NK # 1-122

(NK # 1) MTAKATIFU, MTAKATIFU, MTAKATIFU
(HOLY, HOLY, HOLY)

1. U Mtakatifu! Mungu Mwenyezi!
Alfajiri Sifa Zako Tutaimba;
U Mtakatifu, Bwana Wa Huruma.
Mungu Wavyote Hata Milele.

2. Umtakatifu! Na Malaika
Wengi Sana Wana Kuabudu Wote;
Elfu Na Maelfu Wana Kusujudu
Wazamani Na Hata Milele.

3. U Mtakatifu! Ingawa Giza
Lakuficha Fahari Tusiioone,
U Mtakatifu! Wewe Peke Yako,
Kamili Kwa Uwezo Na Pendo.
(NK # 2) TWAMSIFU MUNGU
(WE PRAISE THEE, O GOD)

1. Twamsifu Mungu, Mwana Wa Upendo,
Aliye Tufia Na Kupaa Juu.

Aleuluya! Usifiwe, Aleluya Amin;
Aleuluya! Usifiwe, Utubariki.

2. Twamsifu Mungu, Roho Mtukufu,
Akatufunulia Mwokozi Wetu.

3. Twamsifu Mwana, Aliye Tufia,
Ametukomboa Na Kutuongoza.

4. Twamsifu Mungu Wa Neema Yote ,
Aliyetwaa Dhambi, Akazifuta.

5. Tuamshe Tena, Tujaze Na Pendo.
Moyono Uwashe Moto Wa Roho.

(NK # 3) MUNGU ATUKUZWE
(TO GOD BE THE GLORY)

1. Mungu Atukuzwe Kwa Mambo Makuu,
Upendo Wake Alitupa Yesu,
Aliyejitoa Maisha Yake,
Tuwe Nao Uzima Wa Milele.
Msifu, Msifu, Dunia Sikia;
Msifu, Msifu Watu Wafurahi;
Na Uje Kwa Baba, Kwa Yesu Mwana,
Ukamtukuze Kwa Mambo Yote.

2. Wokovu Kamili, Zawadi Kwetu,
Ahadi Ya Mungu Kwa Ulimwengu;
Wanaomwamini Na Kuungama,
Mara Moja Wale Husamehewa.

3. Alitufundisha Mambo Makuu,
Alihakikisha Wokovu Wetu;
Lakini Zaidi. Ajabu Kubwa,
Yesu Atarudi Na Tutamwona.
(NK # 4) Jina La Yesu, Salamu (All Hail The Power)

1. Jina La Yesu, Salamu! Lisujudieni,
Ninyi Mbinguni, Hukumu, Na Enzi Mpeni.
Ninyi Mbinguni, Hukumu, Na Enzi Mpeni.

2. Enzi Na Apewe Kwenu, Watetea Dini;
Mtukuzeni Bwana Wenu, Na Enzi Mpeni.
Mtukuzeni Bwana Wenu, Na Enzi Mpeni.

3. Enyi Mbegu Za Rehema Nanyi Msifuni;
Mmeponywa Kwa Neema, Na Enzi Mpeni.
Mmeponywa Kwa Neema, Na Enzi Mpeni.

4. Wenye Dhambi Kumbukeni Ya Msalabani.
Kwa Furaha Msifuni, Na Enzi Mpeni.
Kwa Furaha Msifuni, Na Enzi Mpeni.

5. Kila Mtu Duniani Msujudieni,
Kote-Kote Msifuni, Na Enzi Mpeni.
Kote-Kote Msifuni, Na Enzi Mpeni.

6. Sisi Na Wao Pamoja Tu Mumo Sifani.
Milele Sifa Ni Moja, Ni “Enzi Mpeni”.
Milele Sifa Ni Moja, Ni “Enzi Mpeni”.
(NK # 5) NA TUMWABUDU MFALME MTUKUFU
(O Worship The King)
1. Na Tuumwabudu Huyo Mfalme,
Sifa Za Nguvu Zake Ziimbe;
Ni Ngao, Ni Ngome, Yeye Milele,
Ndizo Sifa Zake Kale Na Kale.

2. Tazameni Ulimwengu Huu,
Ulivyoumbwa, Ajabu Kuu;
Sasa Umewekwa Pahali Pake,
Hata Utimize Majira Yake.

3. Kwa Ulinzi Wako,Kwetu Bwana,
Twakushukuru, U Mwema Sana;
Hupewa Chakula Kila Kiumbe,
Kila Kitu Kina Mahali Pake.

4. Wanadamu Tu Wanyonge Sana,
Twakutumaini Wewe, Bwana;
Kwamwe Haupungui Wako Wema,
Mkombozi Wetu, Rafiki Mwema.
(NK # 6) KUMEKUCHA KWA UZURI
(The Morning Bright With Rosy Light)

1. Kumekucha Kwa Uzuri, Nafumbua Macho;
Baba Amenihifadhi, Ni Wake Mtoto.

2. Bwana Niwe Leo Kutwa, Ulinzi Ni Mwako;
Nisamehe Dhambi, Niwe Mikononi Mwako.

3. Roho Wako Anikae, Moyoni Daima;
Anitakase, Nione Uso Wako Mwema.
(NK # 7) MUNGU MSAADA WETU
(O God Our Helper In Ages Past)

1.Mungu Msaada Wetu Tangu Miaka Yote
Ndiwe Tumaini Letu La Zamani Zote.

2.Kivuli Cha Kiti Chako Ndio Ngome Yetu,
Watosha Mkono Wako Ni Ulinzi Wetu.

3.Kwanza Havija Kuwepo Nchi Na Milima,
Ndiwe Mungu; Chini Wako Twakaa Salama.

4.Na Miaka Elfu Ni Kama Siku Moja Kwako;
Utatulinda Daima , Tu Wenyeji Wako.

5.Bwana Msaada Wetu Tangu Miaka Yote,
Mlinzi Wetu Wa Ngome, Daima,Milele.
(NK # 8) UJE MKOMBOZI
(O Hear My Cry)

1.Unisikie Ninapolia,Uje, M-Kombozi;
Moyo Wangu Huku Tazamia, Uje, M-Kombozi;

Nimepotea Mbali Na Kwangu, Nimetanga Peke Yangu;
Unichukulie Sasa Kwako: Uje, M-Kombozi;

2.Sina Mahali Pa Kupumuzika, Uje, M-Kombozi;
Unipe Raha, Nuru, Uzima, Uje, M-Kombozi;

3.Nimechoka, Njia Ni Ndefu Uje, M-Kombozi;
Macho Yako Kuona Nataka, Uje, M-Kombozi;

4.Bwana, Daima Hutanidharau, Uje, M-Kombozi;
Kilio Changu Utanijibu, Uje, M-Kombozi;
(NK # 9) MWUMBAJI, MFALME
(My Make And My King)

1. Mwumbaji, Mfalme Vitu Vyote Vyako;
Nikwaukarimu Wako, Ninabarikiwa,
Nikwaukarimu Wako, Ninabarikiwa.

2.Uliyeniumba, Nakutegemea;
Sina Budi Kuzisifu, Hisani Zako Kuu,
Sina Budi Kuzisifu, Hisani Zako Kuu.

3. Nitatoa Nini? Kwanza Vyote Vyako.
Upendo Wako Wadai, Moyo Wa Shurani,
Upendo Wako Wadai, Moyo Wa Shurani.

4. Nipewe Neema, Niwe Na Uwezo
Wakuishi Kwako, Bwana: Siku Zangu, Zako,
Wakuishi Kwako, Bwana: Siku Zangu, Zako.

(NK # 10) KRISTO WA NEEMA YOTE
(Come, Thou Fount)

1.Kristo Wa Neema Yote Imbisha Moyo Wangu
Mifulizo Ya Baraka Inaamsha Shangwe Kuu.
Unifunze Nikupende, Nikuandame Kote,
Moyo Wangu Ukajae Furaha Na Tumai.

2.Namshukuru Sana Bwana, Aniwezesha Huku.
Salama Aniongiza Hata Kule Nyumbani.
Yesu Alinitafuta Njiani Mbali Kwake,
Akatoa Damu Yake Nipone Hatarini.

3.Kweli Mimi Mwiwa Mkubwa Wa Neema Daima;
Wema Wako Unifunge Zaidi Kwako Bwana.
Ili Nisivutwe Tena Kukuacha, Ee Mponya,
Nitwalie Moyo Wangu Uwe Wako Kamili.
(NK # 11) JINA LA BWANA LI HERI
(O For Thousand Tongues)

1.Sauti Zote Ziimbe, Jina La Yesu Li Heri!
Sifa Za Mfalme Mungu, Jina La Yesu Li Heri!

Jina Li Heri, Jina Li Heri, Jina La Yesu Li Heri.
Jina Li Heri, Jina Li Heri, Jina La Yesu Li Heri.

2.Hofu Zote Latuliza, Jina La Yesu Li Heri!
Mwenye Dhambi Hukubali, Jina La Yesu Li Heri.

3.Huvunja Nguvu Za Dhambi, Jina La Yesu Li Heri,
Damu Yake Hutakasa, Jina La Yesu Li Heri.

4.Sauti Yake Ni Tamu, Jina La Yesu Li Heri.
Wakaburini Husikia, Jina La Yesu Li Heri.

5.Lugha Maelf(U) Zitaimba, “Jina La Yesu Li Heri.
Astahili Mwana-Kondoo, Jina La Yesu Li Heri.”

(NK # 12) MSIFU MUNGU
(Praise God From Whom)

1. Msifu Mungu Wa Neema,
Enyi Viumbe Po Pote;
Wa Juu Pia Sifuni
Baba, Mwana Naye Roho!

Praise God, From Whom All Blessings Flow;
Praise Him, All Creatures Here Below;
Praise Him Above, Ye Heavenly Host;
Praise Father, Son, And Holy Ghost.

(NK # 13) YESU UJE KWETU
(Jesus, Thou Hast Promised)

1.Umetuahidi Kwamba Wawili,
Watatu, Kwa Jina, Lako Wakija,
Utawabariki; Kwa Hivi Leo,
Twapiga Magoti Nyumbani Pako.

Yesu Uje Kwetu Utubariki;
Yesu Uje Kwetu Uwe Karibu.

2.Umekuwa Nasi Siku Nyingine
Tunakuhitaji Mpaka Mwisho,
Uje Mkombozi; Tupe Neema;
Tisikie Yesu, Utubariki.

3.Uje Utawale Sauti Zetu:
Nyimbo, Nazo Sala Uziagize.
Imani Izidi , Ikamilike;
Pendo Liwe Safi, Na Njia Nuru.

(NK # 14) NITEMBEE NAWE (O Let Me Walk With Thee)

1.Nitembee Nawe Mungu
Alivyotembea Enok;
Mkono Wangu Uushike;
Unene Nami Kwa Pole;
Ingawa Njia Siioni,
Yesu Nitembee Nawe.

2.Siwezi Tembea Pekee;
Pana Dhoruba Mbinguni;
Mitego Ya Miguu Elfu;
Adui Wengi Hufichwa;
Uitulize Bahari,
Yesu Nitembee Nawe.

3.Ukinishika Mkono,
Anasa Kwangu Hasara;
Tautwika Msalaba;
Hata Mji Wa Sayuni
Yesu Nitembee Nawe.
(NK # 15) NENA ROHONI YESU
(Speak To My Soul)

1.Nena Rohoni Yesu, Nena Kwa Upole
Sema Kwangu Kwa Pendo, “Huachwi Upweke.”
Fungua Moyo Wangu, Nisikie Mara;
Jaza Roho Na Sifa, Sifa Zako Bwana.
Kila Siku Unene, Vile Kwa Upole.
Nong’oneza Kwa Pole Wa Upendo:
“Daima Utashinda, Uhuru Ni Wako.”
Nisikie Maneno: “Huachwi Upweke.”

2.Nena Kwa Wana Wako, Waonyeshe Njia,
Wajaze Kwa Furaha, Fundisha Kuomba;
Wajifunze Kutoa Maisha Kamili,
Wahimize Ufalme, Tumwone Mwokozi.

3.Nena Kama Zamani, Ulipoitoa
Sheria Takatifu: Niiweke Pia;
Nipate Kutukuza Wewe Mungu Wangu,
Mapenzi Yako Tena, Daima Kusifu.
(NK # 16) NINAKUHITAJI
(Blessed Lord, How Much I Need Thee!)

1. Bwana Ninakuhitaji Nimpofu, Maskini;
Unishike Mkononi, Kwako Napata Nguvu.

Kila Saa, Kila Saa Bwana Ninakuhitaji;
Kila Saa, Kila Saa Unilinde Kila Saa.

2. Univike Na Mavazi Ya Usikivu Wako;
Nguo Zangu Mi Machafu, Nazitamani Zako.

3. Wewe Ukiniongoza Nitakwenda Salama;
Nenda Nami Siku Zote, U Nuru Na Uzima.

4. Na Ikiwa M-Beleni Sehemu Yangu Ngumu,
Au Ikiwa Furaha, Unilinde Kila Saa.
(NK # 17) SI MIMI, KRISTO (Not I, But Christ)

1.Si Mimi, Kristo Astahile Sifa;
Si Mimi, Kristo Ajulikane;
Si Mimi, Kristo Katika Maneno
Si Mimi, Kristo Kwa Kila Tendo.

2.Si Mimi, Kristo Kuponya Huzuni;
Kristo Pekee, Kufuta Machozi;
Si Mimi, Kristo, Kubeba Mzigo
Si Mimi, Kristo, Kupunga Hofu.

3.Kristo Pekee, Pasipo Kujisifi;
Kristo Pekee, Na Nisizungumze
Kristo Pekee, Na Hakuna Kiburi;
Kristo Pekee, Sifa Yangu Ife.

4.Kristo Pekee, Amhitaji Atoe
Si Mimi, Kristo, Kisima Changu;
Kristo Pekee, Kwa Nwile Na Kwa Moyo.
Simimi, Kristo, Hata Milele.
(NK # 18) MWOKOZI,KAMA MCHUNGA.
(Saviour, Like A Shephered)

1.Mwokozi, Jama Mchunga
Utuongoze Leo;
Ututume Malishoni;
Fanya Tayari Boma.
Bwana Yesu, Peke Yako
Umetuvuta Kako.

2.Tu Wako, Uwe Rafiki,
Uwe Mlinzi Wetu;
Kundi Lako Ulilinde,
Tusivutwe Na Dhambi;
Bwana Yesu, Tusikie,
Tukiomba, Samehe.

3.Umetuahidi Kwamba
Utakubali Watu;
Utawahurumia Na
Utawapa Neema;
Bwana Yesu, Tunapenda
Kuwa Wako, Mapema.
(NK # 19) MSALABANI PA MWOKOZI
(Down At The Cross)

1.Msalabani Pa Mwokozi Hapo Niliomba Upozi,
Moyo Wangu Ulitakaswa, Na Asifiwe.

Na Asifiwe, Na Asifiwe.
Alinikomboa Kwa Damu, Na Asifiwe.

2.Chini Ya Mti Msumbufu Niliomba Utakatifu,
Alinikomboa Kwa Damu, Na Asifiwe.

3.Kwa Ajabu Ninaokoka, Yesu Anakaa Moyoni;
Mtini Alinifilia, Na Asifiwe.

4.Damu Ya Yesu Ya Thamani Huniokoa Makosani;
Huniendesha Wokovuni, Na Asifiwe.
(NK # 20) MUNGU WETU YEYE MWAMBA
(The Lord Is Our Rock)

1. Mungu Wetu Yeye Mwamba, Kimbilio Taabuni;
Msaada Penye Shida Ulio Karibu Sana.

Mwamba Wetu Kutupumzisha,
Yu Kivuli Kuburudisha
Yu Mwongozi Katika Njia,
Kimbilio Taabuni.

2.Mchana Usiku,Yule Kimbilio Taabuni,
Hivyo Hatuta Ogopa, Kwani Yu Karibu Sana.

3.Iwayo Yote, Yeye Tu Kimbilio Taabuni,
Twamjua Yeye Mlinzi Aliye Karibu Sana.

4.Mungu Wetu Ficho Kwetu, Kimbilio Taabuni.
Siku Zote Uwe Boma Lililo Karibu Sana.
(NK # 21) BABA TWAKUJIA
(Father,We Come To Thee)

1.Baba Twakujia, Uwe Msaada;
Uwe Kimbilio, Twakusihi.
Dunia Ni Giza Tukitengwa Nawe;
Tufariji Hapa, Baba Yetu.

Baba Twakujia, Tu Dhahifu,
Usitugeue, Tusikie.

2.Salama Tulinde, Kati Ya Taabu;
Uwe Raha Yetu Mashakani.
Roho Yasumbuka, Baba Tujalie;
Twakuomba Sana, Tupe Nguvu.

3.Neema Utupe, Tukubali Kwako;
Moyo Wetu Linda, Safarini;
Tuongoe Mbele, Tupate Kushinda
Na Kufika Ng’ambo, Kule Kwako.

(NK # 22) USINIPITE
(Pass Me Not)

1. Usinipite, Mwokozi, Unisikie;
Unapozuru Wengine, Usinipite.

Bwana, Bwana, Unisikie;
Unapozuru Wengine, Usinipite.

2.Kiti Chako Cha Rehema, Nakitazama;
Magoti Napiga Pale, Nisamehewe.

3.Sina Ya Kutegemea, Ila Wewe Tu;
Uso Wako Uwe Kwangu: Nakuabudu.

4.Wewe Tu U Mfariji: Sina Mbinguni,
Wala Duniani Pote, Bwana Mwingine.
(NK # 23) YESU FURAHA YA MOYO
(Jesus, Thou Joy Of Loving Hearts)

1. Yesu, Furaha Ya Moyo! Hazina Ya Pendo Na Nuru.
Yote Yatupendezayo, Yasilinganishwe Nawe.

2. Kweli Yako Ya Daima, Wawajibu Wakwitao,
Ni Siku Zote U Mwema Kwao Wakutafutao.

3. U Mkate Wa Uzima, Kupokea Ni Baraka,
Twanywa Kwako U Kisima Roho Zikiburidika.

4. Mwokozi Twakutamani, Kwako Roho Hutulia;
Twakushika Kwa Imani, Nawe Watubarikia.

5. Yesu, Ndiwe Kwetu Mwanga, Tufufahishe Daima;
Giza Ya Dhanbi Fukuza, Uwe Nwanga Wa Uzima.

(NK # 24) JINA LAKE YESU TAMU
(How Sweet The Name Of Jesus Sounds)
1. Jina Lake Yesu Tamu Tukilisikia,
Hutupoza, Tena Hamu Hutuondolea,

2. Roho Iliyoumia Kwalo Hutibika,
Chakula, Njaani Pia; Raha, Tukichoka.

3. Jina Hili Ni Msingi, Ngao, Ngome, Mwanba,
Kwa Hili Napata Ungi, Kwangu Ni Akiba.

4. Yesu, Mchunga, Rafiki, Mwalimu, Kuhani,
Mwanzo, Mwisho, Na Amina, Mali Yangu Yote!

5. Moyo Wangu Hauwezi Kukusifu Kweli;
Ila Sifa Zangu Hizi, Bwana, Zikubali.

(NK # 25) TAJI MVIKENI
(Crown Him With Many Crowns)

1. Taji Mvikeni. Taji Nyingi Sana,
Kondoo Nwake Kitini, Bwana Wa Mabwana;
Nami Tamsifu Alikufa Kwangu,
Ni Mfalme Mtukufu, Seyidi Wa Mbingu.

2. Taji Mvikeni Mwana Wa Bikira;
Anazo Vaa Kichwani Aliteka Nyara;
Shilo Wa Manabii Mchunga Wa Watu
Shina Wa Tanzu Ya Yese Wa Bethilehemu.

3. Taji Mvikeni Bwana Wa Mapenzi;
Jeraha Zake Ni Shani Ni Vito Vya Enzi,
Mbingu Haina Hata Malaika
Awezaye Kuziona Pasipo Kushangaa!

4. Taji Mvikeni Bwana Wa Salama;
Kote-Kote Duniani Vita Vitakoma;
Nayo Enzi Yake Itaendelea,
Chini Ya Miguu Yake, Maua Humea.

(NK # 26) TUTOKAPO TUBARIKI
(Lord, Dismiss Us)

1. Tutokapo Tubariki,Utupe Kufurahi;
Tuwe Na Upendo Wako, Neema Ya Kushinda.
Nawe Utuburudishe Tukisafiri Chini.

2. Twatoa Sifa, Shukurani Kwa Neno Ya Injili;
Matunda Ya Wokovu Yaonekane Kwetu;
Daima Tuwe Amini Kwa Kweli Yako, Bwana.

3. Siku Zetu Zikizidi Tuzitoe Kwa Yesu;
Tuwe Na Nguvu Moyoni Tusichoke Njiani;
Hata Tutakapo Ona Utukufu Wa Bwana.

(NK # 26A) TUPE AMANI
(God The Omnipotent)

1. Mungu Mtukufu Aliyeumba
Pepo Kuvuma Na Radi Kali;
Toa Neema Unapotawala,
Tupe Amani Bwana Wa Wama.

2. Mungu Wa Neema, Nchi Imeacha
Amri Tukufu Na Neno Lako;
Hasira Zako Zisituharibu,
Tupe Amani, Bwana Wa Wema.

3. Mwumbaji Wa Haki, Watu Wa Baya
Wamedharau Utukufu Wako;
Lakini Wema Wako Utadumu;
Endesha Kweli Bwana Wa Wema.

4. Tuna Kutolea Ibada Safi
Kwa Ajili Ya Wokovu Wako;
Hivi Tuna Ziimba Sifa Zako;
Wako Uwezo Na Utukufu.

(NK # 27) TENA,MWOKOZI,JINA LAKO
(Saviour Again To Thy Dear Name)

1. Tena, Mwokozi,Twalitukuza
Jina Lako Lenye Kupendeza,
Twakungojea Neno La Amani,
Kabla Hatujakwenda Nyumbani.

2. Tupe Amani Njiani Mwetu.
Wewe U Mwanzo,U Mwisho Wetu;
Dhambini Kamwe Isiingie
Midomo Ikutajayo Wewe.

3. Utupe Amani Usiku Huu,
Ili Gizani Kuwe Nuru Kuu.
Tulinde Kwa Kuwa Kwako Bwana.
Usiku Ni Sawa Na Mchana .

4. Tupe Amani Ulimwenguni
Ndiyo Dawa Yetu Majonzini;
Na Ikitwita Sauti Yako,
Tupe Amani Milele Kwako.

(NK # 28) JINA LA THAMANI
(Take The Name Of Jesus)

1. Jani Lake Yesu Tamu, Lihifadhi Moyoni;
Litakufariji Ndugu, Enda Nalo Po Pote.

Jina La Thamani,
(Thamani) (Thamani)
Tumai Ya Dunia
Jina La Thamani,
(Jina La Thamani—Tamu!)
Furaha Ya Mbinguni.

