05/06/2016

KESHA LA ASUBUHI

J’pili- 05/06/2016

Tuchague Washirika Wetu kwa Uangalifu

Ndivyo watakavyoweka jina langu juu ya wana wa Israeli; nami nitawabarikia. (Hesabu 6:27.)

Neno la Mungu linasisitiza sana juu ya mvuto unaotokana na mahusiano, hasa kati ya wanaume na wanawake. Nguvu yake ni kubwa zaidi katika kukuza akili na tabia kwa watoto na vijana.

Marafiki wanaoshikamana nao, kanuni wanazozikubali, mazoea wanayojenga, vyote hivi vitatoa jibu la swali kuhusu kufaa kwao hapa, na mustakabali wao katika siku za usoni, manufaa ya milele.

Kupitia katika uhusiano na wasio na dini, wapenda anasa na waliopotoka, vijana wengi sana wanapoteza usahili na usafi, imani katika Mungu na roho ya kujikana nafsi ambayo Baba na mama zetu wa Kikristo walizidumisha na kuzilinda kwa maelekezo mazuri na maombi ya dhati…

Kama ilivyo kanuni, wanaume na wanawake ambao wana mawazo mapana, makusudi yasiyo na ubinafsi, makusudio ya kiungwana, ni wale ambao tabia zao zilikuzwa kutokana na mahusiano yao katika miaka ya awali maishani. Nyakati zote aliposhughulika na Israeli, Mungu aliwasisitizia umuhimu wa kuchunga mahusiano ya watoto wao. Mipango yote ya maisha ya kiraia, kidini na kijamii ilifanywa katika mtazamo wa kulinda watoto dhidi ya mahusiano yanayoharibu hivyo kuwafanya tokea miaka ya awali, wawe wajuzi wa maagizo na kanuni za sheria ya Mungu.

Kielezo kilichotolewa wakati wa kuzaliwa kwa taifa kilikusudiwa kugusa mioyo yote. Kabla ya ile hukumu mbaya sana na ya mwisho haijawafikia Wamisri ya kuuawa kwa wazaliwa wa kwanza, Mungu aliwaamuru watu wake kukusanya watoto wao na kuwaweka ndani ya nyumba zao. Miimo ya kila nyumba ilikuwa imepakwa damu na wote walikuwa wasalie ndani ya ulinzi uliooneshwa kupitia katika kielelezo hiki. Kwa hiyo leo, wazazi wanaompenda na kumcha Mungu sharti wawatunze watoto wao chini ya “mafungo ya agano,” – ndani ya ulinzi wa ile mivuto mitakatifu inayowezekana kupitia kwa damu ya Kristo inayokomboa;