6-8-2016

Mtakatifu Baba na Mungu wetu unaeishi mahali palipoinuka sana juu mbinguni, jina lako takatifu litukuzwe sana. Tunayo kila sababu ya kulisifu na kulitukuza jina lako Mungu, kwa jinsi matendo yako yalivyo makuu kwetu, asante kwa ulinzi wako kwetu maana ni neema yako tu ckwa uwezo wetu lihimidiwe jina lako milele zote.

Tunakushukuru sana Mungu wetu maana unatupenda upeo, hata tulipoenda kinyume na mapenzi yako wewe hukutuacha bali ulituzingira mbele na nyuma kuhakikisha tunakua salama asante sana Yesu. Tunajinyenyekeza miguuni pako tunakuomba tusamehe dhambi na makosa yetu, tutakase kwa damu yako ya thamani ambayo ilimwagika kwa ajili ya ondoleo la dhambi.

Wana na binti zako tunayo mizigo mizito mioyoni mwetu hatuwezi kuibeba, tutue mizigo hii Bwana, na kwasababu wewe mwenyewe ulisema tukitwike mizigo na fadhaa zetu, tafadhali tupokee tangu sasa tukutwike mizigo yetu. Tunamuombea rafiki yetu Lulu, anakulilia ucku na mchana sababu ya wadogo zake kwa jinc wanavyomsumbua hawakai nyumban, hata wengine wametoroka nyumban hawajulikani walipo, Yesu wewe unajua yote simama upande wake mpiganie ktk umri mdogo alionao lkn ameachiwa majukumu mazito, mfungulie njia mpatie ujasiri na imani ya kweli aendelee kukutumaini wewe, na cku moja yeye pamoja na wadogo zake wakae pamoja wakutukuze wewe Mungu wa mbinguni.

Mbele yetu kuna mkutano wa injili tukaoanza hivi karibuni kule mjini bunda, tunauweka mikononi mwako, ratibu mipango yote na ikiwa kuna jambo ambalo bado halija kamilika tunakuomba kamilisha mkutano huu ukawe wenye kuzaa matunda makubwa kwa utukufu wa jina lako. Tunamuweka miguuni pako mchungaji Elly Mshitu, ambae ndie atakae simama kwa siku zote za mkutano akitoa maneno ya uzima, tunakuomba sana Yesu mvuvie Roho Mtakatifu ili kila somo ambalo litasikika ktk viwanja vile likawe lenye kuwavuta wengi kwako, mtumie km chombo cha kufikisha ujumbe wako kwa watu wako na kila mwisho wa juma anapotoa wito wengi wakajitoe kwa ajili ya kukuri kuwa Bwana na mwokozi wa maisha yao. Tunakuomba hata ktk vipindi vingine amvavyo vitaendeshwa pale vikawe na mguso wa pekee kwa watu wako.
Bariki mkutano wa mini extravaganza huko kilosa morogoro, mkutano huu ukawe na manufaa makubwa kwa kila ataeckia sauti yako kupitia watumishi wako.

Bariki watumishi wako popote ulimwenguni tupatie umoja na mshikamano ktk nyakati hizi za mwisho, kwa maana ulituombea tuwe na umoja ili kazi yako isonge mbele. Bariki familia zetu, vijana walio na wachumba, wanaotafuta hata ukatipatie wenzi wenye hofu ya Mungu na jina lako litukuzwe.

Bariki biashara, kazi zetu kule maofisini na mipango yetu inapofanikiwa tukutukuze wewe Mungu wa mbinguni. Wapo wanafunzi wapo kwenye mitihani tunawaombea mitihani mwema wafaulu na jina lako litukuzwe sana.

Baba tupatie njozi kubwa na maoni kwa ajili ya kazi yako, maana ulisema sharti injili ihubiriwe kwa kila kiumbe kuwa ushuhuda ili ktk hukumu acwepo wa kusema hakuwahi kusikia habari za wokovu. Tunaposalimisha nia zetu kwako, tuandae kukutana nawe Mungu wetu na tuwe tayari kukulaki mawinguni ujapo mara ya pili, ili cc pamoja na hao watakaookolewa kwa kusikia ujumbe uliotipatie sote kwa pamoja na malaika zako tukafurahi nawe milele huko juu mbinguni.

Ni imani yetu unatupenda na utatenda hivyo kwa utukufu wa jina lako kwani tumeomba kwa imani kupitia jina la mwanao mpendwa Yesu Kristo ambae ndiye Bwana na mwokozi wetu na kila mmoja aseme amina.