7-4-2016

KARIBUNI KATIKA IBADA YA ASUBUHI
 Saa 11 (Nyimbo za Injili)
 Saa 12 (Maombi ya Jumla)
 Saa 1 (Injili Ya Leo Asubuhi)

SIFA & SHUKRANI: Mshukuru MUNGU kwa:
 Tabia yake isiyobadilika
 Baraka tele & Uaminifu wake kwetu
 Msamaha wa dhambi zetu
 Nafasi nyingine ya Uhai Leo.

RATIBA YA MAOMBI SIKU HII YA LEO
• Ungamo, Toba, & Msamaha
• Tujiandae pia kiroho kwa ajili ya Ratiba ya Mfungo Jumatano

WAGONJWA WETU
• (Dada Noela) “wagonjwa wetu”
 Babu mwenye Kansa ya Ini huko Kenya
 Babu yake Mr. Wisley kapelekwa Hospitalini
 Zaidi ya Majeruhi 200 (Uturuki, Istanbull Airport)
 Waliopata ajali jana (wachungaji)

CHANGAMOTO ZINGINE
• (Dada Noela) “Nina changamoto ya kuabudu bado”
 Makambi yanayoendea sasa sehemu mbalimbali
 Bajeti ya Biblia, na vipaza Sauti
 Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Iringa.
 Tuwaombee vijana katika karne ya 21

KAMPENI ZA INJILI (USA & Zimbabwe)
• Tuombee pia campeni za kununua Biblia (TGV Bible Project)

USHUHUDA WA LEO.

Watoto wadogo wa Barbra (10 & 8 yrs old) wameacha tabia zao mbaya na wamemwambia Mama yao kua wataanza kuomba na kufunga. Tuzidi kuwaombea.

AHADI YA LEO: (Ufunuo 2:10)

Usiogope mambo yatakayokupata; tazama, huyo Ibilisi atawatupa baadhi yenu gerezani ili mjaribiwe, nanyi mtakuwa na dhiki siku kumi. Uwe mwaminifu hata kufa, nami nitakupa taji ya uzima.
TUNAKARIBISHWA KUFANYA YAFUATAYO:
 Kutoa ushuhuda wa Matendo makuu ya MUNGU
 Kuweka Maombi humu (Sauti/ Maandishi)
 Kutujulisha kama ombi lako limejibiwa
 Kushiriki kipindi kingine cha maombi ya Jioni (Saa 3 Usiku)

KARIBUNI KATIKA CHUMBA CHA MAOMBI ILI TUSHIRIKI IBADA YA MAOMBI YA JUMLA PAMOJA.

July 04, 2016
BWANA AWABARIKI.


 

Advocate Kinja

Tuombe wapendwa
Mungu Baba, muumba wa mbingu na nchi bahari na vyote vilivyomo na chemichemi za maji jina lako takatifu litukuzwe sana. Asante Mungu wetu kwa nafasi nyingine maishani mwetu umetupatia tulisifu jina lako, nasi tunanyenyekea miguuni pako tafadhali tunakuomba uturehemu Mungu wetu.

Tunatambua hakuna lolote jema tulilolitenda macho pako hata tustahili nafasi adhimu, ni Neema yako na Rehema zako tu Mungu wetu, tunakushukuru sana mfalme.

Tazama Mungu wetu cc sote tumekutenda dhambi hivyo tumepungukiwa na utukufu wako, tunakuomba tusamehe dhambi zetu na makosa yetu yote, tutakase kwa damu yako ya thamani uliyomwaga kwa ajili ya ondoleo la dhambi zetu tenda hivyo na kuzidi Mungu wetu. Takasa midomo yetu, nia zetu tufinyange kama mfinyanzi, tuumbie moyo mpya moyo wa nyama ili tuweze kuisikia sauti yako na tufanye matengenezo ya maisha yetu na tukuelekee wewe muumbaji wetu.

Bwana sote ni wagonjwa wa kiroho na na kimwili tunakuomba tupatie Roho Mtakatifu ambae ndie msaidizi wetu ili atutie ktk kweli yote tuyafanye mapenzi yako zaidi sana tukujue wewe Mungu wa kweli na Yesu kristo uliye mtuma. Wagonjwa wa kimwili tunawaleta miguuni pako wewe uliye tabibu mkuu waguse kila anayeumwa ikiwa ni kidonda, malaria, saratani, BP, kisukari TB miguu kuwaka moto mgongo kichwa mafua, wote hawa walioko mahospitalini na majumban wapatie uponyaji wa kweli na jina lako litukuzwe Mungu wa mbinguni.

Tunawaombe wabatizwa wote ktk mkutano wa injili kule bunda, tunakushukuru sana Mungu wetu kwa kutenda mambo makubwa, tunakusihi wote waliojitoa wakabatizwa tunawaweka miguu pako uwafundishe kwa Roho Mtakatifu ili ili waendelee kukua ktk pendo lako, ulinzi imara wa malaika watakatifu ukawazunguke ucku na mchana uwaongoze ktk Changamoto za maisha lkn waandae kwa ajili ya uzima wa milele. Wapo waliobatizwa kwenye mikutano ya makambi hawa nao tunawaleta kwako tukiamini kwako ndipo usalama wa kweli ulipo, wengi wao ni wachanga ktk imani hii lkn kwa uwezo utokao juu utawaongoza na kuwafunsha iwapasayo. Ijapokua shetani atawazongazonga ili awarudishe nyuma lkn tumaini letu ni kwamba mikononi mwako wako salama, washilie hadi ujapo Bwana ili wao pamoja nasi tuliokwisha batizwa tangu zamani tusimame imara tukiitetea kweli ya neno lako na utukute tukiwa tayari kukulaki mawinguni tupae pamoja kwenda mbinguni.

Mungu wetu wa mbinguni, tunaomba utupatie umoja, upendo na mshikamano kati yetu wanasauti ya injili, kadiri tunavyo fikia mwisho wa wakati upendo wa wengi unapoa, ndugu kwa ndugu hawaelewani wanasalitiana hata kuuna tunakuomba Baba, tupatie umoja na Upendo ili tukaumbukize kwa majirani na jamaa zetu, ili wakiiona tofauti wasityone cc bali wewe kupitia kwetu.

Tunaomba kwa ajili ya Changamoto tunazopitia maishani wewe watujua hata mimba hazijatunga ndani ya matumbo ya mama zetu, tunakusihi magumu tunayopitia tupatie ufumbuzi tuimarishe tutie nguvu tusirudi nyumba, daima tusonge mbele kwa imani tukitazamia ushindi maana utatupatia na mlango wa kutokea.

Kila aliyeleta haja yake hapa Bwana wewe uliijua hata kabla hajaandika hivyo mpatie sawasawa na mapenzi yako, ikiwa ni habari ya maombi jibu hitaji lako nasi tuzidi kukutuza Mungu wetu.

Neema yako yatosha Bwana, ikatufunike utufunulie yatupasayo ili tuiishi sheria yako takatifu ya upendo ambayo ndiyo tabia yako halisi. Tunaomba haya tukiamini utatenda sawasawa na neno lako ni katika jina la mwokozi wetu Yesu Kristo aliyo mkombozi wetu amina.