Tofauti kati ya Mahusiano na Ndoa.

[2:18 AM, 4/29/2016] Tajieli Panga: Habari za Leo wapendwa….?
[2:20 AM, 4/29/2016] Tajieli Panga: Samahani sana kwa kutokuwepo kwa mda katika familia hii. Ni kwasababu ya mambo yaliyokuwa juu ya uwezo wangu. But I thank God I’m back. Tuzidi kuombeana
[2:21 AM, 4/29/2016] Tajieli Panga: Naomba Leo tujadili kidogo mada ya kaya na familia.

Karibuni sana.
[2:21 AM, 4/29/2016] Tajieli Panga: Mmoja atupe ombi tuanze mada yetu
[2:29 AM, 4/29/2016] +255 653 848 877: Baba ktk jina lako takatifu kapokee maombi yetu mfalme wa amani ikambariki kila atakaye kwenda kishiriki 🙏
[2:30 AM, 4/29/2016] +255 653 848 877: Karibu kwa maombi
[2:31 AM, 4/29/2016] +255 766 893 582: Tofauti kati ya Mahusiano na Ndoa.

Katika darasa la Saikolojia, mwanafunzi alimuuliza professor nini maana ya mahusiano ya kimapenzi? Professor akasema “ili niweze kukujibu swali lako nenda kwenye shamba kubwa la ngano na uchague mche wa ngano ulio mkubwa kuliko miche yote katika hilo shamba.

Kisha urudi nao hapa kipindi kitakachokuja. Ila sheria ni kwamba unapotafuta huo mche mkubwa kuliko yote katika hilo shamba huruhusiwi kurudi nyuma kutizama tena.

Mwanafunzi wa Saikolojia akaenda shambani na kuanza kutafuta mche mkubwa kuliko yote, alipopita tuta la kwanza aliona mche mkubwa lakini akajisemea kwamba niende tuta la pili labda huko kuna mkubwa zaidi, akenda tuta la pili nako akaona mche mkubwa, lakini akajisemesha vile vile kwamba huenda kuna mkubwa zaidi tuta la tatu, akendelea mpaka akaona kwamba matuta mengine yote yanayofuata yana miche midogo zaidi bora ya matuta ya nyuma.

Akajilaumu kukosa mche wa ngano katika matuta ya nyuma na hivyo akarudi darasani kwa Professor mikono mitupu. Professor akamwambia “hiyo ndio maana ya mahusiano, unakazana kutafuta yule aliye bora na amekamilika, lakini baadae unakuja kutambua kuwa ulipoteza mtu bora zaidi katika huo mchakato wako.”

“Kwaio ndoa ni nini?” Mwanafunzi akamuuliza tena professor. Mwalimu akamwambia “ili niweze kukujibu swali lako, nenda katika shamba la mahindi na uchague mmea wa mahindi mkubwa kuliko yote katika shamba na urudi hapa, ila sheria ni ile ile huruhusiwi kurudi nyuma kuchukua yale uliyoyapitia”

Mwanafunzi akaenda katika shamba la mahindi, ila safari hii alikuwa muangalifu kutokurudia kosa la mwanzo, alipofika katikati ya shamba akachagua mmea wa mahindi ambao upo saizi ya kati ambao aliona unaridhisha na akarudi nao kwa mwalimu.

Professor alipomuona akamwambia, “safari hii umeleta mmea wa mahindi, umechukua ule ambao umeona unafaa, na umeamini kwamba huu ndio mzuri na umeizidi miche yote,
“Hii ndio maana ya ndoa”
👰🏾👔
[2:40 AM, 4/29/2016] Tajieli Panga: Tuombe tuanze kipindi.

