6-10-2016

Mfalme wetu wa ajabu, Mungu mkuu Mungu muumbaji wa mbingu na nchi, bahari na chemichemi za maji jina lako na litukuzwe sana.

Asante sana Mungu wetu kwa pumzi ya uhai unayotupatia wana na binti zako hadi wakati huu. Umetulinda cku nzima ukatueousha na madhara mbalimbali cku ya leo, hakuna lolote jema tulilolitenda icpokua kwa uwezo wako tu Mungu wetu. Tunakuja kwako jinc tulivyo tu wadhaifu na wadhambi tusamehe sana, tutakase kwa damu yako tuwe safi Bwana.

SAA hii Bwana twaleta mahitaji yetu miguuni pako tunakuomba ckia maombi yetu tukuombayo na ututendee sawasawa na mapenzi yako. Kati yetu wapo wagonjwa wapo mahoslitalini watembelee ukawaguse ucku huu, lkn pengine ni asbh, mchana au jioni nahali fulani maana sauti ya injili tupo duniani kote, kawaguse kwa mkono wako wenye nguvu na wakapone na jina lako litukuzwe sana. Lkn baba, sisi sote tu wagonjwa wa kiroho tunakuomba tibu maradhi yetu ya kiroho, fufua fahamu za kiroho zilizokufa amsha hamu ya kujifunza maneno yako ya uzima, tunakuomba ikiwa tumekufa kabisa kiroho tufufue kutoka kifo hicho, tupatie Roho Mtakatifu atuwezeshe kuyatenda yaliyo mapenzi yako. Tufundishe kuomba na kunyenyejea maana hajui vile itupasavyo kufanya, tunaomba uongozi wa Roho Mtakatifu maishani mwetu Baba.

Tunauleta mkutano wa injili kule bunda ambao cku chache zijazo utaanza kila lulilohitaji la mkutano kalifanikishe kwa utukufu wa jina lako, kila ujumbe utakaockika ktk viwanja vile kila neno likachome moyo wa mtu fulani na kumleta kwa Yesu aliye tumaini letu, na kila mwisho wa juma ikikupendeza na kwa msaada wa Roho Mtakatifu wengi wakakate shauri kwa ajili ya ubatizo. Mchungaji Elly Mshitu anapocmama ukaonekane wewe kupitia kwake, akanene yaliyoyako wala c yanwadamu. Bariki familia yake na jamaa wa nyumban mwake, mibaraka ikaandamane naye na mwisho wa kazi uzima wa milele.

Tunaombea ndoa zote ikiwa ni changa au kongwe tunazileta kwako wewe uliye muasisi wa ndoa hizi zipo Changamoto nyingi waelekeze kujifunza kwako uwapatie muelekeo wala ckutumia akili zao. Wapo vijana wabaotafuta wachumba wapatie wale walio rafiki za Mungu ili ktk familia hizo mpya sauti za furaha zikackike zikikusifu cku zote.

Tunakuomba sana baba bariki mtu mmoja moja ktk group hili, wewe ujuae hata ya siri tupatie mahijati yetu sawasawa na mapenzi yako. Wapo wajane yatima faraja ya kweli na ya pekee ukawapatie maana ni wewe tu, wapo waliokata tamaa tumaini lako lahitajika Yesu.

Tunakuomba kuza imani zetu, ijapokua tupo ndani ya kanisa kwa muda mrefu sana, ljn bado hofu kutokuamini mashaka, tunakuomba tuongezee imani maana pasipo na imani Bwana tutaangamia kwa kutokuamini kwetu.

Baba, dunia inapita na mambo yake, tusaidie sana kufikilia toba ya kweli, tusalimishe nia zetu kwako ili ufanye vile utakavyo, mafanikio yetu yasitutenge na upendo wako, bali kwa msaada wa Roho Mtakatifu tukanyenyekee ukatukweze kwa wakati wako uliokusudia. Lkn zaidi ya hayo Bwana tuandae kwa ajili ya kuurithi uzima wa milele kwenda kukaa nawe milele zote.
Tunaamini unatupenda na utatenda kwa wjngi wa fadhili zako tunaomba kupitia jina la Yesu Kristo aliye mkombozi wetu amina.