Karibu katika Sauti Ya Injili SDA

Lengo la Sauti Ya Injili SDA ni kama ifuatavyo:

  1. Kuandaa Miongozo ya Kujifunza Biblia – (Bible Study Guides) katika kila sura ya Biblia. Miongozo hii bado inafanyiwa kazi kwa sasa; tutaileta humu kazi hiyo itakapokuwa imekamilika. 
  2. Kuandaa Mafundisho Makuu ya Biblia (Doctrines); mifululizo ya Masomo, Dhima, na Mada mbalimbali katika Biblia.
  3. Kuhubiri neno la MUNGU kila inapowezekana.
  4. Kusoma dhahiri kutoka “Katika Kitabu, Katika Torati Ya Mungu, Kwa Sauti Ya Kusikilika”; na Kutoa Maana Yake, ili kuwasaidia watu wa MUNGU, Kuelewa na Kufahamu yaliyosomwa humo”. (Neh. 8: 8)
  5. Kutoa nakala za Neno la Uzima kwa kila Taifa, Kabila, Lugha na Jamaa, ulimwenguni kote.
  6. Kurejesha watu kwenye Wito wa mwisho wa Muumba wetu: Ujumbe wa Malaika Watatu wa Ufunuo 14:7-14.
  7. Kuandaa watu kukata shauri kwa ajili ya kumlaki Bwana na Mwokozi wao YESU KRISTO.

Kwa matarajio makubwa , tunatamani kuwa miongoni mwa kundi linalotajwa katika Injili ya Isaiah 25:9, Asubuhi ile njema, wakati sauti nyingi za shangwe zitapiga kelele zikisema “Tazama, huyu ndiye MUNGU wetu, Ndiye tuliyemngoja atusaidie; Huyu ndiye BWANA tuliyemngoja, Na Tushangilie na Kuufurahia wokovu wake.”

Ombi letu ni Hili: Kila msomaji/ msikilizaji atapata “Sauti ya Injili” humu, yaani, Sauti ya upole ya Yesu Kristo ikinena nasi, tuachane na dhambi, tutubu, tukate shauri, ili turejeshwe Kwake, tukiandaliwa kwa ajili ya ufalme Wake.

“Kila aliye na sikio, na alisikie Neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa” (ufunuo 3:22) – [1] Kulielewa “Neno la kweli” (2 Tim. 2:15); [2] Kulikubali “Neno la Kristo likae kwa wingi ndani yenu” (Kol. 3:16); [3] Kuliruhusu Neno Lake likae akilini mwenu, hivyo, kuleta uaminifu mkuu na utii mbele za Mungu—“ kwa kadiri mwonavyo siku ile kuwa inakaribia”(Ebr. 10:25). Amina.

UFAFANUZI: Tovuti hii si ya kanisa  au  dhehebu jipya, badala yake, ni huduma ya kujitegemea ya kiadventista, inayoelekeza watu katika kweli zote za Biblia, ikiwemo ukweli kuhusu Sabato ya Siku ya Saba (Kutoka 20:8); Ujumbe wa Malaika watatu (Ufunuo 14:6-12); n.k., kulingana na utafiti wa kina wa kweli za Biblia. Bwana akubariki sana unapotembelea jumbe zitakazowekwa humu tena na tena.