Baba yetu unayeishi juu Mbinguni. Tunaomba uwepo wako kati yetu ili tuweze kujifunza miguuni pako. Ndilo ombi langu kwa jina la Yesu. Amen
[2:40 AM, 4/29/2016] Tajieli Panga: 👫👫👫👫👫👫👫👫👫
Kipindi: kaya na familia

Mada: WAJIBU WA MUME KWA MKE WAKE

Yapo mambo ambayo baba/ mume anapaswa ayafanye kwa mke wake. Na pasipo kuyafanya hayo ndoa huwa mashakani. Mfano kumpenda mke, kumsifia, kumshukuru kwa kazi anazokufanyia, kuongea naye nk.
1. Kwanini baadhi ya akina Baba hawafanyi hayo kwa wake zao?

2. Nini ushauri wako kwa wanandoa Leo?

Karibu tujadili.
[2:53 AM, 4/29/2016] Tajieli Panga: Yapo mambo ya kuangalia kwenye hii mada ya Leo kama tulivyoona hapo juu.

Mume unapaswa kumpenda mke wako. ( waefeso 5:25) hivyo mtaweza kuishi maisha ya amani na uoendo siku zote. Wakati huo mke atakuwa anakutii (waefeso 5:22). Siku zote utamtii umoendaye. Hiyo hali huja automatically….
[2:57 AM, 4/29/2016] +255 714 431 316: Wakinababa nadhani hawafanyi hivyo wanadhani chochote kile ni hakiyao kupata…baadhi yao hufikiri hivyo etii.!!
[2:59 AM, 4/29/2016] +255 753 777 604: Wakinababa wengi wanayafanya hayo kipindi cha uchumba ila wakiisha oa wanasahau kuwa linatakiwa liwe zoezi endelevu ili kuzidi kukuzaupendo katika ndoa wanakua wameridhika nakusahau kuwa wameambiwa wawapende wake zao
[3:01 AM, 4/29/2016] Tajieli Panga: Mambo ambayo baba/ mume unapaswa kumfanyia mkeo.

1. Mpende. Mwonyeshe mke wako kuwa unampenda tena sana. Yaani mwambie hilo neno Mara kwa Mara. Tatizo ni kwamba wanaume wengi hilo neno Mara yao ya mwisho kulitamka ni pale kabisani kwenye kiapo cha ndoa. Hio ni hatari sana. Wengi hudhani kwamba akisha mwingiza huyu mke ndani maneno ya mahaba hayana nafasi tena ni kazi tu…! Hapana hapo mtakuwa mnakosea akina baba mnaosoma hii mada. Hakikisha unaendelea na maneno Yale matamu matamu kila siku mwambie mke wako nakupenda sana. Hivyo anajisikia Kumbe niko na MTU anayenijali
[3:01 AM, 4/29/2016] Tajieli Panga: Mbarikiwe sana kwa michango yenu
[3:07 AM, 4/29/2016] Tajieli Panga: Msifie mke wako.

Hapa mume unapaswa uangalie ni kipi mke wangu amekifanya na anapaswa kusifiwa. Msifie. Msifie mkeo kwamba amepika chakula kizuri na umekifurahia. Msifie maumbile aliyonayo kwamba na wewe umeridika kuwa naye. Mwonyeshe ni jinsi gani unafurahia huduma zake zote. Hapo mtaishi kwa furaha sana
[3:14 AM, 4/29/2016] Tajieli Panga: Mkumbatie na kumbusu mke wako.

Hapa napo ipo shida jamani. Mwanaume Mara ya mwisho kumkumbatia mke wake ni kwenye pozi la kupiga picha siku ile ya harusi. Hapo unategemea nn sasa mpendwa…!! Okoa ndoa yako wewe mwanaume. Tatizo ni kwamba siku hizi michepuko imezidi. Kiasi kwamba hata unaogopa kumkumbatia mke wako na kumtazama usoni ukayaangalia Yale macho Yake vizuri. Kama kuna nafsi inakusuta kwamba kuna mahali ulipita kabla hujaja nyumbani ni changamoto sana kufanya hivyo. Haitawezekana ni mpaka uwe mwaminifu kwa mke wako. Ndipo ndoa yako itakuwa na amani na salama
[3:25 AM, 4/29/2016] Tajieli Panga: Pata muda wa kuongea na mke wako.

