MAJARIBU PART 2.

  • a25

Kipindi; kaya na familia

β€πŸŒΉπŸ’πŸ’žπŸ‘­πŸ‘¨β€πŸ‘©β€πŸ‘§β€πŸŒΉ
Somo: MAJARIBU PART 2.
Kila mwanadamu kuna wakati hupitia katika majaribu ya aina mbalimbali katika maisha yake. Kuna majaribu ambayo huja kwa sababu ya kupungua kwa maombi, kuna majaribu yanayotokana na hila za watu, kuna majaribu yanayotokana tamaa ya mtu mwenyewe na pia kuna majaribu kama kipimo cha MUNGU kwa mtu wake ampendae.
*Swali ni kwanini tunashindwa katika majaribu?
zifuatazo ni sababu 5 za mtu kushindwa katika majaribu na hapa tunajifunza kwa kupitia mtumishi wa MUNGU Ayubu.

SABABU 5 ZA MTU KUSHINDWA KATIKA JARIBU.

πŸ™πŸΌ1:Wahudumu wetu katika majaribu.
Ayubu 2:9.”Ndipo mkewe akamwambia, Je! Wewe hata sasa washikamana na utimilifu wako? Umkufuru Mungu, ukafe”
Hapa mke wa Ayubu ambaye alitakiwa awe ndiye anayemtia moyo mmewe yeye ndio kwanza alimwambia amkufuru MUNGU ili afe. Na hata leo wapo watu wengi sana ambao yawezekana uko kwenye jaribu fulani mfano ugonjwa lakini wao ndio kwanza ushauri wao kwako ni kwamba uende kwa mganga wa kienyeji ukawekewe jini ili upate nafuu kumbe ndio kabisa wanakupoteza. Hivyo wahudumu kwenye jaribu wanaweza kabisa wakasababisha ushindwe katika jaribu fulani hata kama ni dogo.

πŸ‘«2:Marafiki tunaoshilikiana nao au wanaotutembelea wakati wa tatizo.
Ayubu 2:12-13”
Basi walipovua macho yao, nao wakali mbali, wasimtambue, wakainua sauti zao na kulia; kila mmoja akararua joho yake, wakarusha mavumbi juu ya vichwa vyao kuelekea mbinguni. Kisha wakaketi nchi pamoja naye muda wa siku saba, mchana na usiku, wala hapana mmoja aliyenena naye neno lo lote; kwa maana waliona ya kuwa mashaka yake aliyo nayo ni makuu mno.”
Marafiki wakati mwingine wanaweza kuwa kikwazo cha mtu kushinda jaribu alilonalo na hapa tunajifunza kuhusu marafiki watatu wa ayubu ambao walikuja kumtembelea na badala ya wao kuwa faraja ndio kwanza walianza kumshutumu Ayubu kwamba haiwezekani awe hivyo lazima tu kuna dhambi amefanya na wanamwambia awaambie dhambi aliyofanya ili wamwombee kwa MUNGU na jaribu lake liishe kumbe wao ndio wakosaji na sio Ayubu.ndugu ni mara ngapi umepatwa na magumu na marafiki zako kuanza kukushutumu kwamba haiwezekani MUNGU ayaruhusu hayo kwako ni lazima tu umetenda dhambi kumbe hata dhambi hukutenda ila ni jaribu tu la kupima imani yako na baada ya kushinda jaribu hili unapandishwa kutoka utukufu hadi utukufu. Hivyo marafiki au watu wanaokutembelea wakati wa jaribu wanaweza kuwa sababu yako ya kushindwa kama ukiamua kuwasikiliza wakuambiacho. Hapa ayubu hakuwapa nafasi ndio maana alishinda majaribu hayo.
Unaweza ukajiuliza kati ya Ayubu na wale rafiki zake ni nani alikua na mashaka? Marafiki zake walikua na mashaka kuliko hata mgonjwa mwenyewe na kama uko kwenye hali mbaya harafu wazima waliokuzunguka wao ndio wanalia hata wanashindwa kula hakika watazidisha ugonjwa kwako muhusika kamili.

πŸ’₯3:Kujihesabia haki wakati wa majaribu.
Ayubu 9:2”Kweli najua kuwa ndivyo hivyo; Lakini mtu huwaje mwenye haki mbele za Mungu?”
usijihesabie haki wakati wa jaribu na pia ndugu waliochini kiroho usiwasikilize sana wakati wa jaribu maana imani zao ni ndogo hivyo ni rahisi sana kukukatisha tamaa na kukupelekea uchukue maamuzi mabaya tena ukiwa karibu kabisa na ushindi wako.

πŸ™…πŸΌ4:Tusijilinganishe sana na wale ambao hawajaribiwi wakati huo. Ayubu 12:4”Mimi ni mtu wa kuchekwa na jirani yake, Ni mtu niliyemwita Mungu, naye akanijibu; Huyo mwenye haki, aliye mtimilifu, amekuwa ni kicheko”
Ndugu usikubali kujiringanishi na watu ambao hawajaribiwi wakati huo maana unaweza ukaanza kulalamika na kupelelea kukufuru kwa MUNGU na kuona kama unaonewa wewe tu huku wengine wakiishi kwa amani na furaha isipokua wewe tu.

πŸ™Š5:Tusiwahusudu wasioamini.
ukiwahusudu wasioamini utakuwa unajipoteza wewe mwenyewe pia ukiwahusudu wasioamni utakua unaanza kuikataa mbingu.

HAYA YOTE HUPUNGUZA UWEZEKANO WA KUSHINDA MAJARIBU.
MUNGU awabariki sana .

