Usimuache Yesu kwa Sababu ya Changamoto

USIJIKINAI KWA KUWA CHANGAMOTO ZIMEKUFIKA.
- Jitie nguvu, Mshukuru Mungu
- Jisamehe, Samehe waliokuumiza.
- Kumbuka Mungu alipokutoa na Alivyokupigania wakati Ule.
- Usimuache Yesu kwa Sababu ya Changamoto.
- Wala Usipoteze Heshima Uliyonayo kwa Sababu ya Sauti ya Adui.
JIAMBIE NAFSI YAKO KUWA
- Mimi ni Wathamani kuliko Chochote kionekanacho kwa Macho ya Nyama.
TUBU KWA MUNGU WAKO
- Kisha Tangazia Watu Waliokuumiza Msamaha.
- Jitiishe chini ya Mkono wa Mungu wako Kumtaka Mungu Nguvu zake Maishani mwako.
MUNGU HASHINDWI KWA CHOCHOTE.
- Unapofungwa Mlango mmoja Haimaanishi Hawezi Kukufungulia Mlango Mwingine wa Kutokea.
YEYE AMESEMA
- Anatuwazia Mawazo ya Amani,
- Ndiye Aliyeahidi Kutupigania Ili tufanywe Washindi kwa Utukufu wake.
NDIYO MAANA AKASEMA
- Yeye ni Adui wa Adui Zetu
- Mwache Mungu Ashughulike na Magumu yako
- Acha Kutumia Akili zako Utaumia Sana.
NDIYE MUWEZA WA YOTE
- Yeye Aitazamae Kesho Yetu Ni Mungu Muweza Wa Yoote.
- Jitie Nguvu Ktk Kuachilia Yanayokuumiza,
- Usimkimbie Mungu Kwakua Hujaona Majibu,
- Au Kwakua Uliyoyatarajia Hayajawa.
KUMBUKA
- Mungu Ni Wa Majira Na Nyakati
- NA Kwa Wakati Sahihi Atafanya Hata Usiyoyatarajia.
NAKUPENDA RAFIKI LAKIN YESU ANAKUPENDA ZAIDI YANGU.
Kwa hivyo:
- Dumu Kaitaka Maombi