Unapotoka Kazini zungumza na mkeo hata kwa robo saa tu. Usimwache tu kama vile ni mfanya kazi kwa nyumba. Huyo ni mke wako. Zungumza naye mambo yenu nyie wawili. Atazidi kukuheshimu. Na wewe utazidi kumpenda kila siku. Tambua thamani ya mchango wake hata katika maongezi yenu. Usidharau hoja zake. Shirikiana naye kwa kila hatua. Hio ndoa itakuwa mfano bora hata katika jamii
[3:26 AM, 4/29/2016] +255 753 930 942: 🙏🏻
[3:30 AM, 4/29/2016] +255 753 930 942: Muweke wazi mke wako, kipato chako, vitu unavopenda, kama unamajukumu mengine mfano kulea wazazi wako, au watoto wa marehemu ndugu yako. Kila kitu kifanyike kwa Uwazi na kwa Hofu ya Mungu. Ni tool muhimu pia
[3:31 AM, 4/29/2016] Tajieli Panga: Kweli kabisa @ Joseph. Tuwe wawazi katika familia zetu kwa kila jambo itatusaidia sana
[3:32 AM, 4/29/2016] +255 753 930 942: 🙏🏻
[3:36 AM, 4/29/2016] Tajieli Panga: Cheza na mke wako…

Pata muda wa kucheza na mkeo. Taniana naye mambo flani ambayo yatawafanya mfurahi pamoja. Yaani jaribu kumkeep busy mkeo aone yupo na mtu anayetambua uwepo wake pale. Wa mama wengi hupenda matani sasa wewe mume kila siku unakuja nyumbani na sura ya kazi… Kaaaah…! Acheni hizo tabia nyie akina baba. Cheka na ufurahi na mke wako. Mbona huko Kazini , vijiweni nk mnacheka na wapita njia? Kwann nyumbani usicheke na mkeo?

Weka familia yako katika mwonekano wa Upendo siku zote na wakati wote.
[3:52 AM, 4/29/2016] Tajieli Panga: Emma..📡📡📡📡
[3:55 AM, 4/29/2016] Tajieli Panga: Emma njoo na hitinisho la mada yetu ya Leo…

Nini lifanyike kwa wanandoa walioathiriwa na mazingira ya kutokuwepo kwa huduma kama hizo tulizojadili hapo juu? Nini ushauri wako kwao na kwa vijana ambao wanatarajia kuwa wanandoa siku za usoni?
[4:00 AM, 4/29/2016] Emmanuel Samuel: Napenda kuwashauri wanandoa, kila mmoja amuone meenzake ni bora kuliko yeye lakini pia wakati unapokesa kubali kukosolewa….siyo kwa sababu wewe ni baba sasa unataka umpeleke mkeo kama gari……ndoa nitofauti na na Ukurugenzi wako kazini…..
[4:01 AM, 4/29/2016] Emmanuel Samuel: Kwa wale ambao hawajaoa kama mimi, wamwombe MUNGU awapatie wenzi wema…..waachane na nadhalia binafsi za kujiwekea vigezo vyao binafsi……MUNGU kwanza vigezo vitajitosheleza
[4:06 AM, 4/29/2016] Tajieli Panga: Tuombe tufunge kipindi
[4:06 AM, 4/29/2016] Tajieli Panga: Asante BWANA kwa kipindi hiki cha kaya na familia…..tumejifunza mengi ebu tusaidie kuyafanyia kazi lakini pia tunakusihi urejeshe upendo kwa wale ambao ndoa zao zinamigogoro….tusaidie kukutazama wewe katika maisha yetu ya kila siku. Zifanye familia zetu kuwa mbingu ndogo ili ujapo kwa mara ya pili sisi na waume/wake zetu pamoja na watoto wetu tukaurithi Ufalme wako. Kwa jina la YESU KRISTO tunaomba. Amen