4/29/2016

Muumbaji wetu Mfalme vitu vyote ni vyako, ni kwa Neema yako tu ndio maana sisi tu hai hadi sasa, jina lako litukuzwe sana.

Tunakushukuru Mungu wetu, kwa upendo wa agape kwetu, tena ulisema ni upendo mkuu kiasi gani wa mtu kutoa uhai wake kwa ajili ya rafiki zake, Baba huu ni upendo wa agape.

Wewe Yesu ulitupenda ndio maana ukautoa uhai wako kwa ajili yetu, tusamehe dhambi zetu, ututakase kwa damu yako iliyomwagika pale msalabani kwa ajili ya ondoleo la dhambi. Pamoja na kwamba ulishatufia pale msalabani ukatulipia deni letu, bado tunajikwaa mara kadhaa kwa sababu ya udhaifu wetu, Baba usituache wapweke endelea kutukumbatia km vile kuku akusanyavyo vifaranga vyake chini ya mbawa zake, Yesu nasi tunajitoa wakfu muda huu tukiwa ktk chumba cha maombi tukikulilia kila mtu na haja yake, tunakuomba Yesu wewe uliyemuombezi wetu ckia na utuombee rehema ututie nguvu tusimame imara.

Wana sauti ya injili tunakuhitaji zaidi ya nuzi na jana, tafadhali Yesu jidhihirishd kwetu jwa njia ya Roho Mtakatifu ututie nguvu ili tuendelee na safari.

Wapo wagonjwa woote nawaweka mikononi mwako, wengine mafua ya muda mrefu, BP, kisukari, wengine magonjwa ambayo Bwana wewe wajua, ninakuomba uckuu ukawe ucku wa upontaji kwao, wakapone kwa jina la Yesu Kristo wa Nazareth, maana wewe ni tabibu mkuu ucyeshindwa tenda na watu wako wauone mkono wako.

Ule mkutano wa injili ujumbe unaosikika ktk viwanja vile matunda yameanza kuonekana, mavuno yaliyokomaa nayaendelee kuvunwa maana ndio wakati wake kuvunwa. Wezesha watumishi wako wakiongozwa na Roho wako miale ya nuru ya kweli ikaangaze Bunda na jina lako litukuzwe ktk vinja vile.

Wanaotafuta ajira fungua milango ajira zipatikane na watu wako wakushangilie, wanaotafuta mitaji ya biashara nao pia tenda Mungu wetu maana kwako yote yanawezekana.

Ipo ndoa mbele yetu tunawaombea heri na baraka maarusi wetu wanapoendelea kuisubiria cku yao ya kihistoria nakusihi watunze ukiwapatia afya tele na amani mioyoni mwao, lkn baraka za ndoa zikaandamane nao, tukiwatakia ndoa ambayo wengi watavutwa kwa ukarimu wao, wasisahau kuwafadhili wageni maana waweza kuwafadhili malaika pasipo kujua.

Wanaotafuta wacbumba, hawa nao wabariki wapatie wachumba wenye hofu ya Mungu wakakutukuze wewe Mungu wa mbinguni, lkn wapo ambao tayari ni wachumba imarisha uchumba wao ukastawi vema na cku nyingine nao tukawaombee baraka za ndoa, lkn wapo wanao lia sababu wameachwa na wenzi wao, leta faraja kwao ukiwatazamisha kuwapatia wachumba wengine kwa wakatj unaofaa.
Mungu wetu, yote haya tunayaweka mikonnoni mwako, lkn tunakusihi Roho wako ndiye awe kiongozi wetu daima akituelekeza kukutumainia wewe akitufunulia yaliyo mapenzi yako kwetu, nasi tukayaishi tukiwa fundisha na wengine wasiokujua wewe.

Ni imani yetu unatupenda na umesikia maombi yetu na utajibu sawasawa na mapenzi yako kwa maana ndivyo tuombavyo ktk jina la Baba, Mwana na Roho Mtakatifu Amina.