2. Jina La Yesu Lafaa Kama Ngao Vitani.
Majaribu Ya Kisonga, Omba Kwa Jina Hili.

3. Jina Hili La Thamani Lina-Tufurahisha,
Anapotukaribisha, Na Tunapomwibia.

4. Mwisho Wa Safari Yetu Tutakapo Msujudu,
Jina Hili Tutasifu Furaha Ya Mbinguni.
(NK # 29) YESU NAKUPENDA
My Jesus, I Love Thee

1. Yesu Nakupenda, Umali Yangu,
Anasa Za Dhambi Sitaki Kwangu;
Na Mwokozi Aliye Niokoa
Sasa Nakupenda, Kuzidi Pia.

2. Moyo Umejaa Mapenzi Tele
Kwa Vile Ulivyonipenda Mbele,
Uhai Wako Ukanitolea
Sasa Nakupenda, Kuzidi Pia.

3. Ulipo Angikwa Msalabani
Tusamehewe Tulio Dhambini;
Taji Ya Miiba Ulihiyoivaa,
Sasa Nakupenda, Kuzidi Pia.

4. Mawanda Mazuri Na Masikani
Niyatazamapo Huko Mbinguni,
Tasema Na Taji Nitakayovaa
Sasa Nakupenda, Kuzidi Pia.

(NK # 30) YESU, UNIPENDAYE
Jesus, Lover Of My Soul.

1. Yesu Unipendaye, Kwako Na Kimbilia,
Ni Wewe Unitoshaye, Mwovu Akinijia.
Yafiche Ubavuni, Mwako Maisha Yangu;
Nifiche Bandarini, Wokoe Moyo Wangu.

2. Ngome Nyingine Sina; Nategemea Kwako;
Usinitupe Bwana, Nipe Neema Yako,
Ninakuaminia, Mwenye Kuniwezesha;
Shari Wani Kingia, Vitani Wani Tosha.

3. Nakutaka Mpaji, Vyote Napata Kwako,
Niwapo Muhitaji, Utanijaza Vyako;
Nao Wa Angukao, Wanyonge Wape Nguvu;
Poza Wauguao, Uongoze Vipofu.

4. Bwana Umeniosha, Moyo Kwa Damu Yako;
Neema Ya Kutosha, Ya Patikana Kwako;
Kwako Bwana Naona, Kisima Cha Uzima;
Mwangu Moyoni, Bwana, Bubujika Daima.

(NK # 31) NIIMBE PENDO LAKE
I Will Sing Of Jesus Love

1. Niimbe (Niimbe) Pendo Lake,
Pendo La (Pendo La) Yesu Bwana;
Sababu (Sababu) Alitoka; Kwa Baba, Akafa.

Niimbe (Niimbe) Pendo Lake;
Sifa Kuu (Sifa Kuu) Nitatoa;
Akafa (Akafa) Niwe Hai,—– Niimbe Pendo Lake.

2. Machozi (Machozi) Alitoa; Ijapo (Ijapo) Sijalia;
Maombi (Maombi) Yangu Bado, Ani-Ombe-Apo.

3. Upendo (Upendo) Kubwa Huo!
Dunia (Dunia) Haijui
Samaha (Samaha) Kwa Makossa; Kubwa Kama Yangu.

4. Hapana (Hapana) Tendo Jema
Ambalo (Ambalo) Nilitenda,
Nataka (Nataka) Toka Leo; Nimwonyeshe Pendo.
(NK # 32) TANGU KUAMINI
I Have A Song I Love To Sing

1. Ninao Wimbo Mzuri, Tangu Kuamini;
Wa Mkombozi, Mfalme, Tangu Kuamini.

Tangu Kuamini, Jina Lake Tasifu,
Tangu Kuamini, Nita Lisifu Jina Lake.

2. Kristo Anitosha Kweli, Tangu Kuamini,
Mapenzi Yake Napenda, Tangu Kuamini.

3. Ninalo Shuhuda Sawa, Tangu Kuamini;
Linalofukuza Shaka, Tangu Kuamini.

4. Ninalo Kao Tayari, Tangu Kuamini;
Nililorithi Kwa Yesu, Tangu Kuamini.
(NK # 33) KARIBU SANA
(Nearer, Still Nearer)

1. Karibu Sana Univute,
Karibu Sana Daima Niwe.
Bwana Napenda Unishike,
Unilinde Nisi Tengwe Nawe, Unilinde Nisitengwe Nawe.

2. Karibu Sana, Sina Kitu,
Sina Asadaka Kwa Bwana Yesu,
Isipokuwa Moyo Wangu:
Uutakase Katika Damu, Uutakase Katika Damu.

3. Karibu Sana, Wewe Nami.
Nima Furahi Kuacha Dhambi—-
Anasa Zote Na Kiburi:
Nipe Yesu Niliyemsulibi, Nipe Yesu Niliyemsulibi.

4. Karibu Sana. Hata Mwisho.
Hata Mbinguni Nisimamapo:
Daima Dawamu Niwepo
Nitakapoona Uso Wako, Nitakapoona Uso Wako.

(NK # 34) HADITHIA KISA CHA YESU
Tell Me The Story Of Jesus

1. Nipe Habari Za Yesu, Kwangu Ni Tamu Sana;
Kisa Chake Cha Thamani, Hunipendeza Sana.
Jinsi Malaika Wengi, Walivyoimba Sifa,
Alipoleta Amani, Kwa Watu Wa Dunia.

Nipe Habari Za Yesu, Kaza Moyoni Mwangu;
Kisa Chake Cha Thamani Hunipendeza Sana.

2. Kisa Cha Alivyofunga, Peke Yake Jangwani.
Jinsi Alivyolishinda, Jaribu La Shetani;
Kazi Aliyoifanya, Na Siku Za Huzuni,
Jinsi Walivyomtesa: Yote Ni Ya Ajabu!

3. Habari Za Msalaba, Aliposulubishwa;
Jinsi Walivyo Mzika, Akashinda Kaburi.
Kisa Chake Cha Rehema, Upendo Wake Kwangu, Aliyetoa Maisha, Nipokee Wokovu.

(NK # 35) NIMEKOMBOLEWA NA YESU
Redeemed! How I Love To Proclaim It

1. Nimekombolewa Na Yesu Na Sasa Nimefurahi;
Kwa Bei Ya Mauti Yake Mimi Ni Mtoto Wake.

Kombolewa! Nakombolewa Na Damu;
Kombolewa! Mimi Mwana Wake Kweli.

2. Kukombolewa Na Furahi, Kupita Lugha Kutamka;
Kulionyesha Pendo Lake, Mimi Ni Mtoto Wake.

3. Nitamwona Mfalme Wangu Katika Uzuri Wake;
Ambaye Twajifurahisha Katika Torati Yake.

4. Najua Taji Imewekwa Mbinguni Tayari Kwangu;
Muda Kitambo Atakuja, Ili Alipo, Niwepo.

(NK # 36) SIKU KUU
Oh Happy Day!

1. Ni Siku Kuu Siku Ile, Ya Kumkiri Mwokozi!
Moyo Umejaa Tele, Kunyamaza Hauwezi.

Siku Kuu! Siku Kuu!
Ya Kwoshwa Dhambi Zangu Kuu!
Hukesha Na Kuomba Tu,
Ananiongoza Miguu.
Siku Kuu! Siku Kuu!
Ya Kwoshwa Dhambi Zangu Kuu.

2. Tumekwisha Kupatana, Mimi Wake Yeye Wangu,
Na Sasa Nitamwandama, Nikiri Neno La Mungu.

3. Moyo Tulia Kwa Bwana, Kiini Cha Raha Yako:
Huna Njia Nbili Tena: Uwe Naye, Yote Ndako.

(NK # 37) PENDO LAKO, EE MWOKOZI
Love Divine, All Loves Excelling

1. Pendo Lako, Ee Mwokozi, Hushinda Pendo Zote!
Kaa Nasi, Ndani Yetu, Furaha Ya Mbinguni.
Yesu, U Rehema Tupu. Safi Na Kusamehe,
Mfariji Mwenye Huzuni Ziondoe Machozi.

2. Roho Yako Ya Upendo Tuma Kwa Kundi Lako;
Hebu Tuirithi Raha, Iliyoahidiwa.
Uondoe Moyo Mbaya, U Mwanzo, Tena Mwisho
Timiza Imani Yetu, Ili Tuwekwe ‘ Huru.

3. Yesu, Uje Kwetu Sasa, Tupokee Huruma;
Rudi Kwetu, Tena Kamwe Usutuache Pekee.
Tungekutukuza Leo, Pamoja Ma Malaika,
Imba Na Kutoa Sifa, Ingia Kwa Ibada.

4. Sasa, Bwana, Kazi Yako, Imalize Moyoni;
Takasa Hekalu Lako, Wokovu Kamilisha !
Safisha Viumbe Vyako Katika Wakati Huu:
Tupumzike ‘Toka Dhambi, Tuingie Mbinguni.

(NK # 38) NASIFU SHANI YA MUNGU
I Sing The Mighty Power

1. Nasifu Shani Ya Mungu, Mweneza Bahari,
Muumba Pia Wa Mbingu, Jua, Nyota, Mwezi,
Ni Tukufu Yaki Shani, Mtengeza Mambo
Ya Nyakati Na Zamani, Yasiyo Na Mwisho.

2. Kadiri Ya Nionayo, Ya Kusifu Mungu:
Nchi Niikanyagayo, Na Hayo Mawingu;
Hakuna Hata Unyasi, Usiokukuza;
Na Upepo Wavumisha, Au Kutuliza.

3. Nami Kwa Mkono Wako, Naongozwa Sawa,
Ni Pato Nikusifupo, Kukwomba Ni Dawa;
Umenizingira Nyuma, Na Mbele Baraka,
Maarifa Ya Ajabu! Yanishinda Mimi!
(NK # 39) ATI, KUNA MVUA NJEMA
Lord, I Hear Of Showers Of Blessing

1. Ati, Kuna Mvua Njema, Yanya Yenye Neema;
Watu Wanaona Vyema, Bwana, Huninyeshei?

Na Mimi? N Mimi? Bwana, Huninyeshei?

2. Sinipite, Baba Mwema; Dhanbini Nimezama:
Rehema Ni Za Daima; Bwana, Hunionyeshi?

3. Sinipite, Yesu Mwema; Niwe Nawe Daima,
Natamani Kukwandana: Bwana, Hunichukui?

4. Sinipite, Roho Mwema, Mpaji Wa Uzima,
Nawe Shahidi Wa Wema, Bwana Wema Hunipi?

(NK # 40) NIJAZE SASA
Hover O’er Me, Holy Spirit

1. Njoo, Roho Mtukufu Uoshe Moyo Wangu,
Utakase Nia Yangu, Njoo, Nijaze Sasa.

Roho Mtukufu, Njoo, Nijaze Sasa;
Utakase Nia Yangu, Njoo, Nijaze Sasa.

2. Ujalize Moyo Wangu Ijapo Sikuoni,
Nami Ninakuhitaji, Njoo, Nijaze Sasa.

3. Nimejaa Udhaifu, Nainamia Kwako;
Roho Mtukufu Sasa, Nitilie Na Nguvu.

4. Unioshe, Nifariji, Niponye, Nibariki,
Unijaze Moyo Wangu: Ndiwe Mwenye Uwezo.
(NK # 41) ROHO MTAKATIFU
Holy Spirit, Faithful Guide

1. Roho Mtakatifu, Kiongozi Animi;
Utushike Mkono Tulio Wasafiri;
Utupe Kusikia Sauti Ya Upole:
“Msafiri Fuata, Naongoza Nyambani.

2. Wewe Ndiwe Rafiki, Msaada Karibu;
Tusiache Shakani; Na Tukiwa Gizani
Utupe Kusikia Sauti Ya Upole:
“Msafiri Fuata, Naongoza Nyambani.

3. Siku Zetu Za Ka Zi, Zikiwa Zimekwisha,
Wala Hatuna Tamaa Ila Mbingu Na Sala:
Utupe Kusikia Sauti Ya Upole:
“Msafiri Fuata, Naongoza Nyambani.

(NK # 42) EWE ROHO WA MBINGUNI
Spirit Divine, Attend Our Prayer

1. Ewe Roho Wa Mbinguni, Maombi Sikia
Makao Yako Yafanye Mioyoni Mwetu.

2. Kama Nuru, Tupenyeze, Giza Uondoe;
Siri Yako Tuione, Na Amani Yako.

3. Kama Moto, Tusafishe, Choma Dhambi Yetu;
Roho Zetu Ziwe Zote Hekalu La Bwana.

4. Kama Umande, Na Uje, Utuburudishe,
Moyo ‘Kavu Utakuwa Ni Wenye Baraka.

5. Kama Upepo Ee Roho, Katika Pentekoste
Ukombozi Utangaze, Kwa Kila Taifa.

(NK # 43) FURAHA GANI!
What A Felloship

1. Furaha Gani Na Ushiriki
Niki Mtegimea Yesu Tu!
Baraka Gani, Tena Amani,
Niki Mtegimea Yesu Tu!

Tegemea, Salama Bila Hatari;
Tegemea, Tegemea Mwokozi Yesu.

2. Nitaiweza Njia Nyenbamba,
Niki Mtegimea Yesu Tu!
Njia ‘Tazidi Kuwa Rahisi
Niki Mtegimea Yesu Tu!

3. Sina Sababu Ya Kuogopa
Niki Mtegimea Yesu Tu!
Atakuwa Karibu Daima
Niki Mtegimea Yesu Tu!

(NK # 44) URAFIKI WA YESU
There’s Not A Friend

1. Hakuna Rafiki Kama Yesu, Hakuna, Hakuna!
Tabibu Mwingine Wa Rohoni, Hakuna, Hakuna!

Yesu Ajua Shida Zetu; Daima Ataongoza.
Hakuna Rafiki Kama Yesu, Hakuna, Hakuna!

2. Wakati Ambapo Hapo Yeye, Hapana, Hapana!
Wala Giza Kututenga Naye, Hapana, Hapana!

3. Aliyesahauliwa Naye, Hakuna, Hakuna!
Mkosoji Asiyempenda, Hakuna, Hakuna!

4. Kipawa Kama Mwokozi Wetu, Hakuna, Hakuna!
Ambaaye Atanyimwa Wokovu, Hakuna, Hakuna!

(NK # 45) MWANGA UMO MOYONI
There Is Sunlight On The Hilltop

1. Mlimani Pana Mwanga, Mwanga Wa Jua Zuri
Shambani Na Bahari Jua Tukufr Liko;
Mwnga Ulio Mkubwa Umo Moyoni Mwangu,
Kwa Kuwa Yesu Alipo Hapa Pana Mwangaza.

Mwangaza Ulio Mzuri, Mwanga Umo Moyoni;
Akiwapo Bwana Yesu Pana Mwanga Moyoni.

2. Kama Mavazi Kikuu Ninavua Huzuni:
Nguo Nzuri Za Furaha Umenipa Za Kuvaa.
Nakuandana Rohomi Hata Nyumba Ya Juu
Iliyo Pambwa Vizuri Katika Pendo Lako.

3. Ulinikomboa Yesu; Maisha Yangu, Mali,
Vyote Ni Vyako, Mwokozi-Daima Nikusifu.
Nakuandana Rohomi Hata Nyumba Ya Juu
Iliyo Pambwa Vizuri Katika Pendo Lako.

(NK # 46) MIGUUNI PAKE YESU
Sitting At The Feet Of Jesus

1. Miguuni Pake Yesu Maneno Yake Tamu;
Pahali Palipo Heri, Niwepo Kila Siku
Miguuni Pake Yesu Nakumbuka Upendo
Na Hisani Vyake Kwangu, Vimenivuta Moyo.

2. Miguuni Pake Yesu, Hapa Pahali Bora
Pa Kuweka Dhambi Zangu: Pahali Pa Pumziko.
Miguuni Pake Yesu, Hapa Nafanya Sala,
Kwake Napewa Uwezo, Faraja Na Neema.

3. Unibariki Mwokozi, Ni Miguni Pako,
Unitazame Kwa Upendo Nione Uso Wako.
Nipe Bwana Nia Yake Ili Ionekane
Nimekaa Na Mwokozi Aliye Haki Yangu.

(NK # 47) NI HERI KIFUNGO
Blest Be The Tie That Blinds

1. Ni Heri Kifungo Kinachotufunga
Mioyo Yetu Kwa Pendo Pendo La Kikristo

2. M-Bele Ya Baba Tunatoa Sala;
Hofu, Nia, Masumbufu Yetu Ni Mamoja.

3. Tunavishiriki Matata Na Shida,
Na Mara Nyingi Twatoa Shozi La Fanaka.

4. Tunapoachana Moyoni Twalia;
Lakini Tutakutana M-Wisho Mbinguni.
(NK # 48) NINAKUPENDA ZAIDI
I Know I Love Thee Better, Lord

1. Nina Kupenda Zaidi, Ya Vyote Vingine;
Kwani Umenipa Raha, Na Amani Bwani.

Nusu Haijatangazwa (Tangazwa)
Ya Upendo Wako;
Nusu Haijatangazwa (Tangazwa)
Damu Hutakasa (Takasa)

2. Nakujua U Karibu Kuliko Dunia;
Kukukumbuka Ni Tamu Kuliko Kuimba.

3. Kweli Wanifurahisha, Nanita Furahi;
Pasipo Upendo Wako Naona Huzuni.

4. Itakuwaje Mwokozi, Kukaa Na Wewe,
Ikiwa Ulimwenguni Tuna Furaha Hii?

(NK # 49) NINAYE RAFIKI
I’ve Found A Friend

1. Ninaye Rafiki Naye Alinipenda Mbele;
Kwa Kamba Za Pendo Lake Nimefungwa Milele;
Aukaza Moyo Wangu, Uache Ugeuzi,
Ninakaa Ndani Yake, Yeye Kiwangu, Milele.

2. Ninaye Rafiki Ndiye Aliyenifilia;
Alimwaga Damu Yake Kwa Watu Wote Pia;
Sina Kitu Mimi Tena, Nikiwa Navyo Tele;
Pia Vyote Ni Amana Ndimi Wake Milele.

3. Ninaye Rafiki Naye Uwezo Amepewa;
Atanilinda Mwenyewe, Juu ’Tachukuliwa;
Nikizama Mbinguni Hupata Nguvu Tele;
Sasa Natumika Chini, Kisha Juu Milele.

4. Ninaye Rafiki Naye Yuna Na Moyo Mwema,
Ni Mwalimu, Kiongozi, Mlinzi Wa Daima;
Ni Nani Wa Kunitenga Na Mpenzi Wa Mbele?
Kwake Nimetia Nanga, Ndimi Wake Milele.

(NK # 50) MUNGU NAWE NANYI DAIMA
God Be With You!

1. Mungu Nawe Nanyi Daima; Hata Twonane Ya Pili,
Awachunge Kwa Fadhili, Mungu Nawe Nanyi Daima.

Hata Twonane Juu,
Hata Twonane Tena Kwake;
Hata Twonane Juu,
Mungu Nawe Nanyi Daima.

2. Mungu Nawe Nanyi Daima; Awafunike Mabawa,
Awalishe, Awakuze; Mungu Nawe Nanyi Daima.

3. Mungu Nawe Nanyi Daima; Kila Wakati Wa Shida
Awalinde Hifadhini; Mungu Nawe Nanyi Daima.

4. Mungu Nawe Nanyi Daima; Awabariki Na Pendo
Ambalo Halina Mwisho; Mungu Nawe Nanyi Daima.

(NK # 51) KUWA NA YESU
Blessed Assurance

1. Yesu Mwokozi, Kwa Hakika .
Hunipa Furaha Na Amani;
Mrithi Wa Wokovu Wake,
Natakaswa Kwa Damu Yake.

Habari Hiyo Wimbo Wangu, Daima Nitamsifu Yesu.
Habari Hiyo Wimbo Wangu, Daima Nitamsifu Yesu.

2. Nijitoapo Nina Raha,
Na Kwa Imani Namwona Bwana;
Aniletea Malaika,
Wananilinda Niokoke.

3. Hali Na Mali Anaitwaa,
Katika Yesu Nabarikiwa;
Nikimngoja Kwa Subira,
Wema Wake Unanitosha.

(NK # 52) NIPE BIBLIA
Give Me The Bible

1. Nipe Biblia Nyota Ya Furaha, Wapate Nuru Wasafirio;
Hakuna La Kuzuia Amani, Kwani Yesu Alituokoa.

Nipe Biblia Neno Takatifu,
Nuru Yake Itaniongoza;
Sheria Na Ahadi Na Upendo,
Hata Mwisho Vitaendelea.

