6-11-2016

Mtakatifu Baba na Mungu wetu wa mbinguni jina lako takatifu litukuzwe, asante Mungu wetu kwa nafasi nyingine ktk maisha yetu cku ya leo, umekuwa nasi tangu asbh umetuongoza ktk barabari huku na kule, ujahakikisha tu salama tunasema asante Yesu. Lkn Bwana umeendelea kuwa mbaraka wa pekee ktk maisha yetu, na cku ya leo umeendelea kutukusanya mahali mahali ktk makanisa kukuabudu wewe Mungu wa mbinguni, asante kwa sabato takatifu ambayo hutukumbusha juu ya uumbaji. Tusaidie kuyaishi yote tuliyojifunza na kwa msaada wa Roho Mtakatifu atutie ktk kweli yote ya neno lako na lituongoze ktk kuifikilia toba ya kweli.

Baba ingawa tulkua na sabato yako takatifu lkn hatuna jema tulilolitenda tusamehe dhambi zetu na makosa yetu Mungu wetu, tutakase kwa damu yako ya thamani na utuweke huru mbali na dhambi. Na kwakua ni ahadi yako kuwa tunapojinyenyekeza kwa Imani utasikia maombi yetu, tenda hivyo kwa utukufu wa jina lako tutenge mbali km ilivyo kusini na kaskazin vivyo hivyo tutenge mbali na dhambi na uovu usionekane kwetu milele na milele.

Wakati huu Bwana tunawakumbuka wagonjwa huenda kati yetu ni mgonjwa, lkn wapo wengine kule majumban na mahospitalini, tunawaleta miguuni pako Yesu. Yupo Devotha an a sumbuliwa na kifua tumbo, wapo wanaosumbuliwa na BP, kisukari malaria, typhoid na magonjwa mengine Bwana wewe wayajua, tunaamini wewe ni tabibu mkuu usieshindwa kwa kila ugonjwa kwa kugusa tu wote wanapona tenda hivyo kwa utukufu wa jina lako na wapone. Rafiki yetu Michael ambae nae anamuuguza baba yake tunamleta miguuni pako ganga najeraha yote kwa mkono wako akapone.

Mkutano wa injili kule bunda tunauweka miguuni pako fanikisha kwa mafanikio makubwa, asiwepo wa kusema hakuwahi kuckia ujumbe wako, bali popote sauti yako kupitia watumishi wako ikawe km mwangwi masikioni mwao na Roho Mtakatifu akawasumbue na hatimae wajitoe kwa ubatizo, ikiwa ni mapenzi yako uwaandae kwa ajili ya ckukuu kubwa kule mbinguni. Unapowaandaa hao, nasi pia Bwana tuandae tusaidie kwa Roho Mtakatifu tusalimishe nia zetu kwako, tufinyange km vile mfinyanzi afinyangavyo vyungu ili tufae kwa uzima wa milele, kwa wanasauti ya injili acwepo wa kukosa kuingia ktk ufalme wako.

Bariki familia zetu, bariki uchumi wa wanafamilia tupatie uwezo wa kufikiri na mbinu za kuinua uchumi wa familia zetu, lkn kwa njia ikupendezayo tucje tukakuletea sadaka vilema tucje kupata laana badala ya mibaraka.

Tunaomba kwa ajili ya kazi yako ya injili ulimwenguni bariki ili agizo ulilotuachie litimie na watu wako waokolewe. Tupatie njozi kubwa za kuifanya kazi yako kwa njia mbalimbali ili imfikie kila mtu na jina lako litukuzwe.

Tunawaleta wajane yatima wafungwa, wapo waliokata tamaa, tunakuomba ikiwa ni faraja, tumaini kwa makundi haya tenda kwa uaminifu kwao ili wakutukuze Mungu wa mbinguni, ikiwa ni mahitaji tafadhali wabariki sana na kuzidi na jina lako lizidi kutukuzwa.

Baba, tunaamini wewe ni mwaminifu sana kwetu, tubariki sawasawa na mapenzi yako kwa kadiri uonavyo vyema. Lkn Baba tunakuomba tufundishe vile ipasavyo kuomba maana hatujui kuomba, hata wakati mwingine hatujui tuombayo, lkn wewe ujuae dhamiri za mioyo yetu tenda ilivyo vyema kwa utukufu wa jina lako.

Tunaamini utatenda hivyo kwan tumeomba kwa imani kupitia jina la Yesu mkombozi wetu amina.