5/16/2016

MAOMBI YA ASUBUHI (Jumatatu  5/15/16)

 1. Saa 11-12 (Maombi ya binafsi/ Nyimbo za Injili)
 2. Saa 12-1 (Maombi ya Jumla kama Familia ya Sauti Ya Injili)
 3. Mada Ya Leo = TOBA, UNGAMO, MSAMA 

 

SIFA & SHUKRANI: Mshukuru MUNGU kwa:

 1. Baraka tele & uaminifu wake kwetu
 2. Tabia yake isiyobadilika
 3. Msamaha wa dhambi zetu
 4. Nafasi nyingine ya Uhai Leo.

WAGONJWA WETU

 1. Sisi sote tu wagonjwa wa kiroho, hivyo tuombee ili Tabibu Mkuu atuponye

CHANGAMOTO ZINGINE

Dada Mercy Swai:-

 • Yeye alikuwa amelazwa ila sasa ameisharuhusiwa yupo nyumbani..
 • ingawa bado anaendelea na matibabu..
 • tuzidi kumuombea.

Dada Tatu Mkomagi:-

 • Yeye bado amelazwa Katika hospitali ya Ocean Road
 • kutokana kugundulika ana tatzo la blood cancer,,
 • kwa neema ya Mungu Siku ya Jumanne atasafiri kwenda India kama hakutakuwa na kikwazo chochote..

KAMPENI ZA UINJILISTI (Evangelistic Campaign)

 1. Bunda (June/ July 2016)

USHUHUDA WA LEO

Bwana amejipatia Roho  20 tena katika mkutano mkuu wa Sauti Ya Injili huko Bunda –Tanzania, ikiendesha na mch. Elly Mshitu. Tuwaombee.

 

AHADI YA LEO: –  (Yohan 14:1-3)

 1. 1 Msifadhaike mioyoni mwenu; mnamwamini Mungu, niaminini na mimi.
 2. 2 Nyumbani mwa Baba yangu mna makao mengi; kama sivyo, ningaliwaambia; maana naenda kuwaandalia mahali.
 3. 3 Basi mimi nikienda na kuwaandalia mahali, nitakuja tena niwakaribishe kwangu; ili nilipo mimi, nanyi mwepo.

TUNAKARIBISHWA KUFANYA YAFUATAYO:

 1. Kutoa ushuhuda wa Matendo makuu ya MUNGU
 2. Kuweka Audios za Maombi (Sauti), ama Kuandika.
 3. Kutujulisha kama OMBI LAKO limejibiwa (ili tupunguze list)
 4. Kushiriki katika kipindi kingine cha Maombi Ya Jioni (Saa 3 Usiku)

Karibuni katika CHUMBA CHA MAOMBI ili tushiriki ibada ya maombi pamoja.

Ombi limetolowa na ndg. Adocate Kinja

Uhimidiwe Baba yetu muumba wa mbingu na nchi, bahari na chemchem za maji, viumbe vinavyoonekana na vusivyoonekana, jina lako litukuzwe sana.

Tunakushukuru sana, kwa Rehema zako na upendo wako mwingi, hatukustahili lkn kwa huruma zako bado umetupatia nafac nyingine ya kuwepo hai muda huu, asante Yesu.

Wapo ndugu, rafiki na jamaa nao walitamani kuwepo masaa haya lkn wamelala ucngizi wa mauti, hivyo Bwana tuwezeshe kwa Roho wako Mtakatifu tuweze kufanya matengenezo ya kweli ili hata mauti yanapotukuta tuwe tumengeneza uhusiano wetu nawe.

Lkn Baba, tunakuomba tusamehe dhambi na makosa yetu, na kwakua watujua sisi ni wadhaifu tupatie nguvu ya kimbingu nguvu ya roho mtakatifu atuwezeshe kutenda na kuenenda sawa na sheria yako takatifu, na maisha yetu yaakisi tabia yako na kwa namna hiyo tukawe nuru kwa mataifu, nao wakuone wewe Yesu kupitia mienendo ya maisha yetu.

Baba, tunakushuru kwa kundi kubwa la watu ambao wameamua kukufuata wewe baada ya kuusikia ujumbe wako kupitia mtumishi wako mchungaji Elly, Baba wa mbingu kundi hili tunaliweka mikononi mwako, wewe ndiwe mchungaji mwema ambae huwaacha wale 99 na kwenda kumtafuta mmoja aliyepotea, nakuomba kundi hili ukalichunge acpotee hata mmoja kati yao, kwa maana ulishuka kutoka mbinguni ukaja ukafa pale msalabani kwa ajili ya hawa waliojitoa na kubatizwa. Ninakuomba kwakua umeahidi kuonyesha njia pasipo na njia, ongoza kundi hili, kila wanapokuita ktk haja na shida za mioyo yao jibu kwa kadiri ya mapenzi yako kwa utukufu wa jina lako.

Wapo wagonjwa tunawaleta kwako wewe uliye tavibu mkuu, yule mama mwenye saratani ya damu, hivi karibuni wanamsafirisha mpk India, lkn Yesu tunaamini kwa hakika uwezo wakibinadamu unapoushia ndipo unapojidhihisha ili wajue kua wewe ni Mungu wa yasiyowezekana, Baba ninakuomba ikiwa ni mapenzi yako tenda jambo la pekee sana kwa mama yule kwa utukufu wa jina lako, na kwakua tumekutumaini wewe. Lkn km utapenda aende India, kwa uwezo wa kimbingu waende na warudi na hatimae uponyaji uwezejane.

Tunakushukuru kwa yule mama ambae ameruhusiwa kule hospital lkn bado afya yake haijakaa sawa, baba endelea kumtibu cku kwa cku afya yake ikaimarike na jina lako litukuzwe. Na yule mwingine ambae bado amelazwa naye ucmpite ucku huu, maana wewe ndie tumaini letu pekee.

Baba yangu wa mbinguni bariki hali zetu za kiuchumi ktk familia zetu na hata kwa MTU mmoja mmoja ili tuweze kukidhi mahitaji ya familia na kukurudishia zaka na sadaka.

Tunamuombea mchungaji Elly Mshitu kwa kazi ya kule bunda endelea kumtumia km chombo kufanya kazi, na popote utakapomuagiza aende ili kuokoa Roho ulizoziandaa kwa ajili ya uzima wa milele. Acje akajisifu na kujiinua bali akutujuze wewe Mungu wa mbinguni. Wapo wachungaji wengine humu ktk group hili nao kwa ujumla wao nawaleta kwako wabariki maana wameamua kukutumikia, bariki utumishi wao, wapatie njozi za kufanya kazi yako ili habari njema iufikie ulimwengu wote hatimae uje utuchukue Bwana. Wanapoendelea kutupatia masomo na ushauri ooooh Yesu Roho wako awapatie hekima ktk kutuonya ili tuyaishi maandiko yako matakatifu.

Sasa Baba, tunaini tunapita tuandae kwa ajili ya ujio wako mara ya pili, ombi letu kwa kila mmoja liwe, Bwana utukumbuke ktk ufalme wako ujapo mara ya pili.

Tunaomba haya kupitia jina la Yesu Kristo aliye Bwana na mwokozi wetu. amina.