Maombi 4/28/16

MAOMBI YA ASUBUHI (Alhamisi 4/28/16)

 1. Saa 11-12 (Maombi ya binafsi/ Nyimbo za Injili)
 2. Saa 12-1 (Maombi ya Jumla kama Familia ya Sauti Ya Injili)
 3. Mada Ya Leo = IMANI,UPENDO, HAKI YA KRISTO

 

SIFA & SHUKRANI: Mshukuru MUNGU kwa:

 1. Baraka tele & uaminifu wake kwetu
 2. Tabia yake isiyobadilika
 3. Msamaha wa dhambi zetu
 4. Nafasi nyingine ya Uhai Leo.

 WAGONJWA WETU

 1. Sisi sote tu wagonjwa wa kiroho, hivyo tuombee ili Tabibu Mkuu atuponye
 2. Jamani naomba mniombee nina mafuwa natumia dawa na wala hayaponi ni miaaka miwili sasa
 3. Mama yake Barbara – ana maumivu makali sana ya mguuni yapata sasa miaka 25.
 4. Dada Tatu Mkomagi.
 5. Dada Mercy Swai
 6. Rafiki yake Sule Mwassy (Mable) amepata depression, amezimia akakimbizwa Hospitali.
 7. Andrew Songa, anaumwa sana, na amekimbizwa Hospitalini.
 8. Debora & Mwanae
 9. A.B.M,Mwanza-TZ. (dada yangu: anaumwa sana. Tumwombee)
 10. A.B.M,Mwanza-TZ. (mama amekua akihudhuria cliniki: HTN & PUD, at BMC, sasa anasumbuliwa na CHF, Congestive Heart Failure.

MAHITAJI MENGINE / CHALLANGES

Financial Breakthrough

 1. Olerutto,
 2. Job
 3. Cyprian Nyaga
 4. George
 5. Munyaradzi

JOBS (AJIRA)

 1. Namoonga Oreen
 2. Joseph Oruko
 3. Job
 4. Brother na Stashahada inProcurement na usambazaji

UKUAJI WA KIROHO

 1. Cyprian Nyaga
 2. Munyaradzi

FAMILIA

 1. Dada na kuvunjika moyo
 2. Kaka na kuvunjika moyo
 3. Ibrahim na Lydia
 4. Familia ya Pamella kwa ajili ya
  1. fedha (uchumi wao)
  2. Ukuaji wa kiroho,
  3. umoja katika familia yao,
  4. mapepo wachafu, nk.

KAMPENI ZA UINJILISTI (Evangelistic)

 1. Bunda (Aprili 24 – Mei 14)
 2. Baba Elsies – kundi jipya huko Nyazura Kenya
 3. Kikundi kipya cha “Shule ya Sabato” kilichofunguliwa na “Calvary Ministers” huko Kenya.

CHANGAMOTO ZINGINE

 1. Oleruttos – (maombi ya chuo)
 2. Edwin kushinda visa (Greencard ya USA).
 3. Harusi ya Mathania Machuma na Ruth Nyabuti (Mei 1)
 4. Patrick Michael ili kufikia malengo yake
 5. Dada Dora (internet connections)
 6. Dreda Vorsters – (Amani, Usalama Na Ulinzi)
 7. Advocate Kinya -(Maombi ya kimya kimya)
 8. Ndugu yetu mmoja hapa (Swahili group) ambaye hana amani katika eneo lake la makazi. Anahitaji fedha za mahitaji mengine. Mungu amfungulie njia/
  • Kokotoni Sabato shule kufunguliwa na Calvary Mawaziri kwa ukuaji wa idadi na neno la Mungu

USHUHUDA WA LEO

(Mr…)“Nashukuru Mungu amejibu nimepaya ada nacte na nimesha apply”

(Job) “I can testify mungu hujibu maombi. Tuliombea Siz Dorah sasa hivi anaweza kuwa kwa mtandao”.

AHADI YA LEO: –  (Isaya 1:19-20)

 • 19 Kama mkikubali na kutii mtakula mema ya nchi;
 • 20 bali kama mkikataa na kuasi mtaangamizwa kwa upanga; maana kinywa cha Bwana kimenena haya.

 

TUNAKARIBISHWA KUFANYA YAFUATAYO:

 1. Kutoa ushuhuda wa Matendo makuu ya MUNGU
 2. Kuweka Audios za Maombi (Sauti), ama Kuandika.
 3. Kutujulisha kama OMBI LAKO limejibiwa (ili tupunguze list)
 4. Kushiriki katika kipindi kingine cha Maombi Ya Jioni (Saa 3 Usiku)

Karibuni katika CHUMBA CHA MAOMBI ili tushiriki ibada ya maombi pamoja.


 

 

 

CHUMBA CHAMAOMBI

 • Mhudumu: Mr. Advocate Kinja
 • Tuombe tafadhali

Haleluya Baba na Mungu wetu Muumbaji wa mbingu na nchi, tunalisifu na kulitukuza jina lako.

Tunasema asante kwa kua umekua nasi tangu kulivyo pambazuka asbh hadi masaa haya, umekua mwema kwetu, hata pale tulipokutenda dhambi hukutuacha wapweke, bali umeendelea kuwa nasi, Baba jina lako litukuzwe milele zote.

