6-12-2016

Muumbaji mfalme Mungu na Baba yetu wa mbinguni jina lako takatifu litukuzwe sana, asante Baba kwa nafasi nyingine ktk maisha yetu, unaendelea kuudhihirisha ukuu wako kwetu, kwan hakuna lolote jema tulilolitenda likupendezalo machoni pako, lkn bado unatupenda umetupatia nafasi nyingine ya kulisifu na kulitukuza jina lako, na uhimidiwe milele zote.

Baba tunakushujuru sana Mungu wetu kwan wewe ni mwema, Mungu mkuu tunakuja mbele zako miguuni pako kwa jinc tulivyo, sisi ni wadhaifu wanyonge tusio na nguvu wala uwezo, tunakuja kwako wewe mwenye nguvu na uwezo, tupatie nguvu na uwezo. Lkn Baba tusamehe dhambi na makosa yetu tuliyokutenda yakiwa ya wazi ama ya siri, kwa kua wewe unsona hata sirini tafadhali tusaidie kushinda dhambi pekeyetu hatuwezi tujaze kwa Roho Mtakatifu ili atutie ktk kweli yote ili tuyatende mapenzi yako. Tunayo mizigo mizigo mioyo ni mwetu nawe uliahidi kututua mizigo tunakuomba pokea tangu sasa mizigo yetu tuwe huru, lkn huenda ni kwasababu ya chaguzi zetu mbaya tunakuomba tusaidie maana tunalemewa Mungu wetu, wewe ni mwenye uwezo tenda hivyo kwa utukufu wa jina lako.

Baba yetu wa mbinguni, namleta miguuni kwako rafiki yangu Daniel, anadaiwa ada shilingi 372,000/= tu baba wewe wafahamu kwa jinsi gani anavyoumia moyoni mwake maana kesho anafukuzwa chuo km hatolipa, Mungu wetu wewe ni mkuu sana, dhahabu na vyote viijazavyo nchi ni mali yako tenda Bwana kwa utukufu wa jina lako, vile uonavyo ni vyema tenda na jina lako litukuzwe. Itakapopatikana sifa ba shukrani vikurudie wewe Mungu wa mbinguni. Baba si huyo tu pekeake huenda wapo na wengine kati yetu ckatika ada tu, lkn hali za kipato chetu Bwana tubakuomba tubariki ili tuweze kukidhi mahitaji ya familia zetu lkn pia tukutolee zaka na sadaka, tenda hivyo kwa utukufu wa jina lako.

Tunawaombea wagonjwa waliopo majumban na mahospitalini, kwa mkono wako wa uponyaji pita kati yao gusa kila mmoja kwa kadiri ya ugonjwa wake na maumivu yake, ili Bwana wapone na jina lako litukuzwe milele zote.

Yatima wajane wanalia wamekosa wafariji, wamekata tamaa hawana tumaini tena, ucku huu kawapatie faraja na tumaini la kweli uwe mfariji wao wa daima, lkn pia wapatie mahitaji yao ya kila cku kupitia sisi wakuone wewe Mungu wa mbinguni.

Tunaombea kazi ya utume ulimwenguni, popote palipo na mkutano wa injili malaika walinzi waendelee kudhiti majeshi ya ibilidi yasivuruge mpango wwte unaoendelea kwa ajili ya wokovu kwa watu wako, kila ataye sikia sauti yako kupitia wayumishi wako ktk viwanja hivyo wasitoke bure, roho mtakatifu ambae ndie mwenye uwezo wa kuwasaidia kukata shauri akaseme nao kwa pole na siku moja wajiunge na kundi lako kuelekea mbinguni. Lkn pia Baba yeyote atakae ckia sauti na kukiri mwenye ukawazungushie wigo imara ili yule mwovu asiwarudishe nyuma tena bali wasonge mbele ili kuishindania imani waliyopewa watakatifu mara moja tu. Sisi basi Bwana tuliokwisha kuamini tangu zamani tunakuomba tusije tukavutwa na mivuto ya dunia tukakuacha mwokozi wetu, ombi letu Bwana tunahitaji ukae mioyoni mwetu daima utuonze kwa neno lako, maana ndilo ya miguu yetu na mwanga wa njia zetu, kwa maana wewe ndie njia ya kweli na uzima, tukikufuata wewe kamwe hatutatembea gizani, nasi tumekuchagua wewe utuongoze hata zijapo nyakati za taabu Bwana tunajua wewe upo nasi.

Tunayakabidhi maisha yetu kwako maana hutatuacha kamwe, wewe ni mwaminifu sana kwetu. Tunaomba na kushukuru tukiamini kuwa upo nasi kila hatua ktk jina la Yesu aliye Bwana na mwokozi wa maisha yetu amina.