwili, tunakuhitaji mponya wetu. Mioyo yetu imejeruhiwa ina makovu huenda kwa sababu ya uchaguzi wetu mbaya, tunakuomba wewe ulie tabibu mkuu tuponye majeraha yetu uwezo wako wa kimbingu ukatuguse tupone, fufua fahamu zetu, tuundie moyo wa nyama tuweze kuiskia sauti yako na Roho Mtakatifu apate nafasi mioyoni mwetu akituongoza.

Wapo wagonjwa wa kimwili, Dada Noela, Baba alie na saratini ya ini, babu yake na Mr Wisley, Mr shayo, mshiriki mmoja kanisa la kigera. Mungu wetu wa mbinguni haya ni matokeo ya dhambi ndio maana tunateseka na magonjwa, na wale wengine waliopo mahospitalini na majumban wanateseka na maumivu, tunawaleta miguuni pako Yesu kwako wewe usiyeshindwa na jambo lolote bi wewe pekee unaeweza na ndio mana tunakuja kwako kaguse kila mmoja na hitaji lake kila panapouma, tunakuomba tenda hivyo kwa utukufu wa jina lako na watu wakashangae kwa matendo yako makuu. Pale uwezo wa kibinadamu unapoishia wewe ndipo unapojidhihirisha ili watu watambue kua wewe ni muweza tenda hivyo Mungu wetu.

Mungu wetu, Dada yetu noela anayo Changamoto ya kuabudu fungua njia maana wewe unafanya njia pasipo na njia anahitaji kukuabudu tunakuomba nyosha mkono wako ili aweze kukuabudu ktk Roho na kweli.

Tunaombea mikutano ya makambi kote ulimwenguni jifunue kwa watu wako kupitia watumishi uliowaita kufanya kazi yako pamoja nawe, wavute watu wako kwa kamba za pendo lako na Roho Mtakatifu awatie ktk hitaji la kukutana na mwokozi wa maisha yao na wajitoe ili waungane na kundi hili zuri. Lkn Baba tunawaombea watenda kazi ktk makambi hayo, wachungaji viongozi wa makambi na kwaya pamoja na washiriki ambao wapo kuhubiri kwa njia ya nyimbo watie nguvu ondoa vikwazo kwa kadiri wanavyojitoa bariki shughuli zao na kazi zao na kambi la mwaka huu let kawe mbaraka kwao na familia zao na jina lako litukuzwe.

Tunaomba kwa ajili ya bajeti ya biblia na vipaza sauti kwaajili ya mikutano inayoratibiwa na kundili hili, fungua milango ya mibaraka kwa watu wako ili tuweze kuisapoti kazi yako, peke yetu hatuzi bali kwa uwezo wako tutatenda makubwa, tujiweka miguuni pako tukikusihi utuwezeshe Mungu wwtu.

Mungu wetu, ktk maisha haya tunakutana na Changamoto nyingi lkn tunaamini kwa uwezo wako tutashinda. Wapo wanafunzi kule chuo cha Iringa wanakutana na Changamoto ya masomo cku ya sabato wanakulilia wewe ulie Bwana wa sabato watetee lkn imarisha imani zao kwako kisha wasimame kutetea imani zao, bila wewe haliwezekani jambo lolote tenda kwa utukufu wa jina lako.
Mungu wetu, ulimwengu upo kwenye karne ya utandawazi maadili yamepotoka na vijana wamezama huko, tunakuomba hata km iweje lkn lazima wawepo waliowaamini kwako, tunakuomba okoa kundi hili la vijana pasipo wewe kuingilia kati wengi watapotea tufundishe kwa njia ya Roho wako yule wa kweli atufunulie mapenzi yako tukugeukie na tudhamirie kute mema km mfalme Yosia japo alikua kijana wa miaka minane tu lkn aliadhimu kutenda mema nawe ukamfanya kuwa chombo chako, nasi pia vijana wa leo tuwezeshe kuazimu mioyoni mwetu kutenda mema tuwavute wengi kwako. Yupo mdogo ake Isaac tunamuweka miguuni pako unaijua hali yake kwa kupitia dawa anazotumia na ushauri anaoupata pamoja na uwezo wa kimbingu mrejeshe ktk hali yake ya awali kabla kutumia madawa hayo tulisifu jina lako Mungu wetu, tunaamini wewe ni muweza tenda hivyo Bwana.

Tunamuombea mama yule mjamzito, ni mapenzi yako uliwaunganisha mume na mke nao wakawa mwili mmoja nawe ukawapatia uwezo hadi kufikia hatua hiyo, Baba tafadhali fanikisha mama huyu ajifungue Salama lisiwepo la kuzuia bali zoez hilo lifanyike chini ya mapenzi yako, na zawadi uliyokusudia kuwapatia ikawe mbaraka kwako na hatimae wazazi pamoja na Mtto tukutane nao juu mbinguni.

Ya dunia yote yanapita km upepo lkn uzima wa milele utadumu milele zote, ni tumaini letu Bwana cc wanasauti ya injili cku moja tukutane ktk makao uliotuandalia maana ni ahadi yako, andaa mioyo yetu kukutana nawe ujapo mara yapili. Kwan ndivyo tuombavyo kwa jina la Baba Mwana na Roho Mtakatifu, amina.