Wewe ni Mungu mwenye nguvu, kwan umehakikisha unapigania uhai wetu, hata pale ibilisi alipojaribu kutunyemelea atuangamize, wewe umetupigania na kutupatia nafac hadi sasa, tu wazima wa afya.

Mumbaji wetu unaetupenda, tunakuja kwako kwa jinsi tulivyo tuwenye dhambi tusiostahili, lkn kwa damu ya Yesu Kristo iliyomwagika pale msalabani kwa ajili ya ondoleo la dhambi, nasi Bwana tunakuja ututakase kwayo, tupate takasika na kusafishwa na udhalimu wote.

Tazama ktk group hili la sauti ya injili, sisi tu wagonjwa wote, wanjwa wa kiroho na kimwili, hivyo tunakuja kwako wewe uliye tabibu mkuu, tena Yesu mwenye huruma, unaetuletea faraja Yesu mwokozi wetu, tunakuja kwako tugange kila mtu sawasawa na ugonjwa alionao.

Magonjwa ya kimwili nyoosha mkono wako uwaguse nao wapone, haijalishi wamesumbulia kiasi gani, haijalishi wamezunguka mahospital mengi namna gani, wewe ni tabibu usie tumia dawa zilitengenezwa kwa uwe wa kibinadamu, bali kwa neno moja tu, wagonjwa wote wanapona, lkn kwa mguso wa imani wanapona pia, hivyo baba tenda kwa watu wako, maana wanateseka kwa muda sasa, km ilivyokuwa kwa yule mama alipogusa pindo lako tu, akapokea uponyaji, Yesu wangu, mgonjwa yule kwa kusoma ujumbe huu, na kwa njia ya Roho wako Mtakatifu nakusihi mtu fulani akapone kwa jina la Yesu wa Nazareth.

Tazama tupo wagonjwa wa kiroho, cc twajiona tu wazima lkn tunatembea tukiwa marehemu tumekufa kiroho, Yesu wangu tufufue ktk kifo hiki cha kiroho, tupatie mioyo iliyopondeka ili tuweze kuickia sauti yako ya upole ikipenya ndani ya mioyo yetu, ikalete badiliko halisi maishani mwetu, Mfalme wa amani tunakuhitaji sana kila wakati, uctuache wapweke maana cc wenyewe hatuwezi tushike mkono Yesu, yule mwovu kn simba angurumae akimtafuta mtu ammeze, tusaidie tuwezeshe tuweze kuvuka salama, ng’ambo ya mto mambo ni sawasawa, ng’ambo ya mto mambo ni barabara, tusaidie tushinde.

Wapo wanaohitaji ada jidhihirishe kwako watimizie sawasawa na mapenzi yako maana tumaini lao lipo kwako, wasiabike maana wamejenga imani yao kwako, hivyo Bwana hakuna aliekutumaini akaaibika kamwe.

Ipo ndoa tarehe 01/05/2016 tunawaweka mikononi mwako maarusi wetu, tangulia kila jambo, likayendeke kwa utukufu wa jina lako, maana wewe ndie muasisi wa ndoa hii takatifu kwa wazazi wetu wa kwanza, wape afya, amani upendo na mshikamano, ukawe ngao na Msaada kwao, kila lililo gumu wanapolileta kwako, maulisema je ni jambo gani usiloliweza??? Wanapolileta litatue na wala wactumie akili zao bali wakutangulize kwa kila jambo.

Upo mkutano wa injili unaoendelea kule Bunda Bwana tunauweka mikononi mwako, agizo lako tuenende ulimwenguni tukaihubiri injili kwa mataifa yote, ndiyo huduma inafanyika pale Bunda, wapatie afya njema wooote wanaoendelea kusimamia na kuendesha mahubiri ktk eneo lile, na Roho wako Mtakatifu yeye ajuae kusema na mioyo ya watu wako, kwa wakati wake ikiwa mavuno yamekomaa na yavunwe lkn yale ambayo Baba unaona bado yaandae ili kadiri mvua ya Roho Mtakatifu inavonyeshea ikawaandae nao pia kwa ajili ya kukulaki mawingu ujapo mara ya pili.

Baba, baada ya hayo yote tunakungojea uje utuchukue twende kwetu juu mbinguni, maana hapa duniani cc ni wapitaji tu, cc wote wana sauti ya injili, popote ulimwenguni tulipo tuandae kwa ajili ya kuuthi uzima wa milele, na tutakapokombolewa tukutane kule tukielezana habari nyingi.

Lkn lkn Yesu kupitia vipindi hivi ktk group la sauti ya injili mtu fulani akaokolewe, cku moja akashuhudie kuwa kuwepo ktk kundi hili hakika nmemuona Yesu ndani yangu, ikiwa ni mapenzi yako Yesu tuingie sote mbinguni.

Baba, tunajua unatupenda na hutatuacha kwamwe, hivyo tunayaweka yote mikononi mwako kwani ndilo ombi letu kupitia kwa Yesu Kristo aliye Bwana na mwokozi wetu Amina.