6-7-2016

Halleluja Baba na Mungu wetu wa mbinguni jina lako takatifu litukuzwe sana. Baba tunasema asante kwa ulinzi wako wa kutwa nzima ya leo, unaendelea kuupigania uhai wetu, pale mwovu anapotaka kutuangamiza, lkn wewe umesimama upande wetu.

Tunakushukuru sana kwasababu ni neena yako tu ndio maana bado tunaishi. Baba tabia yako ya upendo kwetu ndio ilikufanya ukakubali kuiacha enzi ili kuja kutuokoa cc tusiostahili, ukakubali kudhihakiwa tena ukafa kifo cha aibu pale msalabani kwa ajili ya dhambi zetu. Baba pamoja na kutuokoa kutoka dhambini lkn bado tumeendelea kucheza na dhambi cku hadi cku, tunakuomba Mungu wetu tusamehe cc tusiostahili, tuvute kwa kamba za pendo lako ili turejee kwako Mungu wetu.

Jioni na ucku huu tunakuja miguu pako tu wanyonge na wadhaifu mno, tunalemewa na miziko mizito fadhaa za maisha na masumbuko tunakuomba uwe radhi utege ckio uckie shida zetu tunapokulilia Mungu wetu. Kati wapo wagonjwa wamelazwa mahospitalini lkn wengine wapo majumbani, huenda daktari amewaruhusu kwasababu ameona c wakupone tena, lkn Yesu kwa neno lako na kwa mamlaka yako unaouwezo wa kurejesha afya kwa waliowagonjwa na wadhaifu, tunakuomba wagonjwa wote ambao taarifa zao zimeletwa humu tuwaombee na hata wale ambao hatuna taarifa zao, lkn Bwana ni wagonjwa kawaguse kwa mguso wa imani nao wakapone maana wewe ni tabibu mkuu usiye shindwa, usiyetumia dawa bali kwa neno moja tu au kwa kugusa tu wanapona, tenda hivyo kwa utukufu wa jina lako.

Watu wako baba wengi wametaka tamaa sababu ya maisha magumu wengine wajane wengine yatima wanahitaji faraja yako na tumaini lako tafadhali watembelee ucku huu ukawa patie kila lililohitaji lao wakutukuze wewe Mungu wa mbinguni.

Tunaombea amani kwa watumishi wako, wakati fulani amani imetoweka kuanzia ktk familia zao leta amani kati yao, furaha upendo ukawale na ibada ya kukutukuza wewe ikaonekane ba jina lako litukuzwe. Tunakulilua sana Bwana tunaomba tupatie roho mtakatifu ili awe mwalimu wetu daima ili aendelee kusema nasi kwa saiti ya upole mioyoni mwetu na kutufunulia yaliyo mapenzi yako kwetu nasi tuishi sawasawa na neno lako takatifu.

Baba yetu mpendwa tunaombea lile kundi la rafiki yetu Job, endelea endelea kuliimarisha ijapokua kuna Changamoto zinajitokeza kati yao, tafadhali Yesu ingilia kati kwakua wapo kwa kusudi la kukuinua wewe waimarishe walitukuze jina lako Mungu wetu.

Tunaombea umoja kwa wanasauti ya injili upendo na uimarike tukuze kiroho tuwezeshe kusalimishi nia zetu kwako ili tukukuze wewe Mungu wa mbinguni. Kila Jumatano ya wiki ni cku tuliyoitenga kwa ajili ya kufunga na kuomba tunakuomba kwa kadiri tunavyojinyima tukileta shida zetu ckia na utujibu kila mmoja kwa hitaji lake na jina lako litukuzwe milele zote.

Baba, tunaamini wewe ni mwaminifu wa kweli, hivyo utajibu haja zetu sawasawa na mapenzi yako, ndilo ombi lwtu kupitia jina la Yesu kristo Bwana wetu amina.