Sons and Daughters of God, uk. 182.4

“Endapo wale wanaokusudia kuwa na ndoa hawatakuja kupata taabu na matokeo yasiyokuwa na furaha baada ya ndoa yao, lazima walifanye kuwa suala la tafakari makini na la dhati hivi sasa. Hatua hii inapochukuliwa bila busara ni moja miongoni mwa njia zinazofanikiwa kabisa kuharibu kufaa kwa vijana wa kiume na wa kike. Maisha huwa mzigo, laana. Hakuna mtu mwingine anayeweza kuharibu kabisa furaha na kufaa kwa mwanamke, na kuyafanya maisha kuwa mzigo uumizao moyo, kama anavyoweza kufanya mume wake mwenyewe; na hakuna mtu mwingine anayeweza kufanya kiasi cha sehemu moja kati ya mia ili kuzimisha matumaini na malengo ya mwanamume, kuhafifisha uwezo wake na kuharibu mvuto na matarijio yake, kama anavyoweza kufanya mke wake mwenyewe. Ni katika saa ile ya ndoa ndipo wanaume na wanawake huchumbia mafanikio au kushindwa kwao katika maisha haya, na matumaini ya maisha yao yajayo.”—Ellen G. White: Sons and Daughters of God, uk. 182.4