KUJA KWA YESU MARA YA PILI:

Jibu la Yesu katika Mathayo 24 lilihusu“dalili ya kuja kwako” (aya ya 3),ya kuja kutawala.

Maonyo gani mengine Kristo anatoa katika muktadha wa matukio ya kurudi kwake, na ni jinsi gani hili linaonekana katika kipindi chote cha historia?

Hapa kuna Yesu, kutokana na mtazamo wa kiulimwengu si chochote zaidi ya mhubiri Mgalilaya anayezungukazunguka akiwa na wafuasi wachache, huku akitabiri kuwa watu wengi watakuja kwa sababu ya jina lake, wakidai kuwa ni yeye? Kwa kweli,hiki hasa ndicho kilichotendeka ndani ya karne nyingi na hata katika siku zetu, ukweli ambao unatupatia ushahidi wenye nguvu zaidi juu ya Neno la Mungu.
Soma Mathayo 24:27-31. Kuja kwa Yesu mara ya pili kunauelezeaje? Kitu gani kinatokea pale anapokuja?
Baada ya kuonya kwamba wengi watakuja wakijiita wao ni Kristo,Yesu ndipo anataeleza jinsi kuja kwake kunavyofanana hasa.

Kwanza, kuja kwa Yesu mara ya pili itakuwa katika nafsi yake, na halisi

Ni Yesu mwenyewe ambaye anarudi duniani. “Bwana mwenyewe atashuka kutoka Mbinguni (1Wathesalonike 4:16), ni ukanushaji dhahiri wa wale wanaodai kwamba kurudi kwa Yesu ni wazo la enzi bora au kirahisi enzi mpya katika historia ya mwanadamu.

Kurudi kwake kutaonekana,kama umeme katika anga “Kila jicho litamwona”(Ufun 1:7).

Sitiari ya baragumu inadhihirisha kwamba kutakuwa kwa sauti kubwa, kubwa kiasi cha kuwaamusha wafu! Na muhimu zaidi, iwapo kuja mara ya kwanza kulikuwa na unyenyekevu, kule kwa mara ya pili, Yesu atakuja kama Mfalme mshindi (Ufun 19:16) akiwa ameshinda juu ya maadui zake(na zetu) wote(1Korint 15:25).

Katika wakati wa msukosuko na mashaka katika dunia yetu kuhusu mambo ya baadaye, tunawezaje kupata nguvu binafsi na Tumaini kutoka katika ahadi ya kuja mara ya Pili?

KILA JICHO LITAMWONA

Somo letu la leo linasema kuja kwa Yesu Mara ya pili.

Pamoja na kwamba Biblia imefundisha kuwa kila jicho litamuona lakini wako manabii wa uongo wanawadanganya watu na kuwaambia Yesu atawachukua watakatifu kwa siri, Manabii hawa waodanganya hata Tanzania wako wengi sana.

Uzuri ni kwamba Yesu alishaona ilo “Tazama, nimekwisha kuwaonya mbele.
Basi wakiwaambia, Yuko jangwani, msitoke; yumo nyumbani, msisadiki.”(Mathayo 24:25,26).

Mfano wa wafuasi wa Braham wanaamini Yesu aishakuja mara ya pili kupitia mwili wa nabii Braham.

Mimi na wewe ni mashahidi, wako wanaojiita Yesu, huko na huko, na Kuna Mwingine anajiita Yesu katokea huko Brazil.
Biblia Inasema “Tazama, yuaja na mawingu; na kila jicho litamwona, na hao waliomchoma; na kabila zote za dunia wataomboleza kwa ajili yake. Naam. Amina.”(Ufunuo 1:7).

Makabira yote yatamuona, Biblia inasema kila jicho litamuona si watakatifu tu bali hata waliochoma. “Kwa maana kama vile umeme utokavyo mashariki ukaonekana hata magharibi, hivyo ndivyo kutakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Adamu.”(Mathayo 24:27). Ni dhahiri ya kwamba watu wote watamuona Yesu anapokuja mara ya pili. “ndipo itakapoonekana ishara yake Mwana wa Adamu mbinguni; ndipo mataifa yote ya ulimwengu watakapoomboleza, nao watamwona Mwana wa Adamu akija juu ya mawingu ya mbinguni pamoja na nguvu na utukufu mwingi.”(Mathayo 24:30).
Biblia inasema kila jicho litamuona, lakini manabii wa uongo wanasema atakuja kwa siri huu ni udanganyifu wa Shetani anatumia leo hii tufunguke macho na kuutataa uongo huu.

Katika Ufunuo 6:15-16 Biblia Inasema “Na wafalme wa dunia, na wakuu, na majemadari, na matajiri, na wenye nguvu, na kila mtumwa, na mwungwana, wakajificha katika pango na chini ya miamba ya milima,
wakiiambia milima na miamba, Tuangukieni, tusitirini, mbele za uso wake yeye aketiye juu ya kiti cha enzi, na hasira ya Mwana-Kondoo.”(Ufunuo 6:15,16).

Waovu wataiambia Milima uwaangukie lakini hawatafanikiwa Maana kila jicho lazima limuone.
Tunaweza kuukataa uongo huu leo ili tuwe miongoni mwa watakaomlaki Yesu ajapo mara ya pili.(Isaya 25:9).