61-001 Washirika wa Tabia ya Uungu

2 Petro 1:1-4

 • 1 Simoni Petro, mtumwa na mtume wa Yesu Kristo, kwa wale waliopata imani moja na sisi, yenye thamani, katika hali ya Mungu wetu, na Mwokozi Yesu Kristo. 2 Neema na iwe kwenu na amani iongezwe katika kumjua Mungu na Yesu Bwana wetu. 3 Kwa kuwa uweza wake wa Uungu umetukirimia vitu vyote vipasavyo uzima na utauwa, kwa kumjua yeye aliyetuita kwa utukufu wake na wema wake mwenyewe. 4 Tena kwa hayo ametukirimia ahadi kubwa mno, za thamani, ili kwamba kwa hizo mpate kuwa washirika wa tabia ya Uungu, mkiokolewa na uharibifu uliomo duniani kwa sababu ya tamaa.

 

 

MWITO WA KUWA WASHIRIKA WA TABIA YA UUNGU

 1. 61-001
 2. [Neno Kuu: πιθυμία (epithymia) = Tamaa]
 3. Bofya hapa http://tgvs.org/archives/1919

 

SIFA ZA MWANDISHI

 1. Utangulizi
 2. Simoni Petro
 3. Mtumwa wa Yesu Kristo
 4. Mtume wa Yesu Kristo

SIFA ZA WALENGWA

 1. Wale waliopata Imani moja na sisi
 2. Imani Yenye Thamani
 3. Katika hali ya Mungu wetu, na Mwokozi Yesu Kristo.

SALAAMU KWA WATAKATIFU

 1. Neema na iwe Kwenu
 2. Amani iongezwe Kwenu
 3. Katika kumjua Mungu na Yesu Bwana wetu.

UWEZA WAKE WA UUNGU WAKE

 1. Uungu wake umetukirimia vitu vyote
 2. Vipasavyo UZIMA na UTAUWA

MWITO WA KUWA WASHIRIKA WA TABIA YA UUNGU

 1. Mwito wa kumjua Yeye
 2. Tumeitwa kwa ajili ya utukufu Wake
 3. Tumeitwa kwa wema Wake Mwenyewe.
 4. Tumekirimiwa ahadi kubwa mno, za thamani.
 5. Tumeitwa kuwa washirika wa tabia ya Uungu Wake.
 6. Tunaokolewa na uharibifu uliomo duniani
 7. Tunakuwa washindi dhidi ya “Tamaa”.

MWITO WA LEO

2 Yohana 15-17 (Msipende Dunia)

 • 15 Msiipende dunia wala mambo yaliyomo duniani. Kama mtu akiipenda dunia, hawezi kumpenda Baba. 16 Maana vitu vyote vil ivyomo duniani, yaani, tamaa za mwili, tamaa ya vitu vinavyoone kana kwa macho, na kiburi kiletwacho na mali, vyote hivi havitoki kwa Baba bali hutoka ulimwenguni. 17 Nayo dunia inapita na tamaa zake zote zinapita, lakini mtu anayetimiza mapenzi ya Mungu huishi milele.

TUFANYE NINI BASI?

Wagalatia 5:16-17

 • 16 Kwa hiyo nasema, mruhusuni Roho atawale maisha yenu na msitafute kutimiza tamaa za mwili. 17 Kwa maana tamaa za mwili hushindana na Roho; na Roho hushindana na tamaa za mwili. Roho na mwili hupingana, na kwa sababu hiyo ninyi hamwezi kufanya yale mnayotaka.

 

BWANA ATUBARIKI SOTE