Batimayo Kipofu

KESHA LA ASUBUHI

Ijumaa: 29/04/2016

SOMO : IMANI YA KIPOFU BARTIMAYO KATIKA NEEMA YA MUNGU YATUZWA

Yesu akamjibu, akamwambia, Wataka nikufanyie nini? Yule kipofu akamwambia, Mwalimu wangu, nataka nipate kuona”. Marko 10:51.

 • Ni pale tu mwenye dhambi anapojisikia hitaji la Mwokozi, ndipo moyo wake unapomwelekea yeye aliye na uwezo wa kumsaidia.
  • Yesu alipotembea kati ya watu, wagonjwa ndio waliohitaji tabibu.
  • Maskini, walio na huzuni na walio katika dhiki, walimfuata yeye,
  • ili kupata msaada na faraja ambayo wasingeweza kuipata pengine popote.
 • Kipofu Bartimayo alisubiri kando ya njia; alisubiri muda mrefu ili kukutana na Kristo.
 • Umati wa watu wenye uwezo mzuri wa kuona wakipita pita, lakini hawakuwa na shauku ya kumwona Yesu. Mtazamo mmoja tu wa imani ungegusa moyo wake wa upendo na kuwaletea baraka za neema yake; lakini hawakujua ugonjwa na umaskini wa roho zao, pia hawakujisikia kuwa na hitaji lolote la Kristo.
 • Haikuwa hivyo kwa yule maskini kipofu.
  • Tumaini lake la pekee lilikuwa katika Yesu.
  • Alipokuwa akingoja na kukesha, alisikia vishindo vya miguu mingi ndipo alipohoji kwa shauku, “Kelele ya wasafiri wengi hivi inamaanisha nini?”
 • Wale walioketi karibu naye wakajibu kwamba, “Yesu Mnazareti anapita.”
 • Akiwa na shauku iliyotokana na hamu kubwa, alipaza sauti yake, “Mwana wa Daudi, Yesu, unirehemu!”
 • Walijaribu kumnyamazisha, lakini ndipo akapaza sauti kwa nguvu zaidi, “Mwana wa Daudi, unirehemu!”

OMBI HILI LIKASIKIWA.

 • Imani yake yenye kustahimili ikatuzwa.
 • Hakurejeshewa uwezo wake wa kuona tu, bali pia macho yake ya ufahamu yalifunguliwa.
 • Katika Kristo akamwona Mkombozi wake na Jua la Haki likang’aa rohoni mwake.
 • Wale wote wanaojisikia kumhitaji Kristo kama alivyokuwa kipofu Bartimayo na kuwa na ari na kudhamiria kama alivyokuwa, watapokea baraka wanazotamani kama yeye alivyopokea.
 • Waliokuwa na huzuni, walioteseka ambao walimtafuta Kristo kama msaada wao, walichangamshwa na ukamilifu wa Mungu, uzuri wa utakatifu, ambavyo viling’aa katika tabia yake.

Wale watakaompokea Kristo kwa imani, watapokea pia nguvu ya kufanyika wana wa Mungu.

MUNGU NA AFANYE UPYA TABIA ZETU


 

DONDOO MUHIMU KATIKA SOMO:

Je, ni sababu gani iliyofanya imani ya Batimayo kipofu kuzawadiwa?

 • “Shauku ya kumwona Yesu.”
 • “Tumaini lake pekee liko kwa Yesu.”
 • Alijiona kuwa mhitaji, akamweleza Mwokozi haja yake.
 • “Ni pale tu mdhambi anapohisi hitaji la Mwokozi, ndipo moyo wake unapomwendea Yule awezaye kumsaidi.”
 • “Batimayo kipofu…amekuwa akingojea kwa muda mrefu ili kukutana na Kristo.”
 • Alitambua “ugonjwa na umaskini” wa roho yake.

Tunaweza kujifunza nini kutokana na mwujiza huu wa kushangaza?

 • “Wote wanaojisikia kumhitaji Kristo kama ilivyokuwa kwa Batimayo kipofu, na wataokuwa na juhudi na kusudio la dhati kama alilokuwa nalo, watapokea baraka wanazozitamani sana, kama yeye alivyopokea.”

Batimayo kipofu

 1. Batimayo kipofu alitambua shida yake—alikuwa kipofu (Marko 2:17).
 2. Alikuwa na hitaji/shauku la dhati moyoni mwake—alitaka kupona.
 3. Alikwenda mahali husika—alimtafuta Yesu, alikwenda mahali ambapo Yesu angelipitia.
 4. Aliwaulizia watu wengine (wasafiri, wapitaji)—alitumia kila njia iliyowezekana.
 5. Hakuruhusu chochote kimzuie kupata uponyaji— (Marko 10:48),
  1. walipotaka kumnyamazisha kwa kumkemea…
  2. alipaza sauti na kupiga kelele hata zaidi!
 6. Alimweleza Yesu hitaji lake— Mithali 28:13.
  1. Afichaye Dhambi Zake Hatafanikiwa;
  2. Bali Yeye Aziungamaye Na Kuziacha Atapata Rehema.
 7. Aliamini nguvu za uponyaji kutoka kwa Yesu:
  1. Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza…Mungu” (Waebrania 11:6).
  2. Hakurejeshewa uwezo wake wa kuona tu, bali pia macho yake ya ufahamu

 

Rejea Mafungu Yafuatayo

Yohana 9:41;

 • 40 Basi Wale Wasamaria Walipomwendea, Walimsihi Akae Kwao; Naye Akakaa Huko Siku Mbili.
 • 41 Watu Wengi Zaidi Wakaamini Kwa Sababu Ya Neno Lake.

 

Ufunuo 3:15-18;

 • 15 Nayajua matendo yako, ya kuwa hu baridi wala hu moto; ingekuwa heri kama ungekuwa baridi au moto.
 • 16 Basi, kwa sababu una uvuguvugu, wala hu baridi wala moto, nitakutapika utoke katika kinywa changu.
 • 17 Kwa kuwa wasema, Mimi ni tajiri, nimejitajirisha, wala sina haja ya kitu; nawe hujui ya kuwa wewe u mnyonge, na mwenye mashaka, na maskini, na kipofu, na uchi.
 • 18 Nakupa shauri, ununue kwangu dhahabu iliyosafishwa kwa moto, upate kuwa tajiri, na mavazi meupe upate kuvaa, aibu ya uchi wako isionekane, na dawa ya macho ya kujipaka macho yako, upate kuona.