2. Nipe Biblia Nihuzunikapo; Ikinijaza Moyoni Dhambi;
Nipe Neno Zuri La Bwana Yesu,
Nimwone Yesu Mwokozi Wangu.

3. Nipe Biblia Biblia Nipate Kuona, Hatari Zilizo Duniani;
Nuru Ya Neno Lake Bwana Yesu,
Itaangaza Njia Ya Kweli.

4. Nipe Biblia Taa Ya Maisha; Mfariji Tunapofiliwa;
Unionyeshe Taa Ya Mbinguni,
Nione Utukufu Wa Bwana.

(NK # 53) Napenda Kuhubiri
I Love To Tell The Story

1. Napenda Kuhubiri Habari Za Yesu,
Za Bwana Wa Fahari, Na Pendo Zake Kuu.
Kuhubiri Na Penda, Kwa Hali Na Mali;
Mwenyewe Nimeonja, Najua Ni Kweli.

Napenda Kuhubiri Kisa Cha Bwana Yesu,
Ya Bwana Wa Fahari Na Pendo Zake Kuu.

2. Napenda Kuhubiri Mambo Ya Ajabu
Na Tukiyafikiri Yapita Dhahabu.
Kuhubiri Napenda Yaliyo Nifaa;
Nami Sana Napenda Hayo Kukwambia.

3. Napenda Kuhubiri, Hunifurahisha
Tamu Yake Habari Haiwezi Kwisha.
Napenda Kuhubiri Wa Gizani Nao;
Hawana Muhubiri Wa Kweleza Chuo

4. Kuhubiri Napenda Hata Wajuao;
Kusikia Hupendkama Wenzi Wao.
Nako Kwenye Fahari Nikiimba Wimbo,
Nitaimba Habari Ya Mwokozi Huyo
(NK # 54) NATAKA NIMJUE YESU
More About Jesus

1. Nataka Nimjue Yesu, Na Nizidi Kumfahamu,
Nijue Pendo Lake Tu, Wokovu Wake Kamili.

Zaidi, Zaidi, Nimfahamu Yesu,
Nijue Upendo Wake, Wokovu Wake Kamili.

2. Nataka Nione Yesu, Na Nizidi Kusikia
Anenapo Kitabuni, Kujidhihirisha Kwangu.

3. Nataka Tena Zaidi, Daima Kupambanua
Mapenzi Yake, Nifanye Yale Yanayompendeza.

4. Nataka Nikae Naye, Kwa Mazungumzo Matamu.
Nizidi Kuwaonyesha Wengine Wokovu Wake.

(NK # 55) TWAPANDA MAPEMA
Sowing In The Morning

1. Twapanda Mapema, Na Mchana Kutwa
Mbegu Za Fadhili Hata Jioni,
Twangojea Sasa Siku Za Kuvuna;
Tutashangilia Wenye Mavuno.

Wenye Mavuno, Wenye Mavuno,
Tutashangilia Wenye Mavuno.
Wenye Mavuno, Wenye Mavuno,
Tutashangilia Wenye Mavuno.

2. Twapanda Mwangani Na Kwenye Kivuli;
Tusishindwe Na Baridi Na Pepo;
Punde Itakwisha Kazi Yetu Hapa:
Tutashangilia Wenye Mavuno.

3. Twapanda Kwa Bwana Mbegu Kila Siku,
Tujapoona Taabu Na Huzuni;
Tuishapo Shinda Atatupokea:
Tutashangilia Wenye Mavuno.

(NK # 56) WAPONYENI WATU
(Rescue The Perishing)

1. Walio Kifoni, Nenda Waponye.
Uwatoe Walio Shimoni;
Wanao Anguka Uwainue;
Habari Njema Uwajulishe.
Walio Kido Wasokoeni,
Mwokozi Yuko Huwangojea

2. Wajapokawia Anangojea,
Awasubiri Waje Tobani;
Mwokozi Hawezi Kuwadharau,
Huwasamehe Tangu Zamani:

3. Na Ndani Ya Moyo Wa Wanadamu
Huwamo Shida, Tena Huzuni;
Lakini Kwa Yesu Kuna Rehema
Kuwa Ponya Na Kuwakoa.

4. Walio Kifoni, Nenda Waponye; Kazi Ni Yetu, Zawadi Iko;
Nguvu Kuhubiri Bwana Hutoa
Kwa Subira Tuwavute Sasa.
(NK # 57) USIKATAE KAZI
Ask Not To Be Excused

1. Usikatae Kazi Yake Bwana; Ukae Tayari Kuifanya Kazi;
Uende Po Pote Mungu Akwitapo,
Nawe Utaona Furaha Kazini.

Njoo, We! Usiikatae; Njoo, We! Uifanye Kazi;
Usikatae Kazi Yake Bwana,
Ili Hatimaye Usikatazwe Juu.

2. Usikatae Kazi Yake Bwana;
Kwa Nini Kawia? Fanya Kazi Leo.
Mavuno Meupe, Wachache Wavuni,
Onyesha Furaha Kwa Kazi Ya Bwana.

3. Usikatae Kazi Yake Bwana,
Kukataa Pendo Kwako Ni Hatari.
Saa Ya Rehema, Yesu Akiomba,
Ziengame Dhambi, Zifutwe Mbinguni.

(NK # 58) ZITAKUWA NYOTA TAJINI?
I Am Thinking Today

1. Leo Ninafikiri Ya Nnchi Nzuri Ninayotaka Kuiona;
Nisimamapo Karibu Na Mwokozi,
Tajini Zitakuwa Nyota?

Sijui Tajini Mwangu Kama Nyota
Zitang’aa Kila Wakati!
Nitakapoamka Katika Majumba,
Zitakuwa Nyota Tajini?

2. Kwa Nguvu Za Bwana Nita Fanya Kazi,
Nitavuta Roho Za Watu,
Ili Niwe Na Nyota Katika Taji,
Bwana Anapotupa Tunu.

3. Nita Kuwa Na Furaha Nikimwona,
Kuweka Miguuni Pake
Watu Waliyovutwa Kwa Ajili Ya
Kazi Yangu Na Roho Yake.
(NK # 59) FANYENI KAZI ZENU
Work, For The Night Is Coming

1. Fanyeni Kazi Zenu, Usiku Si Mbali;
Kesheni Saa Zenu Vumilieni;
Kwa Yesu Tumikeni Na Hiyo Injili.
Sana Wahubirini Watu Wa Mbali.

2. Fanyeni Kazi Zenu Giza Ya Songea;
Na Wengi Wenzi Wenu Wamo Gizani,
Msipoteze Moja Dakika Ni Hizi;
Bwana Atarejea Mwisho Wa Kazi.

3. Fanyeni Kazi Zenu, Hivi Jua Lachwa;
Wote Walio Kwenu Apenda Mungu;
Na Sisi Tumjuaye Na Tuwafundishe
Ili Yesu Ajaye Tumfurahishe.

(NK # 60) NITA KWENDA UTAKAPONITUMA
It May Not Be On The Mountain’s Height

1. Pengine Siyo Milimani Utakaponiita;
Pengine Siyo Baharini Wala Palipo Vita;
Lakini Unaponiita, Na Njia Siijui.
Bwana, Nitajibu, Ni Tayari Kwenda Uniagizapo.

Ukiwa Pamoja Nami, Bwana, Mlimani, Baharini,
Niende Utakapioniita; Nafuata Uendako.

2. Pengine Leo Kuna Neno, Neno Tamu La Pendo,
Ambalo Yesu Anataka Ninene Kwa Upole;
Ukiwa Pamoja Nami, Bwana, Nitamtafuta Leo
Yule Aliye Potea Mbali: Nitasema Upendavyo.

3. Pahali Pako Bila Shaka Pa Kuvuna Shambani,
Kazi Niwezayo Kufanya Kwa Yesu Mkombozi;
Hivi Nikikutegemea, Kwa Kuwa Wanipenda,
Mapenzi Yako Nitafanya, Na Niwe Upendavyo.

(NK # 61) BWANA, NAMI
I Have A Friend So Precious

1. Nimemwona Rafiki, Wa Thamani Kubwa,
Ana Ni Penda Kwa ‘Pole, Kwa Pendo Amini:
Kuishi Kutengwa Naye, La, Huku Siwezi,
Tunakaa Pamoja: Bwana Nami.

2. Pengine Ninachoka, Mimi Mdhaifu,
Ndipo Ninamtehemea, Alivyoalika;
Huniongoza Njiani, Pahali Pa Nuru
Twatembea Pamoja, Bwana Nami.

3. Namweleza Huzuni, Nafuraha Yangu,
Vile Vinavyosumbua, Vinavyopendeza;
Huniagiza Kutenda, Yanayonipasa
Twazungumza Pamoja, Bwana Nami.

4. Ajua Natamani, Kuwavuta Watu,
Hivyo Ananipeleka, Kutangaza Neno;
Nitangaze Pendo Lake, Kwa Nini Akafa;
Twahubiri Pamoja, Bwana Nami.

(NK # 62) NAPENDA KITABU CHAKE
I Love The Sacred Book Of God

1. Napenda Kitabu Chake, Kilichotoka Mbinguni,
Barua Kwangu Ya Bwana Ujumbe Wake Wa Upendo.

2. Humo Ndani Ya Kitabu Sura Ya Yesu Naona
Karatasi Zimekuwa, Wayo Zake Za Mwongozi.

3. Neno Lake Ni Maonju, Kubwe La Asali Tamu;
Natamani Kuuonja Ule Mkate Wa Uzima.

4. Mapenzi Yake Mwumbaji, Yanafunuliwa Humo;
Hazina Kuu Ya Hekima, Utajiri Wa Ajabu.

5. Mwangaza Wa Ulimwengu Angaza Humo Moyoni!
Uwe Mwandamizi Pote, Taa Ya Hatua Zangu.
(NK # 63) NIUONAPO MSALABA
When I Survey The Wondrous Cross

1. Niuonapo Msalaba,
Kristo Aliponifia;
Kwangu Pato Ni Hasara.
Kiburi Nakichukia.

2. Na Nisijivune, Bwana,
Ila Kwa Sadaka Yako;
Upuzi Sitaki Tena,
Zi Chini Ya Damu Yako.

3. Tangu Kichwa Hata Nyayo,
Zamwangwa Pendo Na Hamu.
Ndako Pweke Hamu Hiyo.
Pendo Zako Zimetimu

4. Vitu Vyote Vya Dunia,
Si Sadaka Ya Kutosha;
Pendo Zako Zaniwia,
Nafsi, Mali Na Maisha.

(NK # 64) PIGA PANDA YA INJILI.
Watchman Blow The Gospel Trumpet

1. Piga Panda Ya Injili, Onyesha Watu Wote;
Ili Anaye Sikia Atubu Aokoke.

Piga Panda Ya Injili, Uipige Kwa Nguvu;
Mungu Amekuagiza Mateka Wawe Huru.

2. Uipige Vilimani, Kwa Kila Tambarare;
Pande Zote, Miji Yote Isikie Injili.

3. Uipige Mipakani, Barabarani Pia;
Iwatangazie Wote, Wanakwitwa Na Baba.

4. Uipige! Watu Wengi Wataka Wawe Huru;
Waanbie Kwamba Yesu Asema “Njoni Kwangu.”

(NK # 65) TWENDENI ASKARI (Onward, Christean Soldiers)

1. Twendeni Askari, Watu Wa Mungu;
Yesu Yuki Mbele Tumwandame Juu
Ame Tangulia Bwana Vitani,
Twende Mbele Kwani Ndiye Amini.
Twendeni Askari, Watu Wa Mungu
Yesu Yuko Mbele, Tumwandame Juu.

2. Jeshi La Shetani, Likisikia
Jina La Mwokozi, Litakimbia;
Kelele Za Shangwe Zivume Pote;
Ndugu, Inueni Zenu Sauti.

3. Kweli Kundi Dogo, Watu Wa Mungu,
La Mababa Yetu Ni Letu Fungu
Hatutengwi Nao, Moja Imani
Tumaini Moja, Na Moja Dini.

4. Haya Mbele Watu Nasi Njiani,
Inieni Myoyo, Nanyi Sifuni;
Heshima Na Sifa Yake Mfalme,
Juu Hata Chini Sana Zivume.
(NK # 66) ROHO YANGU AMKA SASA
Awake My Soul

1. Roho Yangu Amka Sasa, Mara Jitahidi;
Shindano Ni Lake Bwana, Zawadi Ni Taji.

2. Sauti Ni Yake Mungu, Inayokuita;
Ndiyo Alitekirimu Taji Ya Uzima.

3. Mashahidi Ndio Wengi, Wanaokuoma;
Ya Nyuma Usifikiri, Bali Mwendo Kaza.

4. Bwana Umetuanzisha, Katika Shindano;
Kwa Vile Tunaposhinda, Ushindi Ni Wako.
(NK # 67) KESHA ROHO YANGU
My Soul, Be On Thy Guard

1. Kesha Roho Yangu, Adui Maelfu
Hujaribu Kuangusha, Kuvuta Dhambini.

2. Ukeshe,Uombe, Ili Usishindwe;
Fanya Vita Kila Siku, Omba Msaada.

3. Kushinda Ni Bado: Ulinde Silaha;
Usiache Kupigana Hata Una Taji.
(NK # 68) TUSIMAME IMARA MWAMBANI
Firmly Stand For God

1. Umtetee Mungu Duniani, Ijapo Pepo Kali Zavuma;
Mwanbani Pekee Pana Nguvu, Dhambi Ikilemea.

Tusimame Imara Katika Mwamba,
Mwamba Wa Kristo Pekee;
Ndipo Salameni Tutasimama
Kule Kitini Pa Enzi.

2. Itetee Haki Kwa Bidii, Kwa Moyo Mnyofu Wa Imani;
Mwambani Pekee Utashinda, Wingi Wa Upotevu.

3. Itetee Kweli Itadumu, Ijapokawia Itashinda;
Mwambani Pekee Pana Raha, Yaishapo Tufani.
(NK # 69) CHA KUTUMAINI SINA
My Hope Is Built

1. Cha Kutumaini Sima; Ila Damu Yake Bwana,
Sina Wema Wa Kutosha; Dhambi Zangu Kuziosha.

Kwake Yesu Nasimama,
Ndiye Mwamba: Ni Salama;
Ndiye Mwanba: Ni Salama;

2. Njia Yangu Iwe Ndefu; Yeye Hunipa Wokovu;
Mawinbini Yakinipoga; Nguvu Zake Ndio Nanga.

3. Damu Yake Na Sadaka; Nategemea Daima,
Yote Chini Yakiisha; Mwokozi Atanitosha.

4. Nikiitwa Hukumuni; Rohoni Nina Amani;
Nikivikwa Haki Yake; Sina Hofu Mbele Zake.

(NK # 70) WAPENZI WA BWANA
Come, We That Love The Lord

1. Wapenzi Wa Bwana; Ije Raha Yenu!
Imbeni Nyimbo Za Raha, Imbeni Nyimbo Za Raha:
Za Ibada Yenu; Za Ibada Yenu.

Twenenda Zayuni, Mji Mzuri Zayuni!
Twenenda Juu Zayuni, Ni Maskani Ya Mungu.

2. Wasiimbe Wao Wasioamini,
Watoto Mungu Ndio, Watoto Wa Mungu Ndio
Waimbao Chini, Waimbao Chini

3. Twaona Rohoni Baraka Za Mungu
Tusijafika Mbinguni, Tusijafika Mbinguni
Kwenye Utukufu, Kwenye Utukufu.

4. Tutakapomwona Masumbuko Basi.
Huwa Maji Ya Uzima; Huwa Maji Ya Uzima.
Anasa Halisi; Anasa Halisi.
(NK # 71) KESHENI KAOMBENI
Watch, For The Time Is Short

1. Kesha Ukaombe Panapo Mafasi;
Wakati Si Mwingi. Kwa Vile Ukeshe
Mwili Ni Dhaifu. Adui Hodari
Karibu Atakuja, Bwana Wa Arusi.

Kesha, Omba, Kesha, Omba,
Kesha Kaombe Gizani, Mchana,
Daima Kesha.

2. Fukuza Usingizi, Fukuza Mashaka;
Ahadi Ni Yako, Raha Ya Milele
Bwana Alikesha Kwa Ajili Yako;
Jasho Yeke Ikawa Matone Ya Dame.

3. Yesu Umkubali Awe Nguvu Zako;
Silaha Uzivae; Adui Karibu.
Sasa Nafasi Iko, Isipite Bure;
Bila Kukawia Masihiya Kesha.
(NK # 72) JENGA JUU YA MWAMBA
We’ll Build On The Rock

1. Tutajenga Juu Ya Mwanba,
Wa Yesu, Mwamba Wa Kale;
Tutavumilia Kishindo; Tufani Ivumapo.

Tutajenga Juu, (Tutajenga Juu Ya Mwamba Mkuu)
Tutajinga Juu, (Tutajenga Juu Ya Mwanba Mkuu)
Tuta Jenga Juu Ya Mwamba Mkuu, Juu Yake Yesu.

2. Wingine Hujenga Katika
Mchanga Wa Ulimwengu;
Wingine Katika Mawimbi
Ya Anasa Za Dhambi.

3. Jenga Nawe Juu Ya Mwanba,
Msingi Pekee Wa Kweli:
Tumaini Lake Litadumu,
Tumai La Wokovu.

(NK # 73) “BWANA, UNIONGOZE JUU”
I’m Pressing On

1. Nakaza Mwendo Mbinguni, Kila Siku Napanda Juu;
Naomba Nikisafiri, “Bwana Uniongoze Juu.

Bwana Uniinue Juu; Kwa Imani Hata Mbingu,
Juu Kuliko Dunia; Bwana Uniongoze Juu.

2. Moyo Wangu Hutaki; Kukaa Palipo Shaka;
Wengine Wapenda Chini; Nia Yangu Ni Ku Panda.

3. Nataka Kupanda Juu; Nisishindwe Na Adui;
Kwa Imani Nasikia; Sauti Ya Washindaji.

4. Kupanda Juu Nataka; Niuone Utukufu;
Hata Mwisho Nitaomba, “Bwana Uniongoze Juu.”

(NK # 74) NIAMBIE, EE MLINZI
Watchman, Tell Me

1. Niambie, Ee Mlinzi, Umepambazuka Je!
Utukufu Wa Zayuni; Pana Dalili Zake?
Msafiri Uondoke, Utazame Mbinguni,
Kiunoni Ujifunge, Ni Kucha, Alifajiri.

2. Mlinzi, Inamulika Nuru Njiani Mwako,
Dalili Ya Kuja Kwake, Kwamba Siku Karibu;
Panda Itakapolia Itawaamsha Wafu,
Watakatifu Wa Mungu, Kuwapa Kutokufa.

3. Mlinzi, Ione Nuru Ya Mwaka Wa Sabato;
Sauti Zina Tangaza Ufalme Ni Karibu:
Msafiri Ninaona Mlima Wa Zayuini,
Mji Wa Yerusalemu Nayo Fahari Yake.

4. Kwenye Mji Wa Dhahabu Anaketi Mfalme
Katika Kiti Kizuri: Huku Ana Tawala.
Pana Amani Po Pote, Mashamba Husitawi;
Na Ardhi Ina Rutuba; Mito Ni Mitulivu.

5. Mlinzi, Twakaribia Nchi Iliyo Nzuri;
Twende Mbele, Tufurahi, Nchi Inachangamka.
Sikieni Kuna Wimbo Wa Waliookoka;
Kaza Mwendo, Ujiunge Na Kundi Kubwa Hili.
(NK # 75) MSINGI IMARA, NINYI WA BWANA
How Firm A Foundation

1. Msingi Imara, Ninyi Wa Bwana,
Ume Wekwa Kwenu Kwa Neno Lake?
Nini Zaidi Atasema Bwana?
Imani Yenu Ipate Kuzidi?

2. Wanbiwapo Vuka Maji Ya Giza,
Mito Ya Mashaka Haitazidi;
‘Takuwapo Nawe, Nikuwezeshe,
Shida Upatazo Zisikutishe!

3. Utakapopishwa Ndani Ya Moto
Nguvu Nitakupa, Upate Pato;
Huteketezwi, Ila Taka Zako.
Na Zitasalia Dhahabu Zako.

4. Na Mtu Aliyenitegemea
Nguvu Za Jehanamu Zijapotisha,
Kamwe Kwa Adui Sitamtia;
Mtu Wangu Kamwe Sitamuacha.

(NK # 76) MRITHI UFALME
Heir Of The Kingdom

1. Mrithi Ufalme Kwani Walala? Karibu Wokovu Wasinzia?
Amka Simama Uvae Silaha; Haraka Sana Saa Zapita.

2. Mrithi Ufalme Mbona ‘Kawia’? Mbona Hupokei Zawadi?
Haya Uvae, Mwokozi Yuaja; Haraka, Umlaki Apitapo.

3. Mataifa Makuu Ya Dunia; Yapigana Na Kujiangusha.
Usiziofu Dalili, Mrithi; Ishara Zote Hazikawii.

4. ‘Sitazame Anasa Za Dunia! Kwani Hayo Ya Pita Upesi.
Zivunje Kamba Zinazokufunga; Mrithi Ufalme, Njoo’karudi.

5. Inua Kichwa, Tazama Mbele Tu; Mfalme Aja Na Utukufu;
Jua La Onekana Milimani, Warithi Ufalme Furahini.
(NK # 77) HABARI ZA USIKU
Watchman On The Walls Of Zion

1. Je! Mkinzi Ukutani; Wa Mji Wa Zayuni,
Habari Zake Usiku? Asubuhi Karibu?
Kuna Dalili Za Kupambazuka?
Kuna Dalili Za Kupambazuka?

2. Katika Safari Yetu; Twaona Nchi Kavu?
Tutalala Baharini? Bandari Bado Mbali?
Kweli, Kweli Tutaona Ufalme?
Kweli, Kweli Tutaona Ufalme?

