5/17/2017

mm


Advocate Kinja

Mfalme wa amani Mungu mwenye nguvu, wewe unaetawala milele zote, jina lako na litukuzwe milele na milele.

Unastahili sifa, heshima na utukufu ni vyako Bwana. Tunasema asante kwa namna unavyotupenda upeo, tusamehe dhambi zetu zikiwa za wazi au za siri tusamehe Mungu wetu. Baba wewe watujua sisi ni dhaifu tutie nguvu, tupatie tumaini jipya maishani mwetu tuendelee kukutumainia.

Baba sisi tu wagonjwa wa kiroho na kimwili, yule mwovu ameteka akili zetu hivyo hatusomi maandiko matakatifu, tumekua vipofu hata tucjue hatari iliyo mbele yetu, tunakuomba kwa njia ya Roho wako Mtakatifu akatuponye atupatie dawa ya macho tupate kuona hatari inayotujia mbele yetu. Fumbua macho yetu ya kiroho Bwana kwa uwezo wetu hatuwezi bali ni kwa uwezo wa kimbingu tu.

Wapo wagonjwa, tunawaleta kwako ucku huu, yule mama anaesafirishwa kesho kwenda India tunamuweka mikononi mwako wewe uliye tabibu mkuu wewe unajua ugonjwa wako kwa karidi ya mapenzi yako safari yake ya kwenda kwenye matibabu ikawe yenye mafanikio makubwa, na kila jambo litendeke kwa utukufu wa jina lako.

Wapo wagonjwa wengine Baba, hawa nao tunawaleta kwako maana wewe tu ndiye uwezaye yale yacyowezekana waponye kwa naradhi yao wakutukuze wewe Mungu wa mbinguni.

Baba yetu wa mbinguni, kundi hili linayo mipango ya uinjilisti ktk eneo la bunda, tunakuomba timiza njozi hii kwa utukufu wa jina lako. Hivyo Baba tunaleta kwako bajeti yetu ya sh 15 milioni kupata vyombo vya muziki (sauti) na kwakua kazi hii ni yako nasi umetuachia jukumu hili lkn ulisema tuombe neno lolote kwa jina lako nawe utafanya, tunakusihi tenda kwa utukufu wa jina lako na watu wa eneo lile wakaickie sauti ikisihi ndani ya mioyo yao wakugeukie wewe Mungu wa mbinguni.

Kati yetu wapo wajane, wagane, yatima, wahitaji na waliokata tamaa, makundi yote haya nayaleta kwako, wewe ambae ni muweza wa yote, ikiwa ni faraja itapatikana kwako ikiwa ni tumaini, wewe ndie tumaini la vizazi vyote. Watie nguvu waliochoka na kukata tamaa. Roho wako Mtakatifu awe kati yao akisema nao kwa pendo akiwatazamisha kwako.

Bariki familia zetu, ndoa changa na hata zile za zamani yumkini wanapitia Changamoto maishani wewe ukawe mtatuzi wa Changamoto hizo na jina lako likasikike likitajwa mara zote ktk familia hizi. Walio na wachumba imarisha uchumba wao, wanaotafita wenzi wapatie wa kufanana nao kwa utukufu wa jina lako.

Mfalme wa amani bariki vipato vyetu ikiwa ni biashara au kule maoficn utubariki Bwana tulitukuze jina lako.

Mungu wa mbinguni uctuache yatima, kaa nasi nyakati zote tunakuhitaji sana maishani mwetu, tunapojumuika km wanasauti ya injili tupatie njozi ya kufanya kazi yako. Hata Sasa tunapokua na mpango wa kupanga cku za kufunga na kuomba tunakuomba tawala fikra na mawazo yetu tuwaze yaliyo mapenzi yako.

Lkn Baba tunapokaribia mwisho wa wakati tusaidie kusalimisha nia na nafsi zetu kwako nawe utufinyange tufae kuingia na kuurithi uzima wa milele uliowaandalia wale uwapendao.

Tunaamini utakua pamoja nasi kwani tumeomba kupitia jina la Yesu Kristo aliye Bwana mwokozi wetu amina.