Zaburi 144:15

HALI YA FURAHA NYUMBANI HUKUZA AFYA

“Heri watu wenye Bwana kuwa Mungu wao” (Zaburi 144:15).

Nyumba ambapo upendo upo na ambapo huo upendo unaonekana katika mitazamo, katika maneno, katika matendo ni mahali ambapo malaika wanapenda kuishi…

Hebu jua la upendo, uchangamfu na mambo ya furaha yaingie kwenye mioyo yenu wenyewe na hebu mvuto wake mzuri utawale nyumbani… Mazingira ya namna hiyo itakuwa kwa watoto kama hewa na jua vilivyo kwa mimea, ikiendeleza afya na nguvu ya akili na mwili.

Fundisha nafsi yako kuwa na uchangamfu, shukrani na kuonesha shukrani kwa Mungu kwa sababu ya upendo mkuu ambao kwa huo ametupenda… Uchangamfu wa Kikristo ndio uzuri wa utakatifu.

Wakati ambapo huzuni na fadhaa haviwezi kuponya uovu hata wa namna moja, badala yake hivyo vyaweza kuleta madhara makubwa; lakini uchangamfu na tumaini, huku zikiangaza njia ya wengine, “ni uhai kwa wale wazipatao, na afya ya mwili wao wote.”

Yapasa mama ajenge hali ya uchangamfu, ya kuridhika, mwenendo wa furaha. Kila jitihada yenye mwelekeo huu italipwa kwa namna kubwa sana katika hali nzuri ya kimwili na pia hali ya kimaadili ya watoto wake. Roho ya uchangamfu itaendeleza furaha ya familia yake na kwa kiasi kikubwa itaendeleza afya yake mwenyewe.

Afya ya vijana inahitaji mazoezi, uchangamfu na mazingira yanayozungukwa na furaha, yavutiayo, kwa ajili ya maendeleo ya afya ya kimwili na tabia yenye ulinganifu.

Kama watoto wa nuru mpate kuzitangaza fadhili Zake Yeye aliyewaita mtoke gizani mkaingie katika nuru Yake ya ajabu.