3. Tunaona Nuru Yake; Nyota Ya Asubuhi;
Nyota, Tukufu Na Safi; Inang’aa Mbinguni;
Furahini, Wokovu U Karibu.
Furahini, Wokovu U Karibu.

4. Tumetazama Ramani, Kweli Pwani Si Mbali;
Twende Mbele, Kwa Upesi; Tutaona Bandari;
Furahini, Imbeni Nyimbo Zenu.
Furahini, Imbeni Nyimbo Zenu.

(NK # 78) MPAKA LINI BWANA
How Long, O Lord Our Saviour

1. Mpaka Lini Bwana; Utakaa Mbali?
Kemetuchosha Moyo; Kukawia Hivi.
Utatujia Lini, Ili Tu Furahi
Katika Ile Nuru, Kuja Kutukufu?

2. Mpaka Lini, Yesu, Utaacha Watu
Uliowakomboa; Wawe Na Mashaka?
Wachache Waamini; Kwamba Utarudi;
Wachache Wa Tayari; Bwana Kukulaki

3. Waamshe Watu Wako; Tangaza Kilio:
Mwe Watakatifu, Bwana Yu Karibu!”
Utatujia Lini, Ili Tu Furahi
Katika Ile Nuru, Kuja Kutukufu?

(NK # 79) NATAKA IMANI HII (O For A Faith)

1. Nataka Imani Hii: Imani Imara
Ambayo Haitetemi, Kitu Chote, Wakati Wa Shida,
Wakati Wa Shida.

2. Isiyonung’unika Huzuni, Taabu;
Lakini Katika Saa, Ya Matata, Humwamini Mungu,
Humwamini Mungu.

3. Imani Inayo Ng’aa Katika Tufani;
Isiyoogopa Giza, Wala Shida, Njaa Na Hatari,
Njaa Na Hatari.

4. Haiogopi Dunia, Kudharau Kwake;
Haiangushwi Na Hila, Na Uwongo, Dhambi Na Ogofyo,
Dhambi Na Ogofyo.

5. Bwana, Nipe Imani Hii, Hivi Nita Weza
Kuonja Hapa Chini, Ulimwenguni, Kurithi Furaha,
Kurithi Furaha.
(NK # 80) TUPE MOTO WA UHAI
O For That Flame Of Living Fire

1. Tupe Moto Wa Uhai;
Uliowaka Zamani,
Uliowaongoza Juu; Wazee Watakatifu.

2. Wapi Roho Iliyokaa;
Moyoni Mwa Ibrahimu?
Kadhalika Ndugu Paulo; Aliwezeshwa Na Moto.

3. Neema Yako Haina;
Nguvu Siku Hizi Sawa
Kama Wakati Wa Musa, Ayubu Na Wa Eliya?

4. Zamani Za Kale, Bwana,
Kumbuka Na Kwa Rehema,
Zihuishe Roho Zetu; Kwa Roho Mtakatifu.

(NK # 81) SIKU SITA ZIMEPITA
Another Six Days’ Work

1. Siku Sita Zime Pita,
Sabato Tena Karudi;
Shangilie Roho Yangu, Itukuze Kwa Busara.

2. Msifuni Awapaye
Pumziko Tamu Wachovu,
Kwake Roho Yatulizwa, Kupita Siku Nyingine.

3. Moyo Wetu Ufurahi,
Na Kutoa Mashukuru;
Ujalizwe Raha Ile, Yasipitikwa Kamwe.

4. Raha Hiyo Ya Rohoni,
Ni Amana Ya Pumziko;
Ambalo Limewekwa Juu, Kikomo Cha Masumbuko

(NK # 82) NI SIKU YA FURAHA
O Day Of Rest

1. Ni Siku Ya Furaha, Ni Siku Ya Nuru;
Nasi Twaona Raha, Kuja Kushukuru;
Leo Watu Wa Mungu, Wadogo, Wakubwa,
Hukaribia Mbingu, Lilipo Baraka.

2. Leo, Ndiyo Bandari, Nasi Twawasili,
Hiyo Bustani Nzuri, Ya Nyingi Fadhili:
Kijito Cha Baridi; Kimefanya Ziwa,
Na Kiu Ikizidi, Twanywa Maridhawa.

3. Leo Ngazi Na Iwe Ifakayo Juu,
Mawazo Na Yasiwe Ya Duniani Tu;
Leo Ni Kujilisha; Chakula Cha Mbingu,
Na Kujifurahisha Kwa Mambo Ya Mungu.
(NK # 83) EWE SKULI YA SABATO
Sweet Sabbath School

1. Ewe Skuli Ya Sabato,
U Pazuri Sana;
Moyo Wangu Wanivuta,
Nije Kwako Leo.
Sabato . . . Ni Nzuri . . .
Sabato . . . Ni Nzuri . . .
Moyo Wangu Wanivuta,
Nije Kwako Leo.

2. Moyo Wangu Mpotovu,
Hapa Una Raha;
Ndipo Nimwonapo Yesu,
Nije Kwako Leo.

3. Hapa Yesu Mwenye Pendo
Aniita Pole:
Nimtolee Moyo Yeye,
Nije Kwako Leo.

(NK # 84) IKUMBUKE SABATO
Don’t Forget The Sabbath

1. Ikumbuke Kote Sabato Ya Bwana,
Siku Tamu Na Bora, Kupita Nyingine;
Yatuletea Raha, Na Furaha Kweli,
Mwanga Wake Hungaza, Urembo Wa Yesu.

Karibie, Karibie, Sabato Tamu;
Karibie, Yesu Pia, Bwana Wa Raha.

2. Itakase Kweli, Ukamsifu Leo,
Yeye Aliye Sema “Mimi Ndiye Njia”;
Nasi Tukimfuata Mkombozi Hapa.
Atatunywesha Tele Maji Ya Uzima.

3. Siku Ya Nderemo! Tupishe Wakati,
Tukimwimbia Yesu, Rafiki Mpendwa;
Mponya Wetu Leo, U Mwema Ajabu!
Ukae Kwetu, Bwana, Moyoni Daima.

(NK # 85) SALAMA TUMEPITA Safely Through Another Week

1. Salama Tumepita, Safarini Juma Hii,
Tumwendee Mwokozi, Atubariki Sasa:
Siku Hiyo Ya Raha, Siku Bora Ya Juma;
Siku Hiyo Ya Raha, Siku Bora Ya Juma.

2. Utupe Nuru Leo Toka Hazina Yako;
Ondoa Dhambi Zetu, Tupokee Na Pendo;
Mikono Yapumzika, Tuishi Ndani Yako,
Mikono Yapumzika, Tuishi Ndani Yako.

3. Twakusanyika Hapa, Tusifu Jina Lako;
Ukaribie Kwetu, Tupe Neema Bwana;
Utamu Tusikize, Wa Raha Ya Milele:
Utamu Tusikize, Wa Raha Ya Milele:

4. Injili Yako Leo, Ishike Wenye Dhambi;
Itupe Nguvu Nyingi, Iponye Wenye Shida;
Mioyo Yetu Shangaza, Vyakula Utulishe,
Mioyo Yetu Shangaza, Vyakula Utulishe.
(NK # 86) UKARIBIE TENA
Welcome, Welcome, Day Of Rest

1. Ukaribie Tena,
Ewe Siku Ya Raha;
Roho Yakusalimu
Kama Mwanga Wa Mbingu.

2. Raha Yako Tulivu,
Yafurahisha Moyo;
Yatuliza Taabu,
Hata Waisha Mwendo.

3. Ee Siku Takatifu,
Sifa Na Maombi,
Na Kutuhekimisha.,
Baraka Yako Kubwa.

(NK # 87) SIKU YA SABATO
Thy Holy Sabbath Lord

1. Siku Ya Sabato, Siku Takatifu,
Watu Wako Mungu Wetu, Waipenda Sana.

2. Ulitakasa, Uliibariki,
Siku Hiyo Ya Sabato, Siku Yako Bwana.

3. Nasi Tubariki Tukikuabudu,
Katika Siku Ya Raha, Siku Yako Bwana.

4. Halafu Mbinguni, Pamoja Na Wewe.
Tunataka Kuzishika Sabato Za Bwana.
(NK # 88) SIKU HII YA SABATO
How Sweet Upon This Sacred Day

1. Siku Hii Ya Sabato, Tamu Kufikiri
Juu Ya Mungu Na Mbingu, Kuacha Dunia.

2. Tamu Kusikia Neno Toka Mhubiri
Anayefundisha Toba, Tupate Uzima.

3. Katika Vita Na Dhambi, Ikiwa Twashindwa,
Yeye Atatupa Nguvu, Aonaye Moyo.
(NK # 89) ASUBUHI
Lord, In The Morning

1. Bwana Asubuhi Kucha, Nitakuinua
Sauti Yangu Kuomba, Nipate Baraka.

2. Nakuomba Roho Yako, Niongozwe Nayo;
Nifanye Yanipasayo, Na Mapenzi Yako.

3. Wanaokutegemea, U Mlinzi Wao;
Matumaini Wanayo, Utayatimiza.

4. Na Kwa Wingi Wa Fadhili, Nyumbani Mwako Juu
Nitaingia Na Wimbo, Pale Kusujudu.
(NK # 90) MAPYA NI MAPENZI
New Every Morning

1. Mapya Ni Mapenzi Hayo, Asubuhi Tuonayo;
Saa Za Giza Hulindwa, Kwa Uzima Kuamka.

2. Kila Saku, Mapya Pia, Rehema, Wema Na Afya,
Wokovu Na Msamaha, Mawazo Mema, Furaha.

3. Tukijitahidi Leo, Na Mwendo Utupasao,
Mungu Atatueleza, Yatakayompendeza.

4. Mamboyetu Ya Dunia, Bwana Atayang’aria,
Matata Atageuza, Yawe Kwetu Ya Baraka.

5. Yaliyo Madogo, Haya Bwana Tukimfanyia,
Yatosha: Tutafaidi, Huvuta Kwake Zaidi.

6. Ewe Bwana, Siku Zote, Tusaidie Kwa Yote:
Mwendo Wetu Wote Vivyo, Uwe Kama Tuombavyo.

(NK # 91) KAA NAMI
(Abide With Me)

1. Kaa Nami, Ni Isiku Tena; Usiniache Gizani, Bwana.
Msaada Wako Haukomi; Nili Peke Yangu, Kaa Nami.

2. Siku Zetu Hazakawi Kwisha; Sioni La Kunifurahisha;
Hakuna Ambacho Kakikomi, Usiye Na Mwisho Kaa Nami.

3. Nina Haja Nawe Kila Saa; Sina Mwingine Wa Kunifaa
Mimi Nitaongozwa Na Nani? Ila Wewe Bwana, Kaa Nami.

4. Sichi Neno Uwapo Karibu; Nipatalo Lote Si Taabu;
Kifo Na Kaburi Haviumi; Nitashinda Kwako, Kaa Nami.

5. Nilalapo Nikuone Wewe, Gizani Mote Nimulikiwe;
Nuru Za Mbinguni Hazikomi, Siku Zangu Zote; Kaa Nami.

(NK # 92) MAGHARIBI JUA
Day Is Dyding In The West

1. Magharibi Jua Limekwisha Kushuka,
Mwezi Na Nyota Sasa Vinamsifu Muumba Wa Usiku.

Mungu Mtukufu, Mungu Mkuu,
Wote Juu Mbinguni, Na Wanadamu Chini Twakusifu.

2. Mpaji Wa Uhai, Ukaaye Mbinguni.
Utuhifadhi Sisi, Tufahamu Gizani, U Karibu.

3. Mapenzi Yako Makuu Yawe Nasi Usiku,
Tuli Usingizini, Kucha Vivyo Roho Tushukuru.

4. Na Utakapo Kuja Na Nguvu Kutawala,
Mungu Wangu Kubali Kunichikua Mimi Uliko Juu.

Baba, Mwana, Roho, Mungu Wetu,
Wote Juu Mbinguni, Na Wanadamu Chini Twakusifu.

(NK # 93) JUA LA ROHONI MWANGU
Sun Of My Soul

1. Jua La Rohoni Mwangu, Mpendwa Mwokozi Wangu;
Usiku Giza Hapana, Ukiwa Karibu Bwana.

2. Nikipata Usingizi, Nijaze Fikara Hizi,
Ni Tamu Sana, Nilale, Pendoni Mwako Milele.

3. Kaa Nami, Ewe Bwana, Usiku Kama Mchana,
Nisiishi Mbali Nawe; Ni Uhai Kuwa Nawe.

4. Kama Mtoto Mnyonge Ameshawisha Atange,
Mtafute Ewe Bwana, Ujirudi-shie Tena.

5. Wagonjwa Wape Amani, Waneemeshe Maskini,
Walio, Mtulizi, Wape Wote Usingizi.

6. Asubuhi Tutokapo, Tukaribishe Tulipo;
Twingiapo Duniani, Tuwe Mwako Mkononi.

(NK # 94) PO POTE MASHAMBA YAJAA
Far And Near The Fields

1. Po Pote Mashamba Yajaa, Tele Nafaka Pevu,
Po Pote Yang’aa Meupe, Bondeni Na Nyandani.

Mwenye Mavuno, Twasihi Upeleke Wavuni,
Wayakusanye Mazao, Hata Kazi Yaishe.

2. Wapeleke Uchaoni, Waende Na Jotoni,
Hata Jua Lishukapo, Wakusanye Ko Kote.

3. Enyi Wakazi Wa Bwana, Yaleteni Mazao,
Na Jioni Ingieni, Kwake Na Furaha Kuu.
(NK # 95) ZILETENI ZAKA KWA HAZINA
Bring Ye All The Tithes

1. Sikieni Neno La Mungu Wetu, Zileteni Zaka Kwa Hazina
Leteni Na Mioyo Yenu Yote; Mibaraka Itakuja.

Zileteni Zaka Kwa Hazina,
Kanijaribu, Sasa Nazo;
Nitakupeni Mibaraka,
Zaidi Ya Nafsi, Ya Kupewa.

2. Wataka Roho Mtakatifu Kwako? Uzilete Zaka Kwa Hazina
Ukae Karibu Na Bwana Wako, Ndipo Utakapo Barikiwa.

3. Je! Unakasoro Na Bwana Wako? Uzilete Zaka Kwa Hazina
Uzilete Kama Alivyosema, Ndipo Utakapo Barikiwa.

4. Ushukuru Bwana Na Moyo Wote, Unapoleta Zaka Ghalani;
Usadiki Ahadi Zake Zote, Ndipo Utakapo Barikiwa.

5. Tuimbe Sote Nyimbo Za Furaha, Tunapoleta Zaka Ghalani
Twimbe Kabisa Na Furaha Kubwa, Kwani Tutabarikiwa.

(NK # 96) MALI YAKO SASA
We Give Thee But Thine Own

1. Mali Yako Sasa, Bwana, Tutatoa;
Hatuna Yaliyo Yetu, Yote Ni Vipaji.

2. Sisi Watumishi, Twaungama Deni;
Tunge Irudisha Kwake, Iliyo Ya Bwana.

3. Utusaidie, Upendo Kujua,
Kwa Ajili Yao Wote Walio Gizani.

4. Neno Tumaini Na Kutegemea:
Kwamba Lote Tufanyalo, Tulifanye Kwako.
(NK # 97) SIOSHWI DHAMBI ZANGU
What Can Wash Away My Sin?

1. Sioshwi Dhambi Zangu, Bila Damu Yake Yesu,
Hapendezewi Mungu, Bila Damu Yake Yesu.

Hakuna Kabisa, Dawa Ya Makosa
Ya Kututukasa, Ila Damu Yake Yesu.

2. La Kunisafi Sina, Ila Damu Yake Yesu,
Wala Udhuru Tena, Ila Damu Yake Yesu.

3. Sipati Patanishwa, Bila Damu Yake Yesu,
Hukumu Yanitisha, Bila Damu Yake Yesu.

4. Sipati Tumaini, Bila Damu Yake Yesu,
Wema Wala Amani, Bila Damu Yake Yesu.

5. Yashinda Ulimwengu, Iyo Damu Yake Yesu,
Na Kutufikisha Juu, Iyo, Damu Yake Yesu.

(NK # 98) NILIKUPA WEWE
I Gave My Life For Thee

1. Nilikupa Wewe, Damu Ya Moyoni,
Ili Wokolewe, Winuke Ufuni.

Nimekunyima Ni Wewe? Umenipa Nini?
Nimekunyima Ni Wewe? Umenipa Nini?

2. Nilikupa Myaka Yangu Duniani;
Upate Inuka, Kuishi Mbinguni.

3. Nimekuletea, Huku Duniani;
Pendo Na Wokovu, Zatoka Mbinguni.

4. Nipe Siku Zako, Udumu Mwangani;
Na Taabu Yako, Wingie Rahani.

Nafsi, Nafsi, Pendo, Mali, Twae Imanueli.
Nafsi, Nafsi, Pendo, Mali, Twae Imanueli.

(NK # 99) TWENDE KWA YESU
Come To The Saviour, Make No Delay

1. Twende Kwa Yesu Mimi Nawe,
Njia Atuonya Tuijue,
Imo Chuoni; Na Mwenyewe,
Hapa Asema Njoo!

Na Furaha Tutaiona, Myoyo Iki Takasa Sana;
Kwako Mwokozi, Kuonana, Na Milele Kukaa.

2. “Wana Na Waje,” Atwambia
Furahini Kwa Kusikia;
Ndiye Mwokozi Wetu Hasa,
Na Tumtii, Njoni.

3. Wangojeani? Leo Yupo:
Sakiza Sana Asemapo;
Huruma Zake Zitwitapo,
Ewe Kijana, Njoo.

(NK # 100) KUWATAFUTA
Seeking The Lost

1. Kuwatafuta Wasioweza, Kuomba Wamrejee Yesu,
Kuwaambia Maneno Yake Njooni Kwangu, Nawapenda

Nitakwenda (Nitakwenda- kwenda) Niwatafute
Wapotevu (Wapotevu waje) Wageuke,
Waingie (Waingie wote) Katika Zizi
La Mwokozi (La Mwokozi wetu) Yesu Kristo.

2. Kuwatafuta Wasioweza, Waonyeshwe Mwokozi Wetu,
Kuwaongoza, Wapate Wote Uzima Ule Milele.

3. Kazi Hiyo Nataka Kufanya, Leo Nimesikia Mwito
Kuwainua Waangukao, Waletwe Kwake Yesu Njia.
(NK # 101) YESU AKWITA
Jesus Is Tenderly Calling Today

1. Yesu Akwita, Akwita Wewe, Uje Leo, Uje Leo,
Kwani Kusita, Akwita Wewe Unatanga Upeo;

Msikie, Msikie,
Yesu Akwita, Ujitoe Moyo Sasa.

2. Wliochoka, Na Wapumzike, Uje Leo, Uje Leo,
Wenye Mizigo, Wenye Huzuni Wapate Mapumziko.

3. Anakungoja Uliye Yote, Uje Leo, Uje Leo,
Uliyekosa, Usijifiche: Woshwe, Uvikwe Nguo.

4. Yesu Asihi Wakawiao, Waje Leo, Waje Leo,
Watafurahi Waaminio; Amka, Upesi, Njoo.

(NK # 102) MLANGONI PA MOYO (There’s A Stranger As The Door)

1. Mlangoni Pa Moyo; Mgeni! (Amesimama) x2
Amesimama Pale, Mgeni! (Amesimama) x2
Umkaribishe Sasa, Umkaribishe Mwana
Wa Baba Wa Upendo: Mgeni! (Umkaribishe) x2

2. Moyo Wako Kwa Bwana, Fungua. (Fungulieni) x2
Asikuache Mbali, Fungua. (Fungulieni) x2
Umkubali Rafiki, Roho Atafariji
Naye Atakutunza: Fungua. (Fungukieni) x2

3. Usikie Sauti Ya Bwana (Uisikie) x2
Uyachague Mambo Ya Bwana (Mambo Ya Bwana) x2
Ufungue Mlango, Usimwambie Bado:
Jina Lake Tumai—- Yu Bwana. (Jina La Bwana) x2

4. Na Ufungue Moyo, Kwa Bwana (Fungulieni) x2
Utapewa Msaada, Wa Bwana (Msaada Wetu) x2
Uzuri Utavikwa; Dhambi Ataondoa,
Ukifungua Moyo. Kwa Bwana (Fungulieni) x2
(NK # 103) NJONI KWANGU
Softly And Tenderly

1. Yesu Huita Kwa Upole Mwingi, Atwita Wewe Nami;
Moyoni Mwetu Hungoja, Hukesha, Hukungojea Wewe.

Njoni Kwangu,
Mliochoka, Njoni:
Yesu Huita Kwa Upole Mwingi,
Akwita, “Uje Kwangu”

2. Atuombeapo Usikawie, Hutuombea Sisi;
Usidharau Wema Ma Huruma, Huruma Kwetu Sisi.

3. Siku Za Maisha Hupota Hima, Hupita Kwako, Kwangu;
Usiku Waja, Kifo Kinakuja, Huja Kwako Na Kwangu.

4. Fikiri Juu Ya Upendo Wake, Upendo Kwako, Kwangu;
Dhambi Zetu Amekwisha Samehe. Masamaha Ni Yetu.
(NK # 104) YESU ALINIITA “NJOO”
I Heard The Voice Of Jesus Say

1. Yesu Aliniita, “Njoo Raha Iko Kwangu,
Kichwha Chako Ukilaze Kifuani Mwangu”
Nilikwenda Kwake Mara, Sana Nilichoka;
Nikapata Kwake Raha Na Furaha Tena.

2. Yesu Aliniita, “Njoo, Kwangu Kuna Maji;
Maji Ya Uzima, Bure, Unywe Uwe Hai.”
Nilikwenda Kwake Mara Na Maji Nikanywa;
Naishi Kwake Na Kiu Kamwe Sina Tena.

3. Yesu Aliniita, “Njoo, Dunia I Giza,
Ukinitazama, Nuru Takung’arizia.’
Nili Kwenda Kwake Mara, Yeye Jua Langu,
Ni Kila Wakati Mwanga Safarini Mwangu.
(NK # 105) MCHUNGAJI MPENZI Lovingly, Tenderly Calling

1. Mchungaji Mpenzi Hukuita Uje
Katika Zizi Lake Panapo Salama;
Akina Wanawake, Waume Vijana,
Yesu Aliye Kweli, Huwaita Kwake

Huita Kwa Moyo Wa Huruma,
Uluyepotea Uje Kwangu’;
Hivi Kukungoja Anadumu
Bwana Yesu Mchunga.

2. Akatoa Maisha Kwa Ajili Yetu;
Ataka Wapotevu Waje Kwake Sasa;
Tusijihatirishe; Kwake Tu Salama;
Sikia Wito Wake, Mchungaji Wetu.

3. Tusikawie Tena, Adui Shetani,
Kama Mbwa Wa Mwitu, Atatuharibu;
Tunaitwa Na Yesu, Mkombozi Wetu,
Tuingie Zizini, Panapo Nafasi.
(NK # 106) HUNA KITU KWA YESU? Nothing For Jesus

1. Ukitafuta Mali, Huna Wasaa Kwa Yesu?
Kwa Matendo Ya Haki Huna Wasaa Kwa Yesu?
Ansa Za Kunia, Mambo Yako Ya Raha
Haya Unatafuta; Huna Wasaa Kwa Yesu?

2. Mambo Yanakusonga: Kwake Huna Nafasi?
Watekwa Na Dunia, Kwake Huna Nafasi?
Humwani M-Langoni, Anapopiga Hodi?
Daima Hukusihi: Kwake Huna Nafasi?

3. Sa-A Ni Za Thamani, Kwake Huna Nafasi?
Wala Hamfnyi Bidii, Kwake Hamnayo Kazi?
Hamkufika Kwao Waliomo Shimoni
Na Waliopotea? Kwake Hamnayo Kazi?

4. Na Wazaa Majani Tu? Huna Tunda Kwa Yesu?
Mikono I Mitupu, Huna Tunda Kwa Yesu?
Huna Chembe Kwa Ghala Kazi Yako Kulipa;
Wala Huna Furaha Unapomwona Yesu?
(NK # 107) NIPO BWANA, NITUME
Hark! The Voice Of Jesus
1. Sauti Ni Yake Bwana, “Kwenda, Nani Tayari”
Mavuno Yanakawia, Nani Atayavuna?
Kwa Kudumu Amaita, Zawadi Atatoa;
Nani Atakayejibu “Nipo Bwana, Nitume.”

2. Kana Huwezi Safari; Hata Nchi Za Mbali,
Pana Watu Karibuni;Wasio Mjua Yesu;
Kama Huwezi Kusema; Jinsi Ya Malaika,
Waweza Kuutangaza; Upendo Wa Mwokozi.

3. Ingawa Huwezi Kuwa; Mkesha Mlangoni,
Ukiwatolea Watu; Nafasi Ya Uzima;
Kwa Sala Na Kwa Sadaka; Watoa Msaada,
Kama Haruni Mwaminifu, Kuinua Mikono.

4. Roho Za Watu Zikifa, Bwana Akikuita,
Usiseme Kwa Uvivu, “Hakuna Kazi Kwangu.”
Kwa Furaha Anza Kazi; Ile Akiyokupa,
Ukajibu Mara Moja; “Nipo Bwana, Nitume.”
(NK # 108) TUMESIKIA MBIU We Have Heard A Joyful Sound

1. Tumesikia Mbiu: Yesu Huokoa;
Utangazeni Kote, Yesu Huokoa.
Tiini Amri Hiyo: Nchimi Baharini,
Enezeni Mbiu Hii: Yesu Huokoa.

2. Imba Nawe Askari: Yesu Huokoa;
Kwa Nguvu Ya Kombozi, Yesu Huokoa;
Imbeni Wenye Shida, Unapounwa Moyo,
Na Kaburini Imba: Yesu Huokoa.

3. Mawimbini Uenee. Yesu Huokoa.
Wenye Dhambi Jueni: Yesu Huokoa;
Visiwa Na Viimbe, Vilindi Itikeni,
Na Nchi Shangilie: Yesu Huokoa.

4. Upepo Utangaze: Yesu Huokoa.
Mataifa Ya Shangaa: Yesu Huokoa;
Milimani, Bondeni, Sauti Isikike
Ya Winbo Wa Washindi: Yesu Huokoa.
(NK # 109) ANISIKIAYE
Whoever Heareth

1. Anisikiaye, Aliye Yote, Sana Litangae, Wajue Wote,
Duniani Kote Neno Wapate, Atakye Na Aje!

Ni “Atakaye,” Ni “Atakaye”;
Pwani Hata Bara, Na Litangae:
Ni Baba Mpenzi Alinganaye Atakaye Na Aje.

2. Anijiliaye, Yesu Asema, Asikawe, Aje Hima Mapema
Ndimi Njia, Kweli, Ndimi Uzima: Atakaye Na Aje!

3. Atakaye Aje, Ndiyo Ahadi; Atakaye Hiyo Haitarudi!
Atakaye Lake, Ni La Ahadi! Atakaye Na Aje.

(NK # 110) MLANGO WAZI
There Is A Gate

1. Mlango Uko Wa Wema, Mlango Wazi Huo:
Yesu Aneufungua Na Hakuna Kufunga.

Mlango Wazi, Ajabu,
Uliachwa Wazi Kwangu?
Kwangu, Kwangu?
Wazi, Wazi Kwangu?

2. Mlango Hukaa Wazi Watu Waokolewe:
Maskini Ma Matajiri Wa Mataifa Yote.

3. Maadanu Mlango Wazi, Rafiki Kaza Mwendo;
Msalaba Ukubali- Amana Ya Upendo.

4. Msalaba Tutabeba Daima, Na Furaha!
Pendo La Yesu Hushinda. Unainama Kwake!

(NK # 111) TABIBU MKUU
The Great Physician

1. Tabibu Mku-U Huyu, Yesu Mwenye Huruma:
Atuletaye Faraja : Yesu Mwokozi Wetu.

Imbeni, Malaika Sifa Za Bwana Wetu;
Jina La Pekee Kwetu, Ni La Yesu Bwana.

2. Mwana Kondo-O Msifuni Mwokozi:
Hatia Zote Na Dhambi Huziondoa Yesu.

3. Hakuna Jina Jingine Linalofa-A Sifa:
A-U Kutufurahisha, Isipo Kuwa Lake.

4. Naye Atakapokuja Na Utukufu Wake,
Tutafurahi Milele Kuka-A Kwake Bwana.
(NK # 112) WEWE UMECHOKA SANA?

1. Wewe Umechoka Sana? Wataka Raha?
Kwake Yesu Utapata –Msaada.

2. Alama Anazo Yeye? Sana! Makovu
Ya Mikono, Na Miguu, Na Mbavu.

3. Naye Amevikwa Taji Kichwani Mwake?
Taji, Kweli, Alivikwa –Miiba!

4. Huku Nikimfuata, Nipate Nini?
Maonjo Nje, Na Ndani—Amani.

5. Kwamba Namwandama Yeye, Mwisho Ni Nini?
Kurithi Futaha Naye—Milele.
(NK # 113) BUBUJIKO
There Is A Fountain

1. Damu Imebubujika, Ni Ya Imanweli,
Wakioga Wenye Taka, Husafiwa Kweli.

2. Ilimpa Kushukuru Mwivi Mautini;
Nami Nisiye Udhuru, Yanisafi Ndani.

3. Kondo-O Wa Kuuawa, Damu Ina Nguvu,
Wako Wote Kuokoa Kwa Utimilivu.

4. Bwana, Tangu Damu Yako Kunisafi Kale,
Nimeimba Sifa Zako. ’Taimba Milele.

5. Bwana, Umenikirimu Nisiyestahili
Kwa Damu Yako, Sehemu Ya Mali Ya Kweli.

6. Nikubali Kumwimbia Mbinguni Milele.
Mungu Nitamsifia Jina Lako Pweke.

(NK # 114) YESU NATAKA KUTAKASWA SANA
Lord Jesus, I Long To Be Perfectly Whole

1. Yesu Mwokozi Ili Nitakaswe,
Nataka Mouo Uwe Enzi Yako.
Ukiagnushe Kilichoinuka
Unioshe Sasa Niwe Mweupe.

Mweupe Tu, Ndiyo Mweupe,
Ukiniosha Nitakuwa Safi.

2. Bwana Yesu Sasa Unitazame,
Unifanye Niwe Dhabihu Hai.”
Najitoa Kwako, Na Moyo, Vyote;
Unioshe Sana Niwe Mweupe.

3. Bwana Kwa Hiyo Nakuomba Sana,
Nakuongojea Miguuni Pako,
Wanaokuja Hutupi Kamwe,
Unioshe Sasa Niwe Mweupe.

(NK # 115) NAENDEA MSALABA
I Am Coming To The Cross

1. Naendea Msalaba, Ni Mnyonge, Mpofu,
Yapitayo Naacha Nipe Msalaba Tu.

Nakutumaini Tu, Wee Mwana Wa Mungu;
Nainamia Kwako; Niponye Sasa, Bwana.

1. Nakulilia Sana: Nalemewa Na Dhambi;
Pole Yesu Asema: “Nitazifuta Zote.”

3. Natoa Vyote Kwako, Nafasi Nazo Nguvu,
Roho Yangu Na Mwili Viwe Vyako Milele.

4. Kwa Damu Yake Sasa Amenivuta Sana,
Upendo Hubidisha, Nimtafute Mwokozi.
(NK # 116) MOYO SAFI
One Thing I Of The Lord Desire

1. Bwana Ninataka Hili, Kwa Kuwa Nimechafuka,
Kwa Moto Au Kwa Maji Unisafishe Kabisa.

Unisafishe Mwokozi Ndani, Na Nje, Kwa Moto
Utakavyo: Ili Dhambi Ife Kwangu, Ife Kwangu.

2. Kupewa Hekima Yote, Itakuwa Tunu Kubwa;
Lakini Moyo Safi Ni, Bora Kwangu, Bora Kwangu!

3. Mpaka Moyo Ni Safi Siwezi Kuyafahamu
Mambo Mazuri Ya Mbingu, Mambo Mazuri Ya Mbingu.
(NK # 117) WAMWENDEA YESU
Have You Been To Jesus?

1.Wamwendea Yesu Kwa Kusafiwa. Kuoshwa Kwa Damu Ya Kondoo?
Je, Neema Yake Yatumwagiwa? Waoshwa Kwa Damu Ya Kondoo?

Kuoshwa, Kwa Damu Itutakasayo Ya Kondoo?
Ziwe Safi Nguo Nyeupe Sana;
Waoshwa Kwa Damu Ya Kondoo.

2.Wamwandana Daima Mkombozi.Waoshwa Kwa Damu Ya Kondoo?
Yako Kwa Msulubiwa Mavazi? Waoshwa Kwa. Damu Ya Kondoo?

3.Atakapokuja Bwana-Arusi Uwe Safi Katika Damu!
Yafae Kwenda Mbinguni Mavazi: Yaoshwa Kwa Damu Ya Kondoo?

4.Yatupwe Yalipo Na Takataka; Uoshawe Kwa Damu Ya Kondoo:
Huoni Kijito Chatiririka Uoshwe Kwa Damu Ya Kondoo?
(NK # 118) NILIPOTOKA KABISA
I’ve Wandered Far Away

1. Nilipotoka Kabisa, Sasa Narudi
Nikakawia Dhambini, Bwana Narudi.

Narudi Nyumbani: Daima Kwako.
Kwa Upendo Nipokee: Naja Nyumbani.

2. Nikasusurika Sana, Sasa Narudi
Mwenye Uchungu Natubu, Bwana Narudi.

3. Nimechoka Maovuni, Sasa Narudi;
Pendo Lako Lanivuta, Bwana Narudi.

4. Ndilo Tumaini Langu, Sasa Narudi;
Yesu Alinifilia, Bwana Narudi.

5. Damu Yake Yanitosha, Sasa Narudi;
Unioshe Kenyekenye, Bwana Narudi.

(NK # 119) ALILIPA BEI
I Hear The Saviour Say

1. Yesu Anasema, “Wewe Huna Nguvu
Kesha Ukaombe, Na Uje, Mwanangu.

Alilipa Bei, Nawiwa Naye;
Dhambi Ilitia Waa, Aliiondoa.

2. Bwana, Nimeona Uwezo Wako Tu
Waweza ‘Takasa Mioyo Michafu.

3. Sina Kitu Chema Kudai Neema,
Hivi Nitafua Mavazi Kwa Damu.

4. Ninaposimama Juu Ya Mawingu,
Taji Nitaweka Miguuni Pa Yesu.

(NK # 120) MSALABA WA YESU
Jesus, Keep Me Near The Cross

1. Msalaba Wa Yesu, Nikae Karibu;
Pale Pana Chemchemi Ya Kuponya Dhambi.

Pale Msalaba; Msalaba Wake,
Huo Ni Sifa Yangu; Kwa Maisha Yote.

2. Karibu Msalaba Nalitetemeka,
Pendo Likaniona Likanirenemu.

3. Unikumbushe Yesu, Nikuone Pale;
Niupate Upendo Na Kuvutwa Nao.

4. Karibu Msalaba, Kwa Kutegimea,
Kukesha Na Kungoja, Nitakaa Pale.

(NK # 121) KATIKA WENYE DHAMBI
Chief Of Sinners

1. Katika Wenye Dhambi, Ndimi Mkuu Wao
Ila Yesu Akaja, Kwa Dhanbi Alikufa,
Akamimina Damu Niupate Uzima.

2. Ajabu Pendo Lake! Pendo Lililo Kuu,
Pendo Lisilo Mwisho, Lidumulo Milele
Lililonitafuta, Ingawa Sikumpenda.

3. Ingawa Ni Mbaya, Kristo Ni Vyote Kwangu;
Ajua Haja Zangu; Huzuni Zangu, Zake;
Hata Katika Vita, Akiwapo Salama.

(NK # 122) YOTE NAMTOLEA YESU
All To Jesus I Surrender

1. Yote Namtolea Yesu, Moyo Wangu Ni Wake:
Ninavutwa Na Upendo, Kwa Hivyo, Najitoa.

Yote Kwa Yesu, Yote Kwa Yesu,
Upendo Wako Hushinda; Yesu, Natoa.

2. Yote Namtolea Yesu, Nainamia Pake;
Nimeacha Na Anasa, Kwako Yesu Nipokee.

3. Yote Namtolea Yesu, Nifanye Niwe Wako;
Nipe Roho Yako, Bwana, Anilinde Daima.

4. Yote Namtolea Yesu, Nami Naona Sasa,
Furaha Ya Ukombozi, Nasifu Jina Lake.
(NK # 123) YESU KWA IMANI
My Faith Looks Up To Thee

1. Yesu Kwa Imani, Nakutumaini, Peke Yako;
Nisikie Sasa, Na Kunitakasa,
Ni Wako Kabisa; Tangu Leo.

2. Nipe Nguvu Pia, Za Kusaidia, Moyo Wangu;
Ulikufa Wewe, Wokovu Nipewe,
Nakupenda Wewe, Bwana Wangu.

3. Hapa Nazunguka, Katika Mashaka, Na Matata;
Palipo Na Giza, Utaniongoza,
Hivi Nitaweza, Kufuata.

(NK # 124) UMECHOKA JE UMESUMBUKA
Are You Weary?

1. Umechoka, Je, Umesumbuka?
Mwambie Yesu Sumbuko Lako;
Unayalilia Yapitayo? Mwambie Yesu Pekee.

Mwambie Yesu Sumbuko Lako, Yu Rafiki Amini,
Hakuna Rafiki Kama Yeye, Mwambie Yesu Pekee.

2. Je, Machozi Yakulengalenga?
Mwambie Yesu Sumbuko Lako;
Walemewa Na Dhambi Rohoni? Mwambie Yesu Pekee.

3. Waogopa Shida Na Majonzi?
Mwambie Yesu Sumbuko Lako;
Wasumbukia Mambo Yajayo? Mwambie Yesu Pekee.

4. Kuanzia Kifo Kukutisha?
Mwambie Yesu Sumbuko Lako;
Watamania Ufalme Wake? Mwambie Yesu Pekee.
(NK # 125) UNIANGALIE
There’s Life In A Look

1. ‘Uniangalie’ Atwambia Yesu Aliyetufia;
Msalabani Ni Uzima, Hapa Utaipata Hazina.

Kutazama Kalwari, Kutazama Kalwari,
Ni Kupewa Kuishi Kuutazama Mti.

2. Ninapojaribiwa Ghafla, Shetani Hatanitenga;
Nikitazama Msalaba Nguzu Nitaipata Kwa Bwana.

3. Msalaba Nitautazama Kila Wakati, Daima.
Ahadi Nitategemea, Hovi Kabisa Sitaangukaa.
(NK # 126) NINA HAJA NAWE
I Need Thee Every Hour

1. Nina Haja Nawe Kila Saa;
Hawezi Mwingine Kunifaa.

Yesu Nakuhitaji Vivyo Kila Saa!
Niwezeshe Mwokozi, Nkujia.

2. Nina Haja Nawe; Kaa Nami,
Na Maonjo Haya, Hayaumi.

3. Nina Haja Nawe; Kila Hali,
Maisha Ni Bure, Uli Mbali.

4. Nina Haja Nawe, Nifundishe,
Na Ahadi Zako Zifikishe.

5. Nina Haja Nawe; Mweza Yote,
Ni Wako Kabisa Siku Zote.

(NK # 127) NISALAMA ROHONI MWANGU
When Peace Like A River

1. Nionapo Amni Kama Shwari, Au Nionapo Shida;
Kwa Hali Zote Umenijulisha
Ni Salama Rohoni Mwangu.
Salama Rohoni,
Ni Salama Rohoni Mwangu.

2. Ingawa Shetani Atanitesa, Nitajipa Moyo Kwani,
Kristo Ameona Unyonge Mwangu;
Amekufa Kwa Roho Yangu.

3. Dhambi Zangu Zote, Wala Si Nusu,
Huwekwa Msalabani;
Wala Sichukui Laana Yake,
Ni Salama Rohoni Mwangu.

4. Ee Bwana Himiza Siku Ya Kuja, Panda Itakapolia:
Utakaposhuka Sitaogopa
Ni Salama Rohoni Mwangu.
(NK # 128) TAAMINI NITII PIA
When We Walk With The Lord

1. Namwandama Bwana Kwa Alilonena, Njia Zangu Huning’azia;
Na Nikimridhisha Atanirudisha, Taamini Nitii Pia.

Kuamini, Njia Pweke Ni Hii
Ya Furaha Kwa Yesu: Amini Ukatii.

2. Giza Sina Kwangu, Wala Hata Wingu, Yeye Mara Huviondoa;
Oga, Wasiwasi, Sononeko, Basi; Huamini Nitii Pia.

3. Masumbuko Yote, Sikitiko Lote; Kwa Mapenzi Hunilipia;
Baa, Dhara, Dhiki, Vivyo Hubariki; Taanimi Nitii Pia.

4. Mimi Sitajua Raha Sawasawa; Ila Yote Yesu Kutoa:
Napata Fadhili Na Radhi Kamili, Taamani Nitii Pia.

5. Nitamfurahia Na Kumtumaini, Majumbani Na Njia-Njia;
Agizo Natenda; Nikitumwa Hwenda, Huamini, Nitii Pia.

(NK # 129) KUMTEGEMEA MWOKOZI
‘Tis So Sweet To Trust

1. Kumtegemea Mwokozi, Kwangu Tamu Kabisa;
Kukubali Neno Lake Nina Raha Moyoni.

Yesu, Yesu Namwamini, Nimemwona Thabiti;
Yesu, Yesu Yu Thamani, Ahadi Zake Kweli.

2. Kumtegemea Mwokozi, Kwangu Tamu Kabisa
Kuamini Damu Yake Nimeoshwa Kamili.

3. Kumtegemea Mwokozi, Kwangu Tamu Kabisa;
Kwake Daima Napata, Uzima Na Amani.

4. Nafurahi Kwa Sababu Nimekutegema;
Yesu, M-Pendwa, Rafiki, Uwe Nami Dawamu.

(NK # 130) YESU KWETU NI RAFIKI
What A Friend We Have In Jesus

1. Yesu Kwetu Ni Rafiki, Hwambiwa Haja Pia;
Tukiombawka Babaye, Maombi Asikia;
Lakini Twajikosesha, Twajitweka Vibaya;
Kama Tulimwomba Mungu, Dua Atasikia.

2. Una Dhiki Na Maonjo? Unamashaka Pia?
Haifai Kufa Moyo, Dua Atasikia.
Hakuna Mwingine Mwema, Wa Kutuhurumia:
Atujua Tu Dhaifu: Maombi Asikia.

3. Je, Hunayo Hata Nguvu, Huwezi Kwendelea,
Ujapodharauliwa. Ujaporushwa Pia.
Watu Wange Kudharau, Wapendao Dunia.
Hukwambata Mikononi, Dua Atasikia.

(NK # 131) BABA ANILINDA
I Trust In God

1. Namtegemea Mungu Niwapo; Humo Barani Na Baharini,
Yeye Wa Mbinguni Anilinda; Baba Wa Mbinguni Anilinda.

Namwamini, Mungu Anitunza (Anitunza)
Milimani (Milimani) Au Baharini (Baharini) Baharini
Moyo Wangu (Moyo Wangu) Aulinda (Aulinda).
Baba Wa Mbinguni Anilinda.

2. La Waridi Alinawirisha, Na Huyo Tai Juu Angani,
Nami Kweli Ananilinda, Baba Wa Mbinguni Anilinda.

3. Tunduni Mwa Simba Namwamini, Kwenye Vita Ama Gerezani,
Motoni Na Furikoni, Baba Wa Mbinguni Anilinda.

4. Bondeni Mwa Giza Na Upweke, Mchunga Wangu Yuanilinda,
Kwa Upole Aniongoza; Baba Wa Mbinguni Anilinda.

(NK # 131a) KWA MAHITAJI YA KESHO
Lord For Tommorrow And It’s Needs

1. Kwa Mahitaji Ya Kesho, Sina Ombi;
Unilinde Nisitende, Dhambi Leo;
Nisiseme Neno Baya, Mkombozi,
Nisifikiri Uovu, Leo Hivi.

2. Ningefanya Kazi Sawa Na Kuomba;
Ningekuwa Mtu Mwema Kila Saa;
Mapenzi Yako Nifanye, Na Kutii;
Nitoe Mwili Dhabihu, Leo Hivi.

3. Kama Keo Ningekufa Kwa Ghafula,
Nitegemee Ahadi Zako Bwana.
Kwa Mahitaji Ya Kesho Sina Ombi;
Uniongoze, Nishike Leo Hivi.
(NK # 132) BWANA NI MCHUNGA The Lord Is My Sherpherd

1. Bwana Ni Mchunga, Sitahiji;
Majani Mabichi Mlisho Yangu.
Ananinywesha Maji Matulivu;
Atanirudisha Nikipotea.

2. Nipitapo Bondeni Mwa Mauti
U Mlinzi Wangu—Sitaogopa;
Fimbo Lako Latoshakunilinda;
Ukinifariji Sina Hasara.

3. Kati Ya Mateso Mea Waandaa,
Na Kikombe Changu Kinafurika;
Umenipaka Kichwani Mafuta;
Nitaulizaje Zaidi Kwako?

4. Wema Na Fadhili Zinifuate
Siku Zangu Zote Hata Milele;
Nami Nitakaa Nyumbani Mwa Bwana
Katika Ufalme Wa Pendo Lake.
(NK # 133) PO POTE NA YESU
Anywhere With Jesus

1. Po Pote Na Yesu Nina Furaha;
Anitumako Yesu Ndiyo Raha.
Asipokuwako Hapanifai,
Akiwapo Yesu, Mimi Sitishwi.

Po Pote, Po Pote, Sina Mashaka:
Po Pote Na Yesu Naweza Kwenda.

2. Akiwapo Yesu, Si Peke Yangu;
Na Nijapotupwa, Akali Wangu;
Ajaponiongoza Njia Nbaya,
Niwapo Na Yesu Nashukuria.

3. Akiwapo Yesu Naweza Lala,
Naweza Pumzika Hata Kiyama;
Kisha Nitakwenda Kwake Milele,
Akiwapo Yesu Furaha Tele.

(NK # 134) TAFUTA DAIMA UTAKATIFU Take Time To Be Holy

1. Tafuta Daima Utakatifu;
Fanya Urafiki Na Wakristo Tu;
Nena Siku Zote Na Bwana Wako,
Baraka Uombe Kwa Kila Jambo.

2. Tafuta Saima Utakatifu:
Uwe Peke Yako Ukimwabudu;
Ukimwangalia Mwokozi Wako,
Utabadilishwa Kama Alivyo.

3. Tafuta Daima Utakatifu;
Kiongozi Wako Awe Yesu Tu;
Katika Furaha Au Huzuni
Dumu Kumfuata Yesu Mwokozi.

4. Tafuta Daima Utakatifu;
Umtawaze Roho Moyoni Mwako,
Akikuongoza Katika Haki,
Hufanywa Tayari Kwa Kazi Yake.
(NK # 135) KWA MAOMBI NACHANGAMKA
Sweet Hour Of Prayer

1. Saa Heri Ya Maombi, Sasa Kwako Tunarudi,
Sumbuku Ya Kuondoa, Shida Zitu Na Pungufu.
Taabuni Mara Nyingi, Roho Zetu Zimepona,
Mashakani Tumeshinda, Wakati Wa Saa Tamu.

2. Saa Heri Ya Maombi, Twapelika Dhiki Zetu
Kwake Aliyeahidi Kubariki Wenye Haja.
Huagiza Tumwendee, Tutegemee Neno Lake,
Hivyo Tumwekee Yote, Wakati Wa Saa Tamu.

3. Saa Heri Ya Maombi, Tutazidi Kuingia
Bomani Mwetu Na Ngome, Hata Tuishapo Mwendo.
Yesu Atatusikea, Tutamtafuta Daima,
Na Tu-taka-poku-tana Tutamwona—Saa Tamu!
(NK # 136) NIWE KAMA YESU
Teach Me Father

1. Unifundishe, Baba; Ile Njia Ya Sala;
Uniendeshe Sana, Niwe Kama Yesu.

Niwe Kama Yesu, Niwe Kama Yesu,
Uniongoze, Baba; Niwe Kama Yesu.

2. Unipe Pendo, Baba, Watu Kuwaokoa;
Nyumbani Na Mjini. Niwe Kama Yesu.

3. Na Unifahamishe, Wakati Ndio Mfupi;
Unibidishe, Bwana, Niwe Kama Yesu.

(NK # 137) SAA HERI YA SALA
’Tis The Blessed Hour Of Prayer

1. Saa Heri Ya Sala Tunapojidhili,
Kama Tukija Kwake Yesu Rafiki.
Tukiwa Na Imani Kwamba Yu Mlinzi,
Waliochoka Sana Watapata Raha.

Saa Ya Sala, Iliyo Heri;
Waliochoka Sana Watapata Raha.

2. Saa Heri Ya Sala, Ajapo Mwokozi,
Ili Awasikie Watoto Wake.
Hutwambia Tuweke Miguuni Pake
Mizigo Yetu Yote: Tutapata Raha.

3. Saa Heri Ya Sala, Wawezapo Kuja
Kwa Bwana Yesu Wanaojaribiwa;
Moyo Wake Mpole, Atawarehemu;
Waliochoka Sana Watapata Raha.

4. Saa Heri Ya Sala Tutakapopewa
Mibaraka Ya Roho, Tukimwamini;
Kwa Kuamini Kweli Hatutaogopa;
Waliochoka Sana Watapata Raha.
(NK # 138) NITAKUANDAMA KOTE
I Will Follow Thee

1. Nitakuandama Kote, Nitakapoagizwa,
Wewe Ukiniongoza Nami Nitaandama.

Nitakuandama Kote, Naam, Ulinifia;
Kwa Neema Yako Bwana Napenda Kuandama.

2. Njia Ijapoparuza Kwa Miiba Na Fujo,
Ulitangulia Mbele Nami Nitaandama.

3. Nijapokuta Taabu Na Majaribu Kote,
Nakumbuka Shida Yako, Nami Nitaandama.

4. Nijapoona Ukiwa Na Mateso Makali,
Wewe Uliyatikiza Nami Nitaandama.

5. Ijapo Wanipeleka Vilindini Mwa Giza,
Wewe Uliyatikiza Nami Nitaandana.

(NK # 139) ULINIIMBIE TENA
Sing Them Over Again

1. Uliniimbie Tena, Neno La Uzima;
Uzuri Wake Nione, Neno La Uzima;
Neno Hili Zuri, Lafundisha Kweli:

Maneno Ya Uzima Ni Maneno Mazuri,
Manemo Ya Uzima Ni Naneno Mazuri.

2. Kristo Anatupa Sote, Neno La Uzima:
Mwenye Dhambi Asikie Neno La Uzima:
Latolewa Bure, Tupate Wokovu:

3. Neno Tamu La Injili, Neno La Uzima;
Mwenye Dhambi Asikie Neno La Uzima:
Litatutakasa, Kwa Haki Ya Mwana:
(NK # 140) HIVI NILIVYO UNITWAE
Just As I Am

1. Nitwae Hivi Nilivyo, Umemwaga Damu Yako,
Nawe Ulinyoniita, Bwana Yesu, Sasa Naja.

2. Hivi Nilinyo; Si Langu Kujiosha Roho Yangu;
Nisamehe Dhambi Zangu, Bwana Yesu, Sasa Naja.

3. Hivi Nilivyo; Sioni Kamwe Furaha Moyoni,
Daima Ni Mashakani, Bwana Yesu, Sasa Naja.

4. Hivi Nilivyo Kipofu, Maskini Na Mpungufu;
Wewe Ndiwe U Tajiri, Bwana Yesu, Sasa Naja.

5. Hivi Nilivyo, Mimi Tu, Siwezi Kujiokoa;
Na Wewe Hutanikataa, Bwana Yesu, Sasa Naja.

6. Hivi Nilivyo; Mapenzi Yamenipa Njia Wazi;
Hali Na Mali Sisazi, Bwana Yesu, Sasa Naja.

(NK # 141) CHINI YA MSALABA
Beneath The Cross Of Jesus
1. Chini Ya Msalaba Nataka Simama;
Ndio Mwamba Safarini, Wa Kivuli Chema;
Ni Kweli Kwa Roho Yangu Ni Tuo Kamili,
Tatua Mzigo Wangu; Wakati Wa Hari.

2. Hapa Ni Pema Sana, Ni Ngome Kamili;
Hapa Yameonekana, Mapenzi Ya Kweli;
Kama Alivyoonyeshwa; Yakobo Zamani,
M-salaba Umekuwa Ngazi Ya Mbinguni.

3. Na Yesu Msalabani Walim-kimea,
Alikufa Niokoke Niliyepotea:
Naona Ajabu Sana Ya Manbo Mawili
Jinsi Alivyonipenda Nisiyestahili.

4. Atakayeonana Na Yesu Mbinguni,
Njia Yake Aanzapo Ni Msalabani;
Wokovu Upo Hapa Tu, Mwingine Hapana,
Kisha Kuna Furaha Kuu Pamoja Na Bwana.

(NK # 142) NASIKIA SAUTI YAKO
I Hear Thy Welcome Voice

1. Nasikia Mwito, Ni Sauti Yako;
Nikasafiwe Kwa Damu Ya Kwangikwa Kwako.

Nimesongea Mtini Pako,
Unisafi Kwa Damu Ya Kwangikwa Kwako.

2. Ni Mnyonge Kweli, Umenipa Nguvu;
Ulivyonisfi Taka Ni Utimilivu.

3. Yesu Hunijuvya: Mapenzi Imani,
Tumai, Amani, Radhi, Hapa Na Mbinguni.

4. Napata Wokovu, Wema Na Neema;
Kwako Bwana Nina Nguvu Na Haki Daima.
(NK # 143) NAAMINI
Father, I Stretch My Hands

1. Baba Sina Msaada Ila Kwako Pekee;
Kama Kwangu Ungefichwa, Nifanyeji, Baba?

Sasa Hivi Naamini Yesu Alikufa,
Aliimwaga Damu Yake, Nitoke Dhambini.

2. Naamini Mwana Wako Nipe Nguvu Zako;
Nijazie Mahitaji, Katika Saa Hii.

3. Nifuraha Gain Kwangu Kukuona Uso!
Nijue Sauti Yako, Nipate Neema.
(NK # 144) NI WAKO BWANA
I Am Thine O Lord

1. Ni Wako Bwana, Ninasikia Unaponena Nami;
Lakini, Kweli, Nataka Kwako Nizidi Kusongea.

Bwana Vuta, (Vuta) Nije Nisongee
Sana Kwako Mtini.
Bwana, Vuta, Vuta, Nije Nisongee
Pa Damu Ya –Tha-ma-ni.

2. Niweke Sasa Nikatumike Kwa Nguvu Za Neema;
Uyapendayo Nami Nipende Nizidi Kukwandama.

3. Nina Furaha Tele Kila Saa Nizungumzapo Nawe;
Ninanena Kama Kwa Rafiki Nikipiga Magoti.

(NK # 145) NAMTAKA BWANA YESU
Take The World

1. Ulimwengu Siutaki, Namtaka Bwana Yesu;
Dunia Hunidanganya; Yesu Yu Mwaminifu.

Rehema Ni Ya Ajabu! Pendo Bila Kipimo!
Wokovu Mkamilifu, Amana Ya Uzima.

2. Ulimwengu Siutaki, Namtaka Bwana Yesu;
Kati Ya Dhoruba Kali Yeye Wimbo Mtamu.

3. Ulimwengu Siutaki, Namtaka Bwana Yesu;
Safarini Duniani Yeye Furaha Yangu.

4. Ulimwengu Siutaki, Namtaka Bwana Yesu;
Msalaba Naamini, Hata Namwona Yesu.

(NK # 146) TWAE WANGU UZIMA
Take My Life And Let It Be

1. Twae Wangu Uzima Sadaka Ya Daima;
Twae Saa Na Usiku Zikutukuze Huku.

2. Twae Mikono Nayo, Ifanye Upendayo,
Twae Yangu Miguu, Kwa Wongozi Wako Tu.

3. Twae Sauti Yangu, Niimbe Kwa Mungu Tu;
Itwae Na Midomo, Ijae Neno Lako.

4. Twae Dhahabu Pia Na Yote Ya Dunia;
Twae Yangu Hekima, Upendavyo Tumia.

5. Nia Itwae, Mungu, Haitakuwa Yangu;
Twae Moyo; Ni Wako, Uwe Makazi Yako.

6. Twae Mapenzi Yangu, Sifa Za Moyo Wangu;
Twae Kabisa Nafsi Niwe Wako Halisi.

(NK # 147) UISHI NDANI YANGU Love Out Thy Life Within Me

1. Tawala Ndani Yangu, Ee Yesu, Mfalme.
Uwe Kwangu Majibu Kwa Maswali Yangu;
Uishi Ndani Yangu, Wewe, Mwongozi
Utumishi Ni Wangu, Wako Utukufu.

2. Hekalu Nimetoa, Umelisafisha;
Sasa Fahari Yako Imulike Ndani;
Dunia Iwe Kumya, Mwili Sasa Uwe
Mtumwa Mtulivu Wa Kukutii Tu.

3. Viungo Vyake Mwili, Vyote Vikungoja
Tayari Vikuutwa Kwenda, Kusimama;
Bila Manumguniko Au Malaumu,
Au Kusumbuliwa, Pasipo Majuto.

4. Niwe Na Utulivu Pasipo Haraka;
Tayari Kungojea Maagizo Yako.
Tawala Ndani Yangu, Ee Yesu, Mfalme,
Uwe Kwanfgu Majibu Kwa Maswali Yote.
(NK # 148) UNIVUTE KARIBU
Closer To Thee, My Father, Draw Me

1. Univute Karibu, Baba, Unikumbatie;
Unisogeze Kifuani, Nataka Pumziko.

Univute Karibu (Vuta, Univute Karibu)
Kwa Kamba Za Upendo,
(Kwa Kamba, Kamba Za Upendo)

Univute (Kwa Kamba Za Upendo, Univute Karibu)
Karibu Nawe. (Univute Karibu)

2. Univute Mwokozi Wangu, Na Tusiachane;
Mikono Yako Juu Yangu Leo Nione.

3. Univute Kwa Roho Yako, Nifanane Nawe;
Unioshe, Unihuishe, Niwe Safi, Huru.
(NK # 149) KUWA WAKE YESU
Would You Live For Jesus

1. Kuwa Wake Yesu, Je! Ni Kusudi Lako?
Ungeenda Naye Njia Nyembamba?
Unataka Aubebe Mzigo Wako?
Awe Mwongozi Wako.

Uwezo Wake Unakutosha; Na Danu Yake Itakusafi;
Kwa Vile Ukubali Ni Bora; Afanye Mapenzi Yake Nawe

2. Unataka Kutika Unapokwita?
Kupata Amani Kwa Kumpa Vyote?
Wataka Uwezo Usianguke Kamwe?
Awe Mwongozi Wako.

3. Wataka Raha Katiak Ufalme Wake?
Ungeshinda Kwa Majaribu Yote?
Ungefanya Kazi Yake Vizuri Sana?
Awe Mwongozi Wako.

(NK # 150) HASHA MANENO MABAYA YASITOKE
Angry Words! Oh, Let Them Never

1. Hasha, Maneno Mabaya Yasitoke Kinywani
Moyo Mwema Uzuie Ndimi, Zisichafuke.

“Nanyi Pendeni”, A-sema Yesu, u-u
(Mpendane) (Mpendane)
Kama Mwanzo Alivyotupenda: a-ah

“Nanyi Pendeni”, A-livyotupe-enda:
(Mpendane) (Mpendane)
Wana, Tiini Amri Hii. (Amri Heri Hii).

2. PENDO Ni Mtakatifu; Urafiki; Mzuri:
Visiharibike Mara Kwa Kunena Vibaya.

3. Tusinene Kwa Hasira, Inazaa Huzuni,
Pendo Lako Ee Mwokozi, Inatosha Tushindi.

(NK # 151) HUNIONGOZA MWOKOZI
He Leadeth Me

1. Huniongoza Mwokozi, Ndipo Nami Hufurahi,
Niendapo Pote Napo, Ataniongoza Papo.

Kuongoza Hunishika; Kwa Mkono Wa Hakika;
Nitaandamana Naye Kristo Aniongozae.

2. Pengine Ni Mashakani Nami Pengine Rahani;
Ni Radhi, Ijayo Yote, Yupo Nami Siku Zote.

3. Mkono Akinishika Kamwe Sitanung’unika;
Atakachoniletea Ni Tayari Kupokea.

4. Nikiisha Kazi Chini Sita Kimbia Mauti;
Kushinda Ni Ya Hakika Nikiongozwa Na Baba.

(NK # 152) KARIBU NA WEWE, MUNGU WANGU
Nearer, My God, To Thee
1. Karibu Na Wewe, Mungu Wangu:Karibu Zaidi Bwana Wangu,
Siku Zote Niwe Karibu Na Wewe,
Karibu Zaidi, Mungu Wangu.

2. Mimi Nasafiri Duniani, Pa Kupumzika Sipaoni,
Nilalapo Niwe Karibu Na Wewe,
Karibu Zaidi, Mungu Wangu.

3. Yote Unipayo Yanivuta; Pa Kukaribia Nitapata;
Na Nielekezwe, Karibu Na Wewe,
Karibu Zaidi, Mungu Wangu.

4. Na Kwa Nguvu Zangu Nikusifu;
Mwamba, Uwe Maji Ya Wokovu
Mashakani Niwe Kaaribu Na Wewe;
Karibu Zaidi, Mungu Wangu.

5. Na Nyumbani Mwa Juu, Baba Yangu
Nikinyakuliwa Toka Huko,
Kwa Furaha Niwe Pamoja Na Wewe,
Karibu Zaidi, Mungu Wangu.

(NK # 153) FIKIRA MOJA TU
One Sweetly Solemn Thought

1. Fikira Moja Tu
Hurejea Tena
Nimekaribia Mbingu
Zaidi Ya Jana.

Karibu Na Kwetu Mbingu,
Karibu Na Kwetu Sasa,
Nikwone Karibu.

2. Karibu Na Kwetu
Na Kwenye Makao;
Kiti Cha Enzi Cha Mungu,
Pahali Pa Mto.

3. Kamilisha Yesu,
Kuamini Kwangu;
Nikifika Mwisho Wangu,
Nikwone Karibu.
(NK # 154) YANIPASA KUWA NAYE
I Must Have The Saviour With Me

1. Yanipasa Kuwa Naye, Mwokozi Bwana Wangu,
Akiwa Karibu Nami, Napata Nguvu Kweli.

Moyo Hauogopi, Wala Kitikisika.
Nitakwenda Apendapo.
Kwa Kuwa Anilinda.

2. Yanipasa Kuwa Naye, Kwani Nategemea;
Anaweza Kufariji Na Maneno Matamu.

3. Yanipasa Kuwa Naye Maisha Yangu Yote;
Yakiwapo Majaribu Na Mashaka Yo Yote.

4. Yanipasa Kuwa Naye Katika Njia Zangu;
Macho Yake Yaongoza Hatua Zangu Zote.

(NK # 155) NJIANI HUNIONGOZA
All The Way My Saviour Leads Me

1. Njiani Huniongoza, Yesu Wangu, Mwokozi;
Rehema Hatapunguza, Milele Kiongozi.
Ina Raha Kwandamana Duniani Daima;
Nijaposumbuka Sana, Yeye Hutenda Vyema,

2. Njiani Huniongoza, Hupunguza Matata;
Nikiugua Hupoza, Na Njaani Nashiba.
Lichokapo Guu Langu Nguvu Zikapungua,
Jiwe Lilo Mbele Yangu Hunibubujikia.

3. Njiani Huniongoza, Kwa Pendo Zilizo Kuu,
Mwisho Atanituliza, Kwake Baba Yangu Juu.
Nikivikwa Kutokufa, Nikae Na Mwokozi,
Nitamsifu Sana; Sifa: “Kweli Ni Kiongozi.”
(NK # 156) UNIONGOZE, YEHOVA
Guide Me, O Thou Great Jehovah

1. Uniongoze, Yehova, Ni Msafiri Chini;
Ni Mnyonge, U Hodari, ‘Nilinde Kwa Mkono.
Unitunze, Unilinde, Unionyeshe Njia!

2. Na Kisima Cha Uzima, Maji Ya Utabibu,
Fungua Kwa Moyo Wangu, Ninywe Na Kuponyeka!
Uninyweshe, Unilishe, Hata Nimetosheka.

3. Wakati Wa Kuuvuka, Ule Mto Yordani,
Hofu Yangu Ufariji, ‘Nione Uso Wako.
Nyimbo Shangwe, Nyimbo Shangwe, Nitaimba Daima.
(NK # 157) MFALME YU MLANGONI
The Coming King

1. Mfalme Yu Mlangoni, Ndiye Aliyetufia;
Mara Wote Wampendao Atawakusanya.

Yuaja, Yuaja, Mlangoni Anasimama;
Anakuja, Anakuja, Kuja Kwake Karibu.

2. Dalili Za Kuja Kwake Zinazidi Kutimizwa;
Karibu Wateule Watamlaki Bwana.

3. ’Sitafute Duniani Amani Wala Furaha,
Mpaka Bwana Arudi Dhambi Kuondoa.

4. Tutakaa Na Mwokozi Makaoni Ya Milele;
Daima Tutafurahi Kuwa Watu Wake.
(NK # 158) U Mwendo Gani Nyumbani? How Far From Home?

1. U Mwendo Gani Nyumbani? Mlinzi Akanijibu,
“Usiku Sasa Waisha, Machweo Karibu.”
Usihuzu-nike Tena, Bali Ulemee Mwendo
Hata Ushike Ufalme Kule Mwangani Juu.

2. Na Tena Niliuliza, Nchi Yote Ikajibu:
“Sasa Mwendo Watimika, Milele Karibu.”
Usihuzu-nike Tena, Ishara Kuu Zasonga
Na Viumbe Vyangojea Sauti Ya Bwana.

3. Nikamwuliza Shujaa, Ndivyo Kanitia Moyo:
“Shikilia Mapigano, Kitambo Yaisha.”
Usihuzu-nike Tena, Kazi Ifanye Kwa Moyo;
Tumeahidiwa Tunu Tuishapo Shinda.

4. Siyo Mbali Na Nyumbani! Fikara Tamu Njiani,
Latupoza Roho, Nalo Lafuta Machozi
Usihuzu-nike Tena, Kitambo Tutakutana
Wenye Furaha Kamili Nyumbani Mwa Baba.
(NK # 159) ANAKUJA UPESI How Sweet Are The Tidings

1. Anakuja Upesi, Yesu Bwana Wetu, Msafiri Mbali Na Kwao;
Alisema Dhahiri, “Nitakuja Tena”; Amina; Na Uje, E Bwana.

Yuaja, Yesu Atarudi Sasa; Anakuja Duniani.
Wasafiri Wote Watapumzika Yesu Anaporudi Tena.

2. Makaburi Yote Wafu Wanapolala
Yatafunguliwa Tena;
Na Mamilioni Pale Wataondoka Tena,
Wasione Machozi Kamwe.

3. Hatuta-tengana Na Hao Tena Huko;
Nyimbo Nzuri Tutaimba.
Watakusanyika ’Toka Kila Kabila,
Miguuni Pa Mwana-Kondoo.

4. Aleluya Amin! Aleluya Tena!
Upendo Wake Unashinda!
Tutamsifu Milele, Hata Tutashangaa,
Jinsi Alivyo Tukomboa.

(NK # 160) WATAKATIFU KESHENI
Watch, Ye Saints

1. Watakatifu Kesheni, Nguvu Za Mbingu Zagonga;
Washeni Taa Tayari Kwa Kurudi Kwake Bwana.

Yuaja, Yesu Mfalme, Yuaja Myenye Fahari,
Yesu Yuaja Enzini. Karibu Yesu, Uje.

2. Piga Mbiu, Tangazeni Habari Ya Ukombozi,
Ya Mponya Wa Upendo Nayo Nguzu Za Samaha.

3. Falme Nyingi Zaangushwa, Panda Ya Saba Hulia;
Tangaza Neema Yake Kabla Ya Kupita Saa.

4. Mataifa Yapotea, Nchi Zajaa Uchungu:
Kistro Anaharakisha, Unabii Unatimizwa.

5. Wenye Dhambi Njoni Sasa, Kristo Awapatanishe,
Mbio Twaeni Neema, Kitambo Muda Waisha.

(NK # 161) PIGA PANDA
Lift Up The Trumpet

1. Piga Panda Na Ya Makelele; Yesu Yuaja Tena!
Ipaze Sauti, Imba Sana; Yesu Yuaja Tena!

Anakuja, Anakuja; Yesu Yuaja Tena!

2. Itoe Mwangi Sana Vilima; Yesu Yuaja Tena!
Yuaja Kwa Utukufu Mwingi, Yesu Yuaja Tena!

3. Itangazwe Mahali Po Pote; Yesu Yuaja Tena!
Mwokozi Aliye Tufilia, Yesu Yuaja Tena!

4. Kuona Machafuko Twajua Yesu Yuaja Tena!
Mataifa Ya Kasiriana, Yesu Yuaja Tena!

5. Maradhi, Hofu Hutuhubiri Yesu Yuaja Tena!
Taabu, Njaa Hutulilia Yesu Yuaja Tena!

(NK # 162) TUMAINI LIKO
There Is A Blessed Hope

1. Tumaini Liko La Thamani Kuu,
Kupita Anasa Tupu Zake Ulimwengu.

2. Pana Nyota Nzuri: Nuru Itoayo
Kwetu Wakati Wa Kifo Ndio Ufufuo.

3. Zikiumwa Roho Na Hofu, Mashaka,
Sauti Hutuambia Mungu Hutupenda.

4. Kutoka Kalwari Sauti Hunena;
Nyota Ni Nuru Ya Mbingu, Tumaini Letu.

(NK # 163) ANAKUJA, BWANA YESU
It May Be A Morn

1. Pengine Ni Saa Ya Kupambazuka,
Mishale Ya Ju-a Ipenyapo Giza,
Kwamba Atakuja Yesu Mtukufu, Awapokee Wake.

Bwana Itakuwa Lini Tutapoimba
Anakuja, Bwana Yesu, Aleluya, Amin, Aleluya, Amin.

2. Pengine Mchana, Pengine Jioni,
Pengine Usiku Wa Manane, Giza
Itatoweka Kwa Fahari Akija, Awapokee Wake.

3. Majeshi Yake Yataimba “Hosana,”
Na Wataka-ti-fu Waliotukuzwa
Watamsifu Kwa Kuwa Amekuja, Awapokee Wake.

4. Furaha Tukiitwa Pasipo Kufa,
Pasipo Kuona Maradhi, Machozi;
Kuchukuliwa Winguni Kwa Fahari, Akija Kwa Watu Wake.
(NK # 164) MISHALE YA NURU
The Golden Morning

1. Unakaribia Wakati Wa Kuja Kwa Yesu.
Atawachukua Watu Wake Nyumbani Juu.

Tunaiona Mishale Ya Nuru, Inayopenya Giza;
Tunaiona Mishale Ya Nuru Ya Ufunuo.

2. Injili Inatangazwa Pote Kwa Mataifa;
Bwana Wa Arusi Atakuja Na Tarumbeta.

3. Pamoja Na Malaika Zake Bwana Arudi,
Awapeleke Waaminifu Wasife Tena.

4. Wapenzi Waliotengwa Kale Watakutana;
Machozi Yao Wenye Huzuni Yatafutika.

(NK # 165) “UWE IMARA”
Sweet Promise Is Given

1. Ahadi Tamu, Kwa Waamini,
Tazama Nakuja Upesi Sana.
Uwe Imara, Hatari Kubwa:
Ndugu Usilale, Bali Ukeshe.

Uihifadhi Imani Yako,–Dunia Mpya Itatolewa
Njoo Ingia Furaha Yangu;
Taji Zinangoja; Uwe Imara.

2. Tatakesha Na Kutoa Sala;
Atakuja Kama Mwivi Kwa Wengi;
Ya Kwamba Yu Karibu Twajua,
Ila Hatujui Ni Siku Gani.

3. Tunategemea Neno Lake,
Ambalo Latangaza Kuja Kwake,
Tumaini Letu Ni Ahadi:
“Naja Karibuni, Uwe Imara.”
(NK # 166) FURAHA KWA ULIMWENGU
Joy To The World

1. Furaha Kwa Ulimwengu, Bwana Atakuja!
Kila Moyo Umpokee, Viumbe Imbeni,
Viumbe Imbeni, Viumbe Vyote Imbeni.

2. Na Bwana Atatawala: Watu Na Waimbe;
Miti, Milima Na Mawe; Kariri Furaha,
Kariri Furaha, Kariri Furaha Kubwa.

3. Atatawala Kwa Wema; Atawafundisha
Mataifa Haki Yake, Ajabu Za Pendo,
Ajabu Za Pendo, Ajabu Za Pendo Lake.
(NK # 167) YU HAI, YU HAI
(He Lives, He Lives)

1. Yesu Bwana Mwokozi Aishi Milele,
Najua Kwamba Yupo Pamoja Na Mimi;
Sauti Nasikia, Rehema, Naona;
Wakati Namhitaji, Yupo Nami.

Yu Hai, Yu Hai,Yu Hai Bwana Yesu!
Atembea, Azungumza, Nami Siku Zote.
Yu Hai, Yu Hai, Kutoa Uzima!
Hivi Ndivyo Nijuavyo,
Yu Hai Ndani Yangu!

2. Ulinzi Wake Upo Naona Dhahiri,
Miguu Ichokapo, Sikati Tamaa.
Najua An’ongo-za, Kupita, Dhoruba,
Siku Ya Kuja Kwake Nitamwona.
(NK # 168) TARUMBETA YA MWANA
When The Trumpet Of The Lord

1. Tarumbeta Ya Mwana Itakapolia Mara,
Milele Itakapopambazuka,
Nao Wa Haki Watakapokusanyika Ng’ambo,
Majina Yaitwapo, Lo!—Niweko.
Majina Yaitwapo, Lo!—
Majina Yaitwapo, Lo!—
Majina Yaitwapo, Lo!—
Majina Yaitwapo, Lo!—Niweko.

2. Siku Ile Watakatifu Watakapoamka
Na Kuondoka Huru Kaburini
Watakapokusanyika Makaoni Kule Juu,
Majina Yaitwapo, Lo—Niweko.

3. Tutende Kazi Kwa Yesu Mchana Kutwa Kwa Bidii,
Tutangaze Kote Pendo Lake Kuu,
Nayo Kazi Itakapotimika Hapa Chini
Majina Yaitwapo, Lo—Niweko.
(NK # 169) TUTASHINDAE HUKUMUNI?
When Jesus Shall Gather

1. Hapo Yesu Atakapoita Mataifa Mbele Yake,
Tutashindaje Kwenye Hukumu Mbele Ya Kiti Cha Enzi?

Atakusanya Ngano Ghalani, Atatupambali Makapo;
Tutashindaje Hukumuni Siku Kuu Ya Kiyama?

2. Je, Tutasikua Neno Tamu: “Vema, Wewe Mtumwa Mwema,”
Ama Wenye Uchunguna Hofu Tutakatazwa Ufalme?

3. Atakubali Tu Kwa Furaha Watoto Wake Wapendwa,
Atawapa Mavazi Meupe, Wakea Tayari Kumlaki.

4. Hivyo Tukeshe, Nasi Tungoje, Wenye Taa Zinazo Waka;
Tutakapoitwa Arusini Tuwe Tayari Kumlaki.

5. Roho Ikielekea Mbingu; Twangoja Wenye Saburi,
Hata Safari Yetu Iishe, Tukae Kwake Milele.
(NK # 170) JINA LANGU LIMEANDIKWA JE?
Lord, I Care Not For Riches

1. Siitafuti Mali, Wala Utajiri;
Nataka Kwa Yakini Nipate Mwokozi.
Chuoni Mwa Ufalme, Niambie Yesu,
Jina Langu Yakini Limeandikwa, Je?

Limeandikwa, Je? Jina Langu Huko?
Kitabuni Mbinguni, Limeandikwa Je?

2. Dhambi Zangu Ni Nyingi, Ni Kama Mchanga,
Lakini Damu Yako, Mwokozi, Yatosha;
Kwani Umeahidi: Zijapo Nyekundu
Zitakuwa Nyeupe Ilivyo Theluji.

3. Mji Mzuri Sana, Wa Majumba Makuu,
Walipo Malaika, Mji Bila Ovu;
Wakakapo Walio Na Mavazi Safi,
Limeandikwa Sasa, Jina Langu Huko?

(NK # 171) HUKUMU
The Judgment Has Set

1. Imeanzishwa Hukumu Mbinguni; Tutasimamaje Pale
Apimapo Mungu Hakimu, Kula Wazo Na Tendo?

Tutasimamaje Sote; Katika Siku Kuu Ile?
Dhambi Zitu Zitafutika; Ama Zitatuangusha?

2. Wametangulia Wafu Kupimwa, Kitambo Ndipo Wahai,
Watapokea Neno La Mwisho, Vitabuni Mwa Mungu.

3. Tutasimamaje Usiku Ule, Siri Zetu, Kila Moja,
Zafunuliwa Toka Vitabu; Yesu Atusaidie!
(NK # 172) MFALME AJAPO
Called To The Feast

1. Mfalme Wetu Atuita Tukae Karamuni Kwake;
Itakuwaje Nasi Kule Bwana Akija?

Bwana Ajapo, Ndugu, Bwana Ajapo!
Itakuwaje Na Sisi, Bwana Akija?

2. Atavikwa Vizuri Sana,Taji Badala Ya Miiba;
Kweli Tokeo La Fahari Bwana Ajapo.

3. Kwa Fufaha Awakubali Wenye Mavazi Ya Arusi;
Tu Wa Heri Tukimridhisha Bwana Ajapo.

4. Kutakuwako Na Utengo: Watalia Waliomwasi;
Cha Kutisha Kitambo Kile Kristo Ajapo!

5. Mfalme Utupe Neema Sisi Tunapokungojea
Tusiogope Kukuona Ujapo Bwana.

(NK # 173) HATUJUI SAA
We Know Not The Hour

1. Hatujui Saa-a Ya Kuja Kwwa Bwana,
Lakini Dalili Zinasema Karibu
Atakaporudi,–Lakini Kwa Kweli; Hatujui Saa-a.

Atakuja, (Kwa Vile Tukeshe);
Atakuja, (Mwokozi, Aleluya)!
Atakuja Kwa Fa-hari Ya Baba Yake,–
Hatujui Saa-a.

2. Pana Nuru Kwa-o Wapendao Haki,
Pana Kweli Ka-tika Chuo Cha Mungu;
Unabii Hu-fundisha Kuja Kwake,–Hatujui Saa-a.

3. Tutakesha Na Tutaomba Daima,
Tutafanya Ka-zi Mpaka Akija,
Tutaimba Na Tutasoma Ishara,–Hatujui Saa-a.

(NK # 174) TUKIMNGOJEA
We Know Not The Time When He Cometh

1. Sijui Atakapokuja, Mchana Au Usiku;
Labda Saa-a Ya Alasiri, Pengine Ni Alfajiri.
Hutwambia Tuwe Tayari, Taa Zetu Tusizime;
Ili Ajapo Atukute; Tuwe Tukimngoja Yeye.

Tu – Kimngojea – A, (Kukesha, Tunakungoja Wewe)
Tu – Kimngojea – A, (Kukesha, Tunakungoja Wewe)
Tu – Kimngojea – A, (Kukesha, Tunakungoja Wewe)
Twakesha, Twamngoja Yeye.

2. Nakumbuka Huruma Zake, Bei Ya Wokovu Wetu:
Aliacha Nyumba Tukufu; Awafilie Wabaya.
Ninadhani Itampendeza, Kama Sisi Watu Wake,
Tukionyesha Pendo Letu, Tuwe Tukimngoja Yeye

3. Ee Yesu, Mwokozi Mpendwa, Wajua Nalihifadhi Tumaini La Kukuona; La Kukaribishwa Nawe
Ukija Kwa Watu Wengine, Kama Mhukumu Wao, Kwangu Utakuwa Rafiki,–Nakesha; Nakungojea.
(NK # 175) USO KWA USO
Face To Face

1. Nitaonana Na Yesu, Uso Kwa Uso Kweli;
Siku Ile Shangwe Tele Nitamwona Mwokozi.

Tutaonana Kwa Macho, Huko Kwetu Mbinguni;
Na Kwa Utukufu Wake, Nitamwona Milele.

2. Sasa Siwezi Kujua Jinso Alivyo Hasa,
Bali Atakapokuja, Nitamwona Halisi.

3. Mbele Yake Yafukuzwa Machozi Na Huzuni;
Kipotovu Kitanyoshwa, Fumbo Litafumbuka.

4. Uso Kwa Uso! Hakika Palepale Furaha;
Nitafurahi Kabisa Nikimwona Mwokozi.
(NK # 176) ATI TUONANE MTONI?
Shall We Gather At River

1. Ati Twonane Mtoni? Maji Mazuri Ya Mbingu;
Yanatokea Mwangani, Penye Kiti Cha Mungu.

Naam, Twonane Mtoni! Watakatifu, Kwenu Ni Mtoni!
Tutakutanika Kule Mtoni Penye Kiti Cha Mungu.

2. Tukitembea Mtoni, Na Yesu Mchunga Wetu,
Daima Tu Ibadani Usoni Pake Kwetu.

3. Tukisafiri Mtoni, Tutue Ulemeao,
Wema Wa Mungu Yakini: Una Taji Na Vao!

4. Kwang’ara Sana Mtoni, Cha Mwokozi Ni Kioo,
Milele Hatuachani Tumsifu Kwa Nyimbo.

5. Karibu Sana Mtoni, Karibu Tuatawasili,
Mara Huwa Furahani Na Amani Ya Kweli.

(NK # 177) KAZI YANGU IKIISHA
When My Life-Work Is Ended

1. Kazi Yangu Ikisha, Nami, Nakiokoka,
Na Kuvaa Kutokuharibika,
Nitamjua Mwokozi; Nivukapo Ng’amboni
Atakuwa Wa Kwanza Kunilaki.

Nitamjua, Nitamjua, Nikimwona Uso Kwa Uso;
Nitamjua, Nitamjua, Kwa Alama Za Misumari.

2. Kuona Uso Wake Utanipa Furaha,
Furaha Isiyo Ya Kukomesha;
Nitamsifu Mwokozi Kwa Rehema Na Pendo
Vilivyo Nipa Pahali Mbingini.

3. Nao Walio Kufa Katika Bwana Yesu,
Nitawaona Tena Huko Juu;
Lakini Nifikapo Kwake Huko Mbinguni,
Nataka Kumwona Mwokozi Kwanza.

4. Milangoni Mwa Mji Bwana Atanipisha,
Pasipo Machozi Awla Huzuni.
Nitauimba Wimbo Wa Milele: Lakini
Nataka Kumwona Mwokozi Kwanza.
(NK # 178) UKINGONI MWA YORDANI
On Jordan’s Stormy Banks

1. Ukingoni Mwa Yordani Ninaangalia
Bara Nzuri Ya Kaanani, Ninayotamani.

Tutakaa Pamoja Na Yesu,
Katika Pwani Yenye Raha;
Tutaimba Wimbo Wa Musa Na Kondoo,
Milele Hata Milele.

2. Bara Ile Ina Nuru, Nuru Ya Milele;
Kristo, Jua, Hutawala, Hufukuza Giza.

3. Nitapafikia Lini Na Kubarikiwa,
Penye Ufalme Wa Baba. Na Kumwona Uso?

4. Furaha Yangu Rohoni Ni Kuchukuliwa;
Siyaogopi Mawimbi Katika Yordani.

(NK # 179) WATAFURAHI
O There’ll Be Joy

1. Wavunaji Watafurahi, Pale Watakapo Rudi,
Wakiyaleta Mavuno Hata Yerusalemu.

Furaha Wataipata, Furaha Hata Milele,
Furaha, Wataipata, Wakati Wa Mavuno.

2. Na Siku Ile Tutaimba, Kumshukuru Na Kumsifu
Bwana Yesu Jumbe Wetu, Kule Yerusalemu.

3. Wavunaji Watafurahi Makaoni Mwa Milele
Yaliyowekwa Tayari Kule Yerusalemi.
(NK # 180) PANA MAHALI PAZURI MNO
There’s A Land

1. Pana Mahali Pazuri Mno,
Twapaona Kwa Mbali Sasa;
Baba Yetu Angoja Pale,
Amepanga Makao Yetu.

Kitambo Tu Bado, Tutakutana Ng’ambo Pale.
Kitambo Tu Bado, Tutakutana Ng’ambo Pale.

2. Tutaimba Pale Kwa Moyo
Nyimbo Tamu Za Wenye Heri.
Na Rohoni Hatutaona
Tena Haja Ya Kupumzika.

3. Kwa Baba Yetu Mkarimu
Tutatoa Shukrani Sana,
Kwa Kipaji Cha Pendo Lake
Na Baraka Anazotupa.

(NK # 181) TUTAKAA MAHALI PA MAJI
We’ll Tarry By The Living Waters

1. Mahali Pa Maji Mazuri Maji Ya Uzima;
Anapotungojea Yesu Tutakaribishwa.

Mahali Pa Maji Mazuri,
Penye Maji Ya Uzima;
Tutakaa Na Mwokozi,
Chemchemi Ya Uzima.

2. Tunapochoka Safarini, Tamu Kupumzika
Panapo Maji Ya Uzima Yatufurahisha.

3. Una Kiu? Uje Kwa Yesu, Utaburudishwa;
Yesu Yu Maji Ya Uzima, Unywe, Uokoke.

(NK # 182) HAPANA GIZA
In The Land Of Fadeless Day

1. Mchana Hauishi Mjini Mzuri;
Mji Hautapita; Na Hapana Giza.

Machozi Yatafutwa, Kifo Hapana Pale;
Hawahesabu Siku-u, Na Hapana Giza.

2. Milango Ni Ya Lulu, Mjini Mzuri;
Dhahabu Njia Zake; Na Hapana Giza.

3. Milango Haifungwi Mjini Mzuri;
Mto Ni Wa Uzima Na Hapana Giza.

4. Hawahitaji Jua Mjini Mzuri;
Mwana Kondoo Nuru; Na Hapana Giza.

(NK # 183) YESU ANAPORUDI
There’ll Be No Dark Valley

1. Furaha Na Raha Tutapa,
Furaha Na Raha Tutapa,
Furaha Na Raha Tutapa,
Yesu Anaporudi.

Yesu Anaporudi (Rudi) Yesu Anaporudi (Rudi);
Furaha Na Raha Tutapa Yesu Anaporudi.

2. Tutaimba Nyimbo Za Shangwe Kuu,
Tutaimba Nyimbo Za Shangwe Kuu,
Tutaimba Nyimbo Za Shangwe Kuu,
Yesu Anaporudi.

3. Hapana Machozi Arudipo,
Hapana Machozi Arudipo,
Hapana Machozi Arudipo,
Kwa Wateule Wake.
(NK # 184) PANAPO PENDO
There Is Beauty All Around

1. Vitu Vyote Ni Sawa, Panapo Pendo;
Kila Sauti Tamu, Panapo Pendo.
Pana Amani Pale, Na Furaha Nyumbani,
Siku Zote Salama. Panapo Pendo.
Panapo Upendo; Siku Zote Salama, Panapo Pendo.

2. Furaha I Nyumbani, Panapo Pendo;
Hapana Machukizo, Panapo Pendo;
Chakula Ni Kitamu, Mashamba Ya Sitawi,
Maisha Ni Kamili, Panapo Pendo.

3. Hata Mbingini Juu, Pana Furaha
Wakiona Upendo Nyumbani Mwetu.
Macho Yanapendezwa Na Viumbe Vya Mungu,
Naye Mungu Huona, Panapo Pendo.

4. Ee Yesu Niwe Wako, Wako Kabisa,
Ndipo Patakuwako Pendo Nyumbani;
Nitakaa Salama, Sitaifanya Dhambi;
Nitabarikiwa Tu Panapo Pendo.
(NK # 185) MUNGU, MAPENZI MAKAMILIFU
O Perfect Love

1. Mungu U Mapenzi Mkamilifu ; Yapitayo Fahamu Za Watu
Twanyenye Kea Sisi Wapungufu,
Wape Baraka Wapenzi Wetu.

2. Ewe Mapenzi Yasiyopimika Twawaombea Kitini Mwako;
Wape Mapenzi Yasiyotindika, Waliooana Mbele Yako.

3. Ewe Uhai, Wewe U Dhamana Ya Imani Na Matumaini,
Wape Kuvumilia Hapa Sana Wasiche Maumivu Mwishoni.

4. Wape Furaha Hiyo Iwezayo Kutia Nuru Kwenye Huzuni,
Wape Amani Hiyo Itakwayo Katika Matata Duniani.

5. Waende Mbele Kusaidiana Maisha Yao Ulimwenguni;
Hata Mwisho, Ni Kuja Kwake Yesu,
Wafurahi Milele Mbinguni.
(NK # 186) HATUTAAGANA TENA
With Friends On Earth

1. Tunapo Na Marafiki Sote Twafurahi,
Ila Tumepaswa Mwishowe Kuagana Tena.

Hatutaagana Tena Nyumbani Mbinguni,
Kwenye Nchi Tamu Juu, Hatutaagana.

2. Twatumaini Kwa Furaha Tutaonana Juu
Na Rafiki Tukioagana Tuishapo Shinda.

3. Kule Hatutatamka Kanwe Neno La Kuagana,
Tutaimba Daima Tena Nyimbo Za Furaha.
(NK # 187) KUFARIKI NAYE YESU
Asleep In Jesus

1. Kufariki Naye Yesu! Usingizi Wenye Heri;
Raha Isifujika Kwa Majonzi Na Adui.

2. Kufariki Naye Yesu! Lo! Ya Kubwaga Simanzi
Na Kulala Na Amani Hata Bwana Awatuze.

3. Kufariki Naye Yesu! Heri Watakaoamshwa,
Wataona Siku Ile Utukufu Wake Bwana.

4. Kufariki Naye Yesu! Watamka Aitapo;
Watapasua Kaburi Na Kutoka Watukufu.
(NK # 188) WIMBI LITAKASALO
O Now I See The Crimson Wave

1. Wimbi La Damu Ya Yesu Linatutakasa;
Aliumba Kusudi Tupate Uzima

Wimbi La Damu Naona Naingia Natakaswa!
Bwana Asifiwe Sana, Hutakasa, Hutakaswa.

2. Damu Inasema Kwamba, Nasikia Mvuto;
Inasema, Moyo Wangu Hutakaswa Nayo.

3. Naondoka Kutembea Kwa Nuru Ya Mbingu;
Mavazi Yamesafishwa; Moyoni Ni Yesu.

4. Neema Ni Ya Ajabu, Kutakaswa Ndani!
Na Kuwa Naye Yesu Tu, Aliye Mwokozi.

(NK # 189) TUBATIZE UPYA
Baptize Us Anew

1. Mimina Upya Nguvu Kutoka Juu;
Tupe Pendo Lako Ewe Mwokozi.

Twakusihi Sana Yesu Mwokozi,
Tubatize Upya, Kwa Roho Leo.

2. Kwako Twalia, Wenye Maovu,
Osha Moyo Wetu, Ututakase.

3. Kipaji Cha Juu, Kitume Kwetu,
Tubariki Sasa, Utufariji.

4. Isikilize, Kwa Moyo Wazi,
Sauti Ya Roho; Ubarikiwe.

(NK # 190) RAHA YANGU YOTE, BWANA
For Ever Here My Rest Shall Be

1. Raha Yangu Yote, Bwana, I Mbavuni Pako;
Mimi Sina Haja Tena Ila Kifo Chako.

2. Mwokozi Uliyekufa, Nawe Ndiwe Mungu,
Kifo Chako Ni Mwako Liwe Fungu Langu.

3. Nioshe Na Niwe Wako,Nawe Uwe Wangu;
Nioshe Damini Mwako Liwe Fungu Langu.

4. Nioshe Si Miguu Tu, Osha Tangu Nyayo,
Hata Kichwa Changu Juu, Na Ndani Ya Moyo,

5. Na Iwe Kafara Damu Nifanypo Kazi,
Hata Imani Itimu, Nikwone, Mwokozi.

(NK # 191) MKATE WA MBINGU
Break Thou The Bread Of Life

1. Mkate Wa Mbinguni Mega Kwetu;
Ulivyotoa Kwa Thenashara.
Katika Kitabu, Twakuona.
Moyo Unatweta Kukutana.

2. Neno La Ukweli, Libariki;
Tusikie Mwito Wa Upole.
Vizuizi Vyote Vitakoma,
Tena Tutapata Uungwana.

3. Uzima Na Nguvu, Utanena;
Nakimbiliza Tu Kufuata.
Lakini Mnyonge Ndiye Mimi:
Naye Mshindaji Ndiye Wewe!

(NK # 192) MWAMBA WENYE IMARA
Rock Of Ages, Cleft For Me

1. Mwamba Wenye Imara Kwako Nitajificha!
Maji Hayo Na Damu Yaliyotoka Humu,
Hinisafi Na Dhambi, Hunifanya Mshindi.

2. Kwa Kazi Zote Pia Sitimizi Sheria.
Nijapo Fanya Bidii, Nikilia Na Kudhii,
Hayaishi Makosa; Ndiwe Wa Kuokoa.

3. Sina Cha Mkononi, Naja Msalabani;
Nili Tupu, Nivike; Ni Mnyonge, Nishike;
Nili Mchafu Naja, Nioshe Ni Sijafa.

4. Nikungojapo Chini, Na Kwenda Kaburini;
Nipaapo Mbinguni, Na Kukwona Enzini,
Roho Yangu Na Iwe Rahani Mwako Wewe.
(NK # 193) SAUTI YAKE MCHUNGAJI
Hark! ’Tis The Shephered’s Voice

1. Sauti Ya Mchungaji, Ninasikia Jangwani,
Kondoo Waliopotea Anawaita Warudi.

Leteni, Leteni, Leteni Toka Dhambini;
Leteni, Leteni, Waleteni Kwa Yesu.

2. Nani Atakeyekwenda Amsaidie Mchungaji,
Awarudishe Zizini, Wasife Bure Gizani?

3. Usikose Kusikia Sauti Ya Mchungaji,
“Kondoo Waliopotea Nenda Na Kuwatafuta.”
(NK # 194) TWAOMBA BARAKA ZAKO
1. Twaomba, Bwana, Umpokee Kama Mhudumu;
Ambaye Anajitoa Kuwa Mtumishi.

2. Twaomba, Bwana, Umpokee Kama Mhudumu;
Neno Lako Alitoe, Mwangaza Kung’aa.

3. Mwokozi Wetu, Twaomba, Na Umwandikie
Kitabuni Mwako Juu Mjumbe Wa Injili.

4. Silaha Zake Apewe Kumshinda Adui;
Vitani Awe Hodari, Mpaka Mauti.

5. Yeye Ashindaye, Bwana Kwa Rehema Yako,
Ile Taji Ya Dhahabu, Nawe Utampa.

(NK # 195) MSINGI WA KANISA
The Church Has One Foundation

1. Msingi Wa Kanisa Ndiye Yesu Bwana;
Kiumbe Chake Kipya, Akipenda Sana;
Kutaka’ Kitafuta, Alishuka Chini,
Naye Kwa Haja Yake, Akafa Mtini.

2. Lina Kila Kabila Kisha Ndiyo Moja
Wokovu Wake Una Mwokozi Mmoja;
Uzazi Ni Umoja, Moja Tumaini.
Chakula Ni Kimoja, Moja Tumaini.

3. Watu Hustaajabu Kwa Mashaka Yote
Yaipatayo Nje Hata Ndani Mwote;
Ila Watakatifu Humwomba, Wakikesha
Usiku Ni Kilio, Asubuhi Raha.

4. Mashaka Na Taabu Hata Vita Vyake,
Vyangoja Matimizo Ya Amani Yake,
Ndipo Kwa Macho Yetu Twone Utukufu
Kanisa Ya Kushinda Itastarehe Juu.

(NK # 196) VITO VYA THAMANI
When He Cometh

1. Kitambo Bwana Yuaja, Atafute Kote
Vito Vya Thamani Kubwa: Mali Yake Kuu.

Kama Nyota Tajini Vitang’aa Sana,
Vito Vizuri Kweli Vyenye Thamani.

2. Karibu Atakusanya Vito Kwa Ufalme,
Vizuri Vinavyong’aa: Mali Yake Kuu.

3. Watoto Wote Wadogo Wampendao Yesu,
Ndiyo Vito Ving’aavyo: Mali Yake Kuu,

 

(NK # 197) ANIPENDA NI KWELI
Jesus Loves Me

1. Anipenda Ni Kweli: Mungu Anena Hili;
Sisi Wake Watoto Kutulinda Si Zito.

Yesu Mwokozi Ananipenda;
Kweli Hupenda, Mungu Amesema.

2. Kwa Kupenda Akafa Niokoke Na Kufa:
Atazisafi Taka Sana Ataniweka.

3. Anipenda Kabisa; Niuguapo Sasa,
Anitunza Mbinguni Niliyelala Chini.

4. Kunipenda Haachi Tu Sote Hapa Chini,
Baada Ya Mashaka Kwake Tanipeleka.

(NK # 198) KAZA SANA MACHO
I Washed My Hands

1. Nilinawa Mikono Safi Asubuhi,
Itende Kazi Kutwa Kwa Yesu Mwokozi.

Kaza Sana Macho Njiani Kote,
Utende Kwa Yesu Kazi Njema Tu.

2. Natega Masikio Nitambue Wasaa,
Mikono Na Itende Upole Daima.

3. Macho Yangu Yachunga Mikono Kazini;
Ilindwe Maovuni Impendeze Yesu.
(NK # 199) UPENDO NI FURAHA
’Tis Love That Makes Us Happy

1. Upendo Ni Furaha, Ni Kweli Desturi
Yake Kuzisahihisha Njia Zetu Zote.

Yu Pendo: Tu Watoto Wake.
Yu Pendo, Mwana Wa Mungu!
Na Sisi Tupendane Kama Baba Mungu.
Amri Yake Ndiyo Hii, Kupendana Sana.

2. Duniani Huzuni, Ugonjwa, Mauti,
Kwa Pendo Tuwafariji Wenye Mahitaji.

3. Na Atakapokuja Kutuchukua Juu,
Tutaimbia Milele Pendo Lake Yesu.

(NK # 200) BABA YETU ALIYE MBINGUNI
I Am So Glad That Our Father In Heaven

1. Baba Yetu Aliye Mbinguni,
Amenifurahisha Yakini;
Kuniambia Mwake Chuoni,
Ya Kuwa Nami Yesu Pendoni.

Anipenda Mwokozi Yesu, Anipenda, Anipenda:
Anipenda, Mwokozi Yesu, Anipenda Mimi.

2. Nimuachapo Kutanga Mbali,
Yeye Yu Vivyo, Hupenda Kweli:
Hunirejeza Kwake Moyoni,
Kweli Yu Nami Yesu Pendoni.

3. Anipenda! Nami Ninampenda,
Kwa Wokovu Alionitenda;
Akanifilia Msalabani,
Kwa Kuwa Nami Yesu Pendoni.

(NK # 201) HUNIPENDA PIA.
He Loves Me, Too

1. Mungu Huona Videge Wanaoanguka;
Akiwapenda Videge,Vile Hunipenda.

Hunipenda, Hunipenda, Pia;
Najua Ananipenda Niliye Mdogo.

2. Rangi Ya Namna Nzuri Upamba Maua;
Akiyapenda Maua, Vile Unipenda.

3. Mungu Aliyeviumba Videge, Maua,
Atasahau Watoto Kweli Huwapenda.

(NK # 202) SIKIA MLIO
Hear The Pennies Dropping

1. Sikia Mlio! Pesa Koponi
Zinalialia—Zote Kwa Yesu.

Kuanguka Kuanguka Pesa Koponi,
Kila Moja Kwako, Yesu Zipokee.

2. Huanguka Pesa Toka Mikononi:
Sadaka Kwa Yesu Ya Kundi Dogo.

3. Tulio Wadogo Tuna Haba Tu;
Tuishapo Kuwa Pendo ’Tazidi.

4. Wenye Mali Chache Tumpe Moyo;
Kwa Furaha Tupu Atakubali.

(NK # 203) YA SABA NI KWA YESU
The Seventh Day Is For Jesus

1. Siku Sita Fanya Kazi, Ya Saba Ni Kwa Yesu.
Hapo Tunapo Pumzika, Kwani Ni Yake Yesu.

Moja, Mbili, Tatu, Nne, Tano, Sita, Zote Kwetu;
Lakini Tutakumbuka, Ya Saba Ni Kwa Yesu.

2. Huonyesha Ya Kufanya, Kwa Kuwa Ni Ya Yesu,
Na Atuonyesha Njia, Tutamfuata Yesu.

3. Tuombe Kila Sabato, Na Kujifunza Kwake;
Tutamtii Daima, Tutakaa Na Yesu.

(NK # 204) KUWA NA YESU NYUMBANI
Happy, Happy, Home

1. Kuwa Na Yesu Nyumbani,
Furaha Nyingi, Furaha Nyingi, Furaha Nyingi.
Kuwa Na Yesu Nyumbani,
Furaha Nyingi, Furaha Nyingi,

2. Yesu Yu Ndani Ya Baba,
Nyumba Salama, Nyumba Salama, Nyumba Salama;
Yesu Yu Ndani Ya Baba.
Nyumba Salama, Nyumba Salama.

3. Yesu Yu Ndani Ya Mama . . .
Nyumba Salama, Nyumba Salama, Nyumba Salama;
Yesu Yu Ndani Ya Mama.
Nyumba Salama, Nyumba Salama.

4. Yesu Ndani Ya Watoto . . . .
Nyumba Salama, Nyumba Salama, Nyumba Salama;
Yesu Ndani Ya Watoto
Nyumba Salama, Nyumba Salama.

(NK # 205) MSIFU MUNGU EE WATOTO
Praise Him, Praise Him

1. Msifu Mungu, Ee Watoto Wote,
Yu Pendo, Yu Pendo;
Msifu, Msifu, Ee Watoto Wote
Mungu Ni Upendo.

2. Tunampenda, Ee Watoto Wote,
Yu Pendo, Yu Pendo,
Tunampenda, Ee Watoto Wote
Mungu Ni Upendo.

3. Tumikeni, Ee Watoto Wote.
Yu Pendo, Yu Pendo,
Tumikeni, Ee Watoto Wote
Mungu Ni Upendo.

(NK # 206) MWOKOZI WANGU ANIPENDA
Now I Belong To Jesus

1. Mwokozi Wangu Alinipenda,
Maovu Ayanitengi Naye,
Alijitoa, Kuniponya,
Sasa Mimi Wake.

Mimi Wake Kabisa, Naye Yesu Wangu,
Si Kwa Wakati Huu Tu, Bali Na Milele.

2. Dhambi Nilijidhili Sana,
Yesu Akaja Kunikomboa,
Akanitoa Sumbukoni,
Sasa Mimi Wake.

3. Furaha Nyingi Moyoni Mwangu,
Bwana Yesu Kunifanya Huru,
Kunitwaa Kwa Damu Yake,
Sasa Mimi Wake.

(NK # 207) NANI AFANYA MAUA
Who Makes The Flowers

1. Nani Ayafanya Maua, Maua,
Nani Ayafanya—Mungu Juu.

2. Nani Apambaye Machweo, Machweo,
Nani Ayapamba—Ni Mungu.

3. Nani Afanya Theluji, Theluji,
Nani Aifanya—Ni Mungu.

(NK # 208) MUNGU AFANYA UPINDE
The Rainbow

1. Nani Afanya Upinde,
Namjua, Namjua
Mungu Afanya Upindi
Nampenda Kwa Hiyo.

2. Mungu Atuma Upindi
Ni Bora Mweupe,
Mungu Atuma Upindi,
Kwamba Yu Karibu.
(NK # 209) NAPENDA SANA KIFIKA
I Love To Come To Sabbath School

1. Napenda Sana Kufika, Skuli Ya Sabato
Napenda Sana Kufika, Siku Ya Sabato

2. Napenda Sana Kuimba, Habari Za Yesu,
Napenda Sana Kuimba, Siku Ya Sabato.

3. Napenda Sana Kutoa, Sadaka Kwa Yesu,
Napenda Sana Kutoa, Siku Ya Sabato.

4. Napenda Sana Kuomba, Kwa Yesu, Kwa Yesu,
Napenda Sana Kuomba, Siku Ya Sabato.

5. Napenda Sana Kujua, Maneno Ya Yesu,
Napenda Sana Kujua, Siku Ya Sabato.

6. Napenda Sana Kusema, Fungu La Kukariri,
Napenda Sana Kusema, Siku Ya Sabato.

(NK # 210) Maitikio
ROHO WA MUNGU WANGU
Spirit Of The Living God

Roho Wa Mungu Wangu, Nakuhitaji!
Roho Wa Mungu Wangu, Nakuhitaji!
U-ni-linde, U-ni-jaze;
Roho Wa Mungu Wangu, Nakuhitaji!
(NK # 211) MOYONI
Into My Heart

Moyoni, Moyoni; Ingia Moyoni, Yesu.
Njoo Leo, Njoo Kukaa, Ingia Moyoni Bwana.
Moyoni, Moyoni, Angaza Moyoni Yesu,
Ng’aa Leo Siku Zote, Angaza Moyoni Bwana.

(NK # 212) MTAZAME MWOKOZI
(Turn Your Eyes Upon Jesus)

Mtazame Mwokozi,
Usoni Mwake Mzuri,
Mambo Ya Dunia Hugeuka,
Usowake Tukiuona.

(NK # 213) NIWE NAO UZURI WA MWOKOZI
(Let The Beauty Of Jesus)

Niwe Nao Uzuri Wa Mwokozi,
Nazo Huruma Zake Na Usafi,
Roho Mtakatifu Anibadilishe,
Aonekane Yesu Ndani Yangu.

(NK # 214) NATAKA NIWE TAYARI
(I Want To Be Ready When Jesus Comes)

Nataka Niwe Tayari, Bwana,
Nataka Niwe Tayari, Bwana,
Furaha Za Ulimwengu Ni Bure;
Nilinde Hata Uje!

(NK # 215) ULIMWENGU WATAKA
(What The World Needs Is Jesus)

Ulimwengu Wataka Kumwona Yesu;
Ulimwengu Wataka Kumwona Yesu.
Analeta Furaha, Shangilio Kutosha,
Ulimwengu Wataka Kumwona Yesu.

(NK # 216) MOYONI ’NIJAZE
(With Thy Spirit Fill Me)

Moyoni ’Nijaze,
Na Roho Wa Yesu;
Nataka Kujitoa,
Moyoni ’Nijaze.

(NK # 217) OMBA SANA ASUBUHI
(Whisper A Prayer In The Morning)

1. Omba Sana Asubuhi,
Omba Sana Mchana,
Omba Sana Na Jioni,
Bwana Hutusikia.

2. Mungu Hujibu Maombi,
Asubuhi Na Mchana,
Hata Hutungojea Tena,
Wakati Wa Jioni.

3. Na Tuimbe Asubuhi.
Tena Saa Za Mchana.
Hivi Tutafurahi Naye.
Pumziko La Jioni.

(NK # 218) YESU MWOKOZI MPENDWA
(Wonderful, Wonderful Jesus)

Yesu Mwokozi Mpendwa.
Hakuna Mwingine!
Yesu Mwokozi Mpendwa,
Yesu Mwokozi Mpendwa,
Nakutazama Wewe Pekee,
Yesu Mwokozi Mpendwa,
Ninakutafuta;
Wewe U Mali Yangu.
Sasa Na Milele.
(NK # 219) PAMBAZUKA NURU
(There’s A New Day Dawning)

Pambazuka Nuru,
Siku Mpya Yaja,
Basi Amkeni Na Kuimba,
Ninyi Nyote!
Pambazuka Nuru,
Siku Mpya Yaja,
Yesu Atakaporudi Kama Mfalme!

(NK # 220) KWA HERI
(Goodbye Chorus)

Kwa Heri, Mungu Awalinde;
Kwa Heri, Na Awaongoze;
Kwa Heri, Na Kuwapa Amani,
Bwana Awabariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published.