🌹Hebu tuangalie mfano; kuna wakati Yesu Kristo alizuiliwa na Wasamaria kuingia katika kijiji chao, Yakobo na Yohana walichukizwa na jambo hilo na wakataka kuagiza moto kutoka mbinguni ili kuwaangamiza Wasamaria wale lakini Yesu Kristo aliwazuia (Luka Mtakatifu 9:51-56)

Ilipofika wakati Yesu Kristo anakikabiri kikombe cha mateso, baada ya kuila pasaka aliwachukua wanafunzi wake hadi bustani ya Gethsemane na akawachukua Petro, Yakobo na Yohana kwa ukaribu zaidi. Akawaambia Roho yangu ina huzuni kiasi cha kufa, kaeni hapa mkeshe pamoja nami (muombe pamoja nami), lakini wanafunzi hawa walipofika sehemu hii walilala wakamuacha Yesu Kristo apambane mwenyewe. Kwa sababu hawakua na sehemu ya kukinywea kikombe cha mateso cha Yesu Kristo (Mathayo Mtakatifu 26:36-40)

Kwa hiyo ninataka utambue kuwa uwapo katika jaribu hupaswi kutumia akili, ufahamu, elimu na nguvu zako kujinasua kutoka katika jaribu. Mruhusu Mungu akuvushe mwenyewe kwa utukufu wake kwa jina la Yesu Kristo. Pia ni lazima wapendwa au wakristo wenzako wakuache ili uvuke wewe mwenyewe kwa sababu unayejaribiwa ni wewe na siyo wao.

Namna ya kupita katika jaribu ili upate ushindi wa heshima
Hapa ndipo penye kiini cha somo hili, namna unavyopita katika jaribu ndivyo kunaamua namna na aina ya ushindi utakao upata. Ukipita kwa akili zako utapata matokeo yanayolingana na akili yako, na hata ukishinda hutapata ushindi wa heshima wenye utukufu wa Mungu. Kwa mfano wapo mabinti wawili wanatafuta kazi, mmoja akatumia mwili wake (rushwa ya ngono) na mwingine akamtumaini na kumtegemea Mungu, wote wanaweza kupata kazi, lakini furaha ya kupata kazi na utukufu wa kazi utatofautiana na hata muda wa kudumu katika kazi utatofautiana pia.

Unapopita katika jaribu, ni lazima uzingatie mambo yafuatayo ili Mungu akupiganie na upate ushindi wenye sifa na utukufu kwa Mungu, ushindi wenye taji safi kwa imani na ushuhuda wako.

Utii kwa sauti ya Mungu
Unapokuwa na jaribu shetani huongea mara nyingi kwa sauti nyingi, lakini Mungu huongea mara chache sana kwa sauti moja tu. Ni lazima ukubali kuisikiliza, kuitambua na kuitii sauti ya Mungu, huo ndio ushindi wako.

Yoshua 6:3-4. β€œNanyi mtauzunguka mji huu, watu wote wa vita, mkiuzunguka mji mara moja. Fanya hivi siku sita. Na makuhani saba watachukua tarumbeta saba za pembe za kondoo waume, mbele ya hilo sanduku; na siku ya saba mtauzunguka mji mara saba, nao makuhani watapiga tarumbeta zao.”

Kabla ya kufika katika mji wa Yeriko, Israeli walipigana vita vingi na kama ni ujuzi wa vita basi walikuwa nao. Wangeweza kuingia Yeriko pasipo kumshirikisha Mungu kwa sababu vita nyingi walizopigana walishinda, walikuwa na kila sababu ya kujiamini. Lakini waliamua kumshirikisha Mungu, na Mungu aliposema nao walimsikiliza na kutii sauti yake.

Watu wengi tunachokosea ni kwamba tunaomba msaada wa Mungu na wakati tunasikiliza sauti nyingine tofauti na sauti ya Mungu. Mungu anapotupa majibu, tunafuata na kutii sauti nyingine na siyo sauti ya Mungu, na hapa ndipo tunajipata tumeangamizwa.

Kwa kutii maelekezo ya Mungu, Israeli walipata ushindi wa kuuingia mji wa Yeriko kwani Mungu alifanya vita kwa ajili yao (Yoshua 6:15-16, 20).

Na wewe ukiamua kuisikiliza sauti ya Mungu na kutii kufuata maelekezo yake, hakika ushindi utakuwa upande wako kwani Mungu mwenyewe atapigana na adui zako kwa ajili yako.

Uwe na imani, Mungu atatenda
Mungu ni Mungu wa ahadi, anatenda jambo kulingana na ahadi iliyopo ndani ya neno lake. Pale tunapoona hakuna njia, kiza kinene mbele, hatuna msaada ndipo Mungu hufanya njia hapo (Isaya 43:16).

Unapokuwa katika jaribu, kadri siku zinavyoongezeka ndivyo unapaswa kuzidisha imani yako kwa Mungu. Na kama ulikuwa ukimuomba Mungu mara moja kwa siku, ongeza maombi zaidi ikiwezekana hata mara tano kwa siku. Ipo siri katika kufanya hivi, kwanza unamfanya Mungu aoneimani yako kwake inakuwa na nia yako thabiti ya kuhitaji msaada wake. Pili, ni njia ya kumdhohofisha shetani na kumfanya ashindwe vita na kukuachilia mara moja.

Ninakuhakikishia, kwa kufanya hivi ni lazima Mungu atakuokoa katika jaribu lako kwa ushindi mkubwa na haraka iwezekanavyo.