Kutulia kabisa katika “kweli yote”

Tangu mwanzo kabisa, watu wa Mungu wamekuwa alama au ishara maalum ya utambulisho wa utii wao kwa Mungu. Wana wa Israeli halisi (ambao sisi pia tu wa kiroho, Wagalatia 3:7, 29), walielekezwa kwa namna ya pekee juu utambulisho huu Amri za Mungu ambazo ziliwatofautisha kabisa na mataifa mengine yote.

Katika utambulisho huu Mungu aliagiza kupitia Musa: “Bali ninyi mlioambatana na Bwana, Mungu wenu, mnaishi kila mmoja wenu, hata leo. Angalieni nimewafundisha amri na hukumu, vile vile kama Bwana, Mungu wangu, alivyoniamuru, ili mzitende katika nchi mwingiayo ili kuimiliki. Zishikeni basi, mkazitende, maana hii ndiyo hekima yenu na akili zenu, machoni pa mataifa watakaozisikia amri hizi zote, nao watasema, Hakika taifa hili kubwa ni watu wenye hekima na akili. Kwa maana liko taifa gani kubwa, lililo na Mungu aliye karibu nao, kama Bwana, Mungu wetu, alivyo, kila tumwitapo? Tena liko taifa gani kubwa, lililo na amri na hukumu zenye haki kama torati hii yote, ninayoiweka mbele yenu leo” (Kumbukumbu 4:4-8, angalia pia Kumbukumbu 5:29).

Na hakuna shaka kuwa Amri ya 4, Amri ya Sabato ya siku ya saba ndiyo ingelikuwa kitambulisho kikuu cha utii huo: “Kwa ajili ya hayo wana wa Israeli wataishika Sabato, kuiangalia sana hiyo Sabato katika vizazi vyao vyote, ni agano la milele. Ni ishara kati ya mimi na wana wa Israeli milele; kwani kwa siku sita Bwana alifanya mbingu na nchi, akastarehe kwa siku ya saba na kupumzika” (Kutoka 31:17, 18, linganisha pia Ezekieli 20:12, 20).

Roho Mtakatifu, ambaye aliahidiwa kwa ajili ya kutufundisha na kututia katika “kweli yote” (Yohana 16:13) hupiga Muhuri Wake (Waefeso 1:13; 4:30) kwa mwumini ambaye ameikubali “kweli yote” kama ilivyofunuliwa katika Maandiko uadhimishaji wa Sabato ya siku ya saba ukiwa ndio alama au “ishara” kuu kwa watu hawa waaminifu “wazitunzao Amri za Mungu na imani ya Yesu.”

Kwa hiyo uhusiano wa Sabato na Roho Mtakatifu ni upi katika suala la kutiwa mhuri? Utunzaji wa Amri zote za Mungu, Sabato ya siku ya saba (Kutoka 20:8-11; Kumbukumbu 5:12-15) ikiwa ni udhihirisho wa pekee wa nje wa uhusiano huu ndio hasa Muhuri wa Mungu.
Kwa ufupi, watu wa Mungu hutiwa Mhuri Wake pale wanapokuwa wametulia kabisa katika “kweli yote” kiasi cha kutoweza kuhamishika.