URITHI BORA

URITHI BORA

“Tupate na urithi usioharibika, usio na uchafu, usionyauka, uliotunzwa mbinguni kwa ajili yenu” (1 Petro 1:4).

Maombi yetu kwa Mungu hayapaswi yatoke kwenye mioyo iliyojawa shauku za ubinafsi. Mungu anatusihi tuchague zile karama ambazo zitamletea utukufu. Ni shauku Yake kuwa tuchague hazina ya mbinguni badala ya vitu vya kidunia. Mbele yetu ametuwekea wazi uwezekano na faida za biashara ya kimbingu. Huwa anatutia moyo kwa ajili ya kufikia malengo yetu ya juu kabisa, ambayo ni usalama kwa ajili ya hazina zetu bora zaidi. Pale mali za kidunia zinapofagiliwa mbali, muumini atafurahia hazina zake za kimbingu, utajiri ambao hauwezi kupotea katika maafa yoyote ya kidunia.

Inasikitisha sana pale watu wanapogeukia mbali na urithi usio na mwisho na kuishi kwa namna ya kuridhisha na kutosheleza ufahari wao, kwa ubinafsi na kujionesha, na kwa njia ya kujisalimisha kwa utawala wa Shetani, wanapoteza baraka ambazo wanaweza kuwa nazo kwa ajili ya maisha haya na yale yajayo. Kama ingaliwezekana kwa hawa kuingizwa kwenye ikulu za mbinguni na kuhusishwa katika viwango vya uhuru na usawa pamoja na Kristo na malaika wa mbinguni na pia wana wa Mungu na bado, kitu cha ajabu kama ambavyo kingaliweza kuonekana, wangegeukia mbali na mivuto ya kimbingu.

Shetani anashindana na roho za watu. Hatawaacha wapate taswira ya heshima inayokuja, utukufu wa milele, ambao umeandaliwa kwa ajili ya wale watakaokuwa wakazi wa mbinguni, au kuwa na mwonjo wa uzoefu ambao unakuwa limbuko la furaha ya mbinguni.

Wale wanaomkubali Kristo kama Mwokozi wao, wanakuwa na ahadi ya maisha ya sasa na wa kile kinachokuja. Mwanafunzi wa Kristo aliye chini kabisa anaweza kuwa mkazi wa mbinguni, mrithi wa Mungu kwa ajili ya urithi usioharibika, ambao hauwezi kupotea. Laiti kila mtu angefanya uchaguzi wa karama ya kimbingu, kuwa mrithi wa Mungu kwa ajili ya ule urithi ambao haki yake ni salama dhidi ya mharibu yeyote, dunia isiyo na mwisho! Lo, usiichague dunia!