Kutoka 31:12-18

KWANINI SABATO? (part 3)
- June 24, 2016
- Majukwaa Ya Sauti Ya Injili.
- Fungu Kuu: Kutoka 31:12-18
MUHTASARI WA INJILI YA LEO:
- Amri: Hakika mtazishika Sabato zangu,
- Sababu: Ni ishara kati ya Mimi (Yahweh) na ninyi
- Muda: “katika vizazi vyenu vyote”
- Ujuzi: ili mpate kujua ya kuwa (19:5)
- Utambuzi: Mimi Ndimi Bwana (our identity)
- Utakaso: niwatakasaye ninyi.
- Adhabu ya kuinajisi Sabato
- Siku Sita za Kazi & Sabato
- Pumziko la Sabato
- Utakatifu wa Sabato
- Sabato & Agano la milele
- Sabato & Ishara ya milele
Kutoka 31:12-18
- 12 Bwana akasema na Musa, na kumwambia,
- 13 Kisha, nena wewe na wana wa Israeli, na kuwaambia, Hakika mtazishika Sabato zangu, kwa kuwa ni ishara kati ya mimi na ninyi katika vizazi vyenu vyote; ili mpate kujua ya kuwa mimi ndimi Bwana niwatakasaye ninyi.
- 14 Basi mtaishika hiyo Sabato; kwa kuwa ni takatifu kwenu; kila mtu atakayeitia unajisi hakika yake atauawa; kwa kuwa kila mtu afanyaye kazi katika siku hiyo, nafsi hiyo itakatiliwa mbali na watu wake.
- 15 Kazi itafanywa siku sita; lakini siku ya saba ni Sabato ya kustarehe kabisa, takatifu kwa Bwana; kila mtu atakayefanya kazi yo yote katika siku ya Sabato, hakika yake atauawa.
- 16 Kwa ajili ya hayo wana wa Israeli wataishika Sabato, kuiangalia sana hiyo Sabato katika vizazi vyao vyote, ni agano la milele.
- 17 Ni ishara kati ya mimi na wana wa Israeli milele; kwani kwa siku sita Bwana alifanya mbingu na nchi, akastarehe kwa siku ya saba na kupumzika.
- 18 Hapo Bwana alipokuwa amekwisha zungumza na Musa katika mlima wa Sinai, akampa hizo mbao mbili za ushuhuda, mbao mbili za mawe, zilizoandikwa kwa chanda